Kila Rais wa Tanzania alipoondoka aliacha nini kwa awamu iliyomfatia?

Kila Rais wa Tanzania alipoondoka aliacha nini kwa awamu iliyomfatia?

kwa marais wote JPM kwa infrastruture kwa kweli nilimpa mkono , sema jamaa alikuwa kichwa kigumu , kikwete naye aliacha legacy ya wizi sana sema enzi zake pesa ilikuwa na mzunguko sana , wote kwa issue la deni
"Infrastructure" ipi au zipi unazoongelea za mwendazake?
 
Kichwa cha habari kimeeleweka.

Kwa faida ya wengi, waliokuwepo na wasiokuwepo awamu zilizopita. kila mmoja wetu ana mtazamo wake tofauti na wa mwengine, tujadili mafanikio na madudu ya awamu zilizopita.

Binafsi nashukuru, nimeziishi awamu kadhaa za Tanganyika kuanzia tupo utawala wa Muingereza chini ya Umoja wa Mataifa.

Naikumbuka Tanganyika ya Muingereza kwa mbali, naikumbuka Tanganyika ya utawala wa Nyerere kwa ukaribu zaidi.

Kwa kuwa viongozi waliotuongoza ni wanaadam kama sisi, hawakosi mema yao na mapungufu yao, tuyajadili waliotuwachia.

Hata kama hukuwepo na umeyasoma au umehadithiwa tu, rukhsa kuyaleta ili tuchekeche na tuchambuwe mchele, chenga na chuya.

Bila kufahamu wapi tulipotoka na wapi tupo itakuwa vigumu kuelewa wapi tunaelekea.

Tujadili.
Tawala zote za Ccm huachiana matatizo tu.
 
Umasikini,madeni,na ongezeko la deni la taifa.
Kumbuka wakati wa Uhuru Dola moja ilikua sawa na sh 60 Leo ni 2500.Jibu unalo
Hapana, haikuwa shillingi 60, nilikuwepo, kwanza wakati wa uhuru Dollar ilikuwa haiongelewi kabisa, imeanza kuongelewa baadae sana, tulikuwa tunaongea Paundi (Sterling Pounds).

nakumbuka nilipoanza kuifahamu Dollar, ilikuwa ni 1 Dollar = Shillingi 3. Wakati huo Poung 1 Shillingi 7.
Dollar ilianza kupata umaarufu baada ya azimio (bovu) la Arusha 1967.

Nasema bovu kwa sababu ndipo umasikini wa kufa watu ulipoanzia.
 
Asante kwa kusahihisha nilitaka kusema sh 6.
Kosa la mwalimu ni kuwachukia wakoloni na mazuri yao
 
Nyerere==aliacha kila kitu kikiwa intact, alipambana na umaskini na hakuumaliza
Mwinyi===aliacha kila kitu kikiwa intact, alipambana na umaskini na hakuumaliza
Mkapa===aliuza kila kitu zikiwemo rasilimali; alitujengea uwanja wa mpira
Kikwete===alipambana na umaskini na hakuumaliza, alituachia vyuo vikuu vipya zaidi ya 40 na shule nyingi mpya za Sekondari za nyongeza
...................
etc
mkapa aliuza kilakitu zikiwemo rasilimali???
kikwete kajenga vyuo zaidi ya 40 nitajie vitano tu.
 
Nachojua kwenye awamu ambazo rais wa JMT toka upande wa Zanzibar (awamu ya pili na ya sita) basi marais hao wametuachia moja ya legacy zifuatazo:
1. Wali/wameteua mtu kwenye cheo cha Naibu Waziri Mkuu, (hakipo kwenye katiba)
2. Wameuza ardhi sehemu ya Tanganyika kwa Waarab kwa umiliki wa kificho
3. Kuteua Wazanzibar kwenye vyeo vya DC bara kitu ambacho kwa Mtanganyika hakiwezekani kwa huko Zanzibar
 
SGR , Airports na kununua ndege , barabara nyingi ikiwemo ya kwenda kwangu nyumbani ifakara , sema ujuaji na kichwa ndo zilikuwa hinderance kubwa kwake , yule jamaa angejua kutuliza kichwa askize maoni angefanya mengi ndani ya miaka mitano
SGR aliukuta mradi upo tayari, alichofanya yeye ni kupiga chini Wachina waliokuwa wauanzishe na kuwaleta Waturuki. Ushahidi:

Mradi wa kuifufua ATC pia ulikuwa tayar on ythe pipelinei, Kikwete alishatembelea mpaka Boeing na Canada ili zianze kuletwa. Hii ni miradi amabayo Magufuli kaikuta na kaondoka bila kuimalizia, kwa ujuwaji wake. Ushahidi:

Kwa ushahidi huo, wa hapahapa JF, mwendazsake hakuanzisha miradi ya SGR na Ndege. Aliianzisha Kikwete.
 
Mtazamo wangu...

Nyerere
Positive: uzalendo, utaifa na diplomasia kimataifa
Negative: uchumi dhaifu

Mwinyi
Positive: uhuru na demokrasia
Negative: ufisadi na uuzwaji wa maliasili za nchi, udini

Mkapa
Positive: uchumi imara na diplomasia kimataifa
Negative: ufisadi

Kikwete
Positive: demokrasia na diplomasia kimataifa
Negative: rushwa na ufisadi

Magufuli
Positive: uchumi imara na miundombinu bora, uzalendo
Negative: demokrasia na diplomasia dhaifu, ukanda na ukabila

Samia
Positive: diplomasia kimataifa na demokrasia
Negative: ufisadi na uuzaji wa rasilimali za nchi, udini na uzanzibari
 
mkapa aliuza kilakitu zikiwemo rasilimali???
kikwete kajenga vyuo zaidi ya 40 nitajie vitano tu.
Hapana; the issue is simple.
Orodhesha tu vyuo vikuu vilivyokuwepo wakati Mkapa anaondoka madarakani
Orodhesha pia viwanja vya mpira vilivyokuwepo wakati anaingia madarakani
 
Nyerere alituachia Umoja wa kitaifa.

Mwinyi alitufungulia milango ya nchi.

Mkapa alituachia ubinafsishaji na matokeo yake.

Kikwete alituachia mtandao mpana wa barabara nchini.

Magufuli alituachia sheria za kimageuzi za rasilimali na miradi mikubwa ya kimkakati.

Samia bado namsoma.
 
Nyerere==aliacha kila kitu kikiwa intact, alipambana na umaskini na hakuumaliza
...................
etc
Hapana, si kweli nilikuwepo.

Nyerere aliiacha Tanzania ikiwa ni nchi ya mwisho kwa umasikini duniani. Aliiwacha hata chakula inabidi tukae foleni, wakati yeye aliipokea kwa Mkoloni ikiwa ni nchi ya kwanza katika Afrika inayosfirisha mazao ya kilimo.

Unajuwa kuwa Tanzania Nyerere alituwacha chakula hatuna, mafuta hatuna, akiba benki hatuna.

Umri wa kutenegemea kuishi mtanzania(life expectancy) wakati wa nyerere ulikuwa haufiki miaka 45.

Yule mzee usisikie anavyopambwa, alituwachia na mabalaa ya kila kitu Kawacha nchi foleni kila kitu foleni.

Kwa mtazamo wangu, Nyerere hakuwa na baraka za Mwenyezi Mungu kabisa katika kipindi chake. Majanga mwanzo mwisho.

Naamini huwezi kudhulumu watu Mwenyezi Mungu akakubariki.
 
Kichwa cha habari kimeeleweka.

Kwa faida ya wengi, waliokuwepo na wasiokuwepo awamu zilizopita. kila mmoja wetu ana mtazamo wake tofauti na wa mwengine, tujadili mafanikio na madudu ya awamu zilizopita.

Binafsi nashukuru, nimeziishi awamu kadhaa za Tanganyika kuanzia tupo utawala wa Muingereza chini ya Umoja wa Mataifa.

Naikumbuka Tanganyika ya Muingereza kwa mbali, naikumbuka Tanganyika ya utawala wa Nyerere kwa ukaribu zaidi.

Kwa kuwa viongozi waliotuongoza ni wanaadam kama sisi, hawakosi mema yao na mapungufu yao, tuyajadili waliotuwachia.

Hata kama hukuwepo na umeyasoma au umehadithiwa tu, rukhsa kuyaleta ili tuchekeche na tuchambuwe mchele, chenga na chuya.

Bila kufahamu wapi tulipotoka na wapi tupo itakuwa vigumu kuelewa wapi tunaelekea.

Tujadili.

1. Aliuza rasilimali.
2. Alijijenga kwao.
3. Marafiki zake aliwaacha serikalin.
4. Alikua tajiri wa kutupwa.
5. Matabaka.

Aliacha:

1. Hakuba hela hazina.
2. Maumivu kwa vyama vya upinzani.
3. Makovu kwa wa Tanzania.
4. Maadui wake jela.

Anakoelekea:

1. Kuishi maisha kitajiri.
2. Kutokuwa na amani.
3. Kujuta.
 
Umasikini,madeni,na ongezeko la deni la taifa.
Kumbuka wakati wa Uhuru Dola moja ilikua sawa na sh 60 Leo ni 2500.Jibu unalo
Eti dola mbili kwa sasa ni buku tano... hapa bongo kuna mtu anafanya budget ya siku nzima maisha yasogee kwa siku kwa shilingi elfu tano ("5000") ya kitanzania, huko kwao hiyo dola mbili hata kinywaji hupati. Afrika shikamoo! 😀😅😅😅🙌🏾
 
Nyerere alituachia Umoja wa kitaifa.
Hii ni propaganda inayotumika sana.

Nyerere hakuikuta nchi hii ikiwa haina umoja wa kitaifa. Hata yeye alipotoka kwao kwenda Tabora alikuta watu wa kila mkoa na kabila wanaishi kwa amani, hata alipokuja Dar lipokelewa na wenyeji wa Dar, ukoo wa Sykes, namely, Abdul Wahid Sykes alimpokea kwa heshima na taadhima na akamtambulisha mjini, bila tatizo lolote.

Hiyo pekee inaonesha kuwa hii nchi haikuwa na tatizo la umoja wa Kitaifa hata kabla ya uhuru. Matatizo yetu yallikuwa mengine kabisa, hilo hapana.
 
Back
Top Bottom