Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Uzi wako wote umejikita na Nyerere tu,Hapana, si kweli nilikuwepo.
Nyerere aliiacha Tanzania ikiwa ni nchi ya mwisho kwa umasikini duniani. Aliiwacha hata chakula inabidi tukae foleni, wakati yeye aliipokea kwa Mkoloni ikiwa ni nchi ya kwanza katika Afrika inayosfirisha mazao ya kilimo.
Unajuwa kuwa Tanzania Nyerere alituwacha chakula hatuna, mafuta hatuna, akiba benki hatuna.
Umri wa kutenegemea kuishi mtanzania(life expectancy) wakati wa nyerere ulikuwa haufiki miaka 45.
Yule mzee usisikie anavyopambwa, alituwachia na mabalaa ya kila kitu Kawacha nchi foleni kila kitu foleni.
Kwa mtazamo wangu, Nyerere hakuwa na baraka za Mwenyezi Mungu kabisa katika kipindi chake. Majanga mwanzo mwisho.
Naamini huwezi kudhulumu watu Mwenyezi Mungu akakubariki.
Jikite katika uzi kwa ujumla wake badala ya kumshambulia kwa sababu zako binafsi baba wa taifa lako, mwl Julius Nyerere.Hilo nalo neno, kuna mjadala tuliujadili sana zamani, enzi za jmabo forums, uligusia kuwa tuliwahi sana kudai uhuru?
Binafsi naamini hatukuwahi, tulichelewa, sema aliyetufikisha hapa ni Nyerere, aliweka misingi mibovu ya kiutawala na kiuchumi. Aliwategemea sana Waingereza na waznngu wa vatikano akidhani ni watu wa maana kwa kuwa walimpa scholarship, kumbe wanamuingiza kichwa kichwa.
Naaamini nyerere alikuwa ni msemaji mzuri na ni mtu wa "literature", hekaya na porojo ndiyo mwenyewe, lakini sayansi za uongozi na uchumi zilimpiga chenga sana tena sana.
Nyerere angekuwa ni "salesman" anagefanya vizuri sana.
Yeah siwezi kushindana nao kabsa. Yaan how comes mtu unaomba tende arabuni na unaiomba serikali isitoze kodi 😀😀😀huhuhuhuh a. aah sorry madam president ah tunaomba sirikali itulete darubin ya kuangalia mwezi 😀😀😀😀Ma shaa Allah, wewe hata usome upindukie huwezi kabisa kushindana, kwa lolote, na mwanafunzi aliyepata hijaza ya Ustadh wake wa madrassa.
Kumbuka hilo.
Awamu ya 5 ndio pekee ya kutolewa mfano wa mengi mazuri yanayoonekana.Kichwa cha habari kimeeleweka.
Kwa faida ya wengi, waliokuwepo na wasiokuwepo awamu zilizopita. kila mmoja wetu ana mtazamo wake tofauti na wa mwengine, tujadili mafanikio na madudu ya awamu zilizopita.
Binafsi nashukuru, nimeziishi awamu kadhaa za Tanganyika kuanzia tupo utawala wa Muingereza chini ya Umoja wa Mataifa.
Naikumbuka Tanganyika ya Muingereza kwa mbali, naikumbuka Tanganyika ya utawala wa Nyerere kwa ukaribu zaidi.
Kwa kuwa viongozi waliotuongoza ni wanaadam kama sisi, hawakosi mema yao na mapungufu yao, tuyajadili waliotuwachia.
Hata kama hukuwepo na umeyasoma au umehadithiwa tu, rukhsa kuyaleta ili tuchekeche na tuchambuwe mchele, chenga na chuya.
Bila kufahamu wapi tulipotoka na wapi tupo itakuwa vigumu kuelewa wapi tunaelekea.
Tujadili.
Bandari zote za Mashariki ya Afrika zilikuwa za wenye wa Mashariki ya Afrika, walikuja Waarabu wakaendeleza, waalikuja Waajemi wakaendeleza, Walikj aWareno, Wajerumani, Waingereza, wamezikuta, wamefanya waliyofanya wakaziwacha kama walivyozikuta.
Hata neno "Bandari" linatokana na Kiajemi.