WALOLA VUNZYA
JF-Expert Member
- Nov 20, 2020
- 7,154
- 7,155
1.Nyerere alituachia:-Kichwa cha habari kimeeleweka.
Kwa faida ya wengi, waliokuwepo na wasiokuwepo awamu zilizopita. kila mmoja wetu ana mtazamo wake tofauti na wa mwengine, tujadili mafanikio na madudu ya awamu zilizopita.
Binafsi nashukuru, nimeziishi awamu kadhaa za Tanganyika kuanzia tupo utawala wa Muingereza chini ya Umoja wa Mataifa.
Naikumbuka Tanganyika ya Muingereza kwa mbali, naikumbuka Tanganyika ya utawala wa Nyerere kwa ukaribu zaidi.
Kwa kuwa viongozi waliotuongoza ni wanaadam kama sisi, hawakosi mema yao na mapungufu yao, tuyajadili waliotuwachia.
Hata kama hukuwepo na umeyasoma au umehadithiwa tu, rukhsa kuyaleta ili tuchekeche na tuchambuwe mchele, chenga na chuya.
Bila kufahamu wapi tulipotoka na wapi tupo itakuwa vigumu kuelewa wapi tunaelekea.
Tujadili.
a.Umoja na Mshikamano
b.Uhuru wa kweli
c.Lugha ya Kiswahili
d.Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
e.Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya 1977
2.Mwinyi alituachia
a.Uhuru wa kweli
b.Mfumo wa Vyama vingi vya siasa
c.Deni kubwa la Taifa
d.Ndiyo wakati Watanzania wengi walijenga sana
e.Mitumba na Biashara ya Minada
3.Mkapa alituachia:-
a.Barabara safi zinazounganisha mikoa yote
b.Taasisi mbalimbali imara kama vile TRA,TCRA,TAKUKURU,TASAF nk.
c.Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pale Dodoma
d.Uwanja mkubwa wa mpira Afrika Mashariki na Kati
e.Alifuta kodi ya Kichwa na kodi mbali mbali za Halmashauri zisizoeleweka.
4.Kikwete alituachia:-
a.Barabara safi zinazounganisha mikoa yote ya Tanzania
b.Vyuo vikuu mbalimbali Tanzania
c.Gharama za maisha zikiwa katika hali nzuri Tanzania kuliko wakati wowote ule.
d.Nidhamu mbovu za Watumishi na viongozi mbalimbali Serikali
e.Bunge lenye nguvu na mvuto
5.Magufuri alituachia:-
a.Ndege
b.Madaraja makubwa kama vile Kigamboni na Busisi
c.Ujenzi wa SGR
d.Ukabila na ukanda
e.Watu wasiojulikana
6.Mama Samiah ametuletea:-
a.Umoja na mshikamano uliopotea awamu ya tano
b.Uzanzibar na Utanganyika
c.DP World
d.Udini
e.Utegemezi