Kila Rais wa Tanzania alipoondoka aliacha nini kwa awamu iliyomfatia?

Kila Rais wa Tanzania alipoondoka aliacha nini kwa awamu iliyomfatia?

MJERUMANI
1. Reli ya Kati
2. Ikulu ya Dar Es Salaam
3. Bandari

Mjerumani nakubali alituwachia reli ya kati ambayo mpaka leo ipo.

Bandari na Ikulu alizikuta, hakuziwacha yeye.

Ikulu ndipo lilipoanzia jina Dar Es Salaam. Tazama uzi huu:

Kichwa cha habari kimeeleweka.

Kwa faida ya wengi, waliokuwepo na wasiokuwepo awamu zilizopita. kila mmoja wetu ana mtazamo wake tofauti na wa mwengine, tujadili mafanikio na madudu ya awamu zilizopita.

Binafsi nashukuru, nimeziishi awamu kadhaa za Tanganyika kuanzia tupo utawala wa Muingereza chini ya Umoja wa Mataifa.

Naikumbuka Tanganyika ya Muingereza kwa mbali, naikumbuka Tanganyika ya utawala wa Nyerere kwa ukaribu zaidi.

Kwa kuwa viongozi waliotuongoza ni wanaadam kama sisi, hawakosi mema yao na mapungufu yao, tuyajadili waliotuwachia.

Hata kama hukuwepo na umeyasoma au umehadithiwa tu, rukhsa kuyaleta ili tuchekeche na tuchambuwe mchele, chenga na chuya.

Bila kufahamu wapi tulipotoka na wapi tupo itakuwa vigumu kuelewa wapi tunaelekea.

Tujadili.
Sasa wewe hapa umechangia kitu gani, kama siyo mada za kichokonozi tu?

Hii mada ni ngumu kuliko uwezo wako na unajua unachotafuta hapa ni mlengo ule ule wa siku zote.

Anza wewe uliyeyaona ya awamu zote, halafu sisi wengine tutafuatia na historia tuliyoisoma kama ile ya wazee wa Kariakoo!
 
Kichwa cha habari kimeeleweka.

Kwa faida ya wengi, waliokuwepo na wasiokuwepo awamu zilizopita. kila mmoja wetu ana mtazamo wake tofauti na wa mwengine, tujadili mafanikio na madudu ya awamu zilizopita.

Binafsi nashukuru, nimeziishi awamu kadhaa za Tanganyika kuanzia tupo utawala wa Muingereza chini ya Umoja wa Mataifa.

Naikumbuka Tanganyika ya Muingereza kwa mbali, naikumbuka Tanganyika ya utawala wa Nyerere kwa ukaribu zaidi.

Kwa kuwa viongozi waliotuongoza ni wanaadam kama sisi, hawakosi mema yao na mapungufu yao, tuyajadili waliotuwachia.

Hata kama hukuwepo na umeyasoma au umehadithiwa tu, rukhsa kuyaleta ili tuchekeche na tuchambuwe mchele, chenga na chuya.

Bila kufahamu wapi tulipotoka na wapi tupo itakuwa vigumu kuelewa wapi tunaelekea.

Tujadili.
Wameicha nchi inaitwa Tanzania. Pamoja na mapungufu yao, ujuaji wa baadhi yao, usomi na hekima iliyopindukiwa ya wengine, lakini hakuna hata mmoja aliyetugawa kama vipande vya shekeli.
Nchi yetu ilikaa ikawa nchi ambayo mambo ni bulibuli 😂 😂 😂 😂

Nashukuru wewe hujawahi kuwa Rais na haitakaa itokee...utatuchinja wote ambao hatusomi kitabu chako. Sijui ni kitabu gani😂😂😂😂😂
 
Mjerumani nakubali alituwachia reli ya kati ambayo mpaka leo ipo.

Bandari na Ikulu alizikuta, hakuziwacha yeye.

Ikulu ndipo lilipoanzia jina Dar Es Salaam. Tazama uzi huu:

Ni kweli walimiki wa Ikulu walikuwa waislamu? Na wamiliki wa bandari je? Kuna watu kichwani kumeota matango😂😂😂😂😂
 
Nijuavyo, miundo mbinu alituwachia Kikwete, hakuna awamu iliyojikita kwenye miundombinu zaidi ya awamu ya Kikwete.

Magufuli aliikuta miradi yote, nijuavyo miundombinu ya barabara za mwendazake ni ile ya moroccco - Mwenge, au kuna nyingine?
😂😂😂😂😂😂😂😂😂..hata bwawa la Nyerere, Ikulu ya Chamwino na ndege za ATCL alituachia yeye pia
 
Nyerere==aliacha kila kitu kikiwa intact, alipambana na umaskini na hakuumaliza
Mwinyi===aliacha kila kitu kikiwa intact, alipambana na umaskini na hakuumaliza
Mkapa===aliuza kila kitu zikiwemo rasilimali; alitujengea uwanja wa mpira
Kikwete===alipambana na umaskini na hakuumaliza, alituachia vyuo vikuu vipya zaidi ya 40 na shule nyingi mpya za Sekondari za nyongeza
...................
etc
It does make sense...kuangalia kitu kwa mapana yake, na sio kwa dini aliyotoka
 
Nijuavyo, miundo mbinu alituwachia Kikwete, hakuna awamu iliyojikita kwenye miundombinu zaidi ya awamu ya Kikwete.

Magufuli aliikuta miradi yote, nijuavyo miundombinu ya barabara za mwendazake ni ile ya moroccco - Mwenge, au kuna nyingine?
Kumbe unaongelea DAR tu au wewe hujawahi kutoka nje ya Daslam! nenda Tabora-Mpanda ukaangalie mkeka ule
 
Sikudhania kama Faiza ni mtu mwenye umri mkubwa kiasi hiko, baadhi ya maudhui yako hapa jukwaani yanakuweka kiwango Cha kijana mwenye upeo mdogo lakini kumbe ni kinyume chake.
😂😂😂😂😂😂😂. Ni kuvurugwa tu. Mtu mwema anaweza kugeuka mganga wa kienyeji au Pastor fake wa kanisa
 
Ni kweli walimiki wa Ikulu walikuwa waislamu? Na wamiliki wa bandari je? Kuna watu kichwani kumeota matango😂😂😂😂😂
Bandari zote za Mashariki ya Afrika zilikuwa za wenye wa Mashariki ya Afrika, walikuja Waarabu wakaendeleza, waalikuja Waajemi wakaendeleza, Walikj aWareno, Wajerumani, Waingereza, wamezikuta, wamefanya waliyofanya wakaziwacha kama walivyozikuta.

Hata neno "Bandari" linatokana na Kiajemi.
 
Umasikini,madeni,na ongezeko la deni la taifa.
Kumbuka wakati wa Uhuru Dola moja ilikua sawa na sh 6 Leo ni 2500.Jibu unalo
Hapana. Dola 1 ilikuwa sh 5. Na ilikaa hivyo mpaka mwishoni mwa miaka ya 1970.
 
Nyie Faiza hamumjui vzuri. Nia yake kwenye huu uzi ni kuonesha na kupangua hoja zenu kuwa hayo mnayowaza kuanzia Nyerere, Mkapa, na Magufuli si kitu dhidi ya mnaowabeza yan Mwinyi, Kikwete na Samia. Atawapeleka puta sana
 
Tunafaham uwezo na matokeo ya marais waliowahi kuitawala JMT . Jpm alikuta miradi mingi on papers !!! Tena mingne toka enzi za nyerere mfano lile bwawa la kufua umeme (stiglers) pale rufiji , upanuzi wa termina 3 JNIA jengo la abiria awamu ya nne ilikuwa ngonjera tu, jamaa kaingia fasta kakamilisha zaidi ya bilion 500 . Na upande wa usafiri wa anga alikuta ngonjera tu na marais wengne kwenda hadi Boeing ila chengaa !! Mwamba kaja fasta tu bomberdier Q400 hizi hapa, airbus 220 hizi hapa, dreamliner787 hili hapa.
Ata ILE ikulu pale chamwino ilianza ngonjera kitambo tu toka kwa nyerere alivyoingia mwamba hakutaka ngonjera Leo hii dude limesimama pale chamwino. Inshort magu alikuta vitu au projects nyingi on papers !!! Yeye kaziconvert into real ones
 
Kichwa cha habari kimeeleweka.

Kwa faida ya wengi, waliokuwepo na wasiokuwepo awamu zilizopita. kila mmoja wetu ana mtazamo wake tofauti na wa mwengine, tujadili mafanikio na madudu ya awamu zilizopita.

Binafsi nashukuru, nimeziishi awamu kadhaa za Tanganyika kuanzia tupo utawala wa Muingereza chini ya Umoja wa Mataifa.

Naikumbuka Tanganyika ya Muingereza kwa mbali, naikumbuka Tanganyika ya utawala wa Nyerere kwa ukaribu zaidi.

Kwa kuwa viongozi waliotuongoza ni wanaadam kama sisi, hawakosi mema yao na mapungufu yao, tuyajadili waliotuwachia.

Hata kama hukuwepo na umeyasoma au umehadithiwa tu, rukhsa kuyaleta ili tuchekeche na tuchambuwe mchele, chenga na chuya.

Bila kufahamu wapi tulipotoka na wapi tupo itakuwa vigumu kuelewa wapi tunaelekea.

Tujadili.
Huyu wa kwetu anatuachia dolla ikiwa imefiK 5000
 
Mwinyi sina hamu nae kabsa toka nisikie aliuza loliondo !!
 
Hawa akina Faiza fox ni well trained my friends !! Huyu anauwezo wa kuua hoja in a minute !! kwahyo unapodeal nae kuwa na facts za kumpinga. Huyu hayupo bure uku kama wengi wetu . Nimefatilia nikagundua kwamba nearly 75+% mada zake na michango yake nying ni politics na ni wa upande mmoja. Pia nimegundua kwamba ametoa maoni na positive crédits kwa asilimia 100% kwa Marais wa upande mmoja !! . Pia katika mabishano ya hoja karibu asilimia 80%+ amekuwa akiwin(well trained) narudia tena amekuwa trained sana kwenye eneo hili anaua hoja zinazokinzana na marais mwinyi, kikwete na maza house mlieni tyming mtaona. Ana uwezo wa kudeal na kikundi cha watu wengi na akatoboa. Tena kuna mahali nilipata mashaka kuna uwezekano hii Id hatumii mtu mmoja
 
Huyu wa kwetu anatuachia dolla ikiwa imefiK 5000
Hatuongelei waliopo.

Nyerere alikabidhiwa nchi nzuri, safi, tamu kama tende. Jionee chini hapa Dar aliyokabidhiwa Nyerere:

Alipong'atuka kamwachia Mwinyi mitaa yote ina mahandaki, Mwinyi nakaanza kuijenga na kuitia lami upya.

Fikiri kama Dar anapoishi kapaacha nyang'a-nyang'a huko mikoani palikuwaje?
 
Back
Top Bottom