Kila Rais wa Tanzania alipoondoka aliacha nini kwa awamu iliyomfatia?

Kila Rais wa Tanzania alipoondoka aliacha nini kwa awamu iliyomfatia?

Hawajatufikisha popote. Hata ikulu ingekuwa hamna mtu hapa tulipo tungefika. Tungeendelea kutawaliwa tungekuwa zaidi ya hapa. Kwa kifupi hawajatuachia kitu bali kuna vitu wametuchukulia.
Hilo nalo neno, kuna mjadala tuliujadili sana zamani, enzi za jambo forums, uligusia kuwa tuliwahi sana kudai uhuru?

Binafsi naamini hatukuwahi, tulichelewa, sema aliyetufikisha hapa ni Nyerere, aliweka misingi mibovu ya kiutawala na kiuchumi. Aliwategemea sana Waingereza na waznngu wa vatikano akidhani ni watu wa maana kwa kuwa walimpa scholarship, kumbe wanamuingiza kichwa kichwa.

Naaamini nyerere alikuwa ni msemaji mzuri na ni mtu wa "literature", hekaya na porojo ndiyo mwenyewe, lakini sayansi za uongozi na uchumi zilimpiga chenga sana tena sana.

Nyerere angekuwa ni "salesman" anagefanya vizuri sana.
 
Ikiwa na mifumo ya uongozi ambayo hatujabadili mpaka Leo zaidi ya kubadili rangi tu kwenye hizo nafasi
Unafahamu kuwa kwa miaka yote aliyokuwepo Nyerere ikulu kulikuwa kuna pandikizi la Kingereza, Joan Wicken, ambalo Nyerere alikuwa hafanyi kitu bila kupitia kwake?

1693555002807.png


Hakuaminiwa hata alipokuja Malkia, ilibidi pandikizi linaloaminika liwepo hapo hapo:

1693555250893.png
 
Hapana, si kweli nilikuwepo.

Nyerere aliiacha Tanzania ikiwa ni nchi ya mwisho kwa umasikini duniani. Aliiwacha hata chakula inabidi tukae foleni, wakati yeye aliipokea kwa Mkoloni ikiwa ni nchi ya kwanza katika Afrika inayosfirisha mazao ya kilimo.

Unajuwa kuwa Tanzania Nyerere alituwacha chakula hatuna, mafuta hatuna, akiba benki hatuna.

Umri wa kutenegemea kuishi mtanzania(life expectancy) wakati wa nyerere ulikuwa haufiki miaka 45.

Yule mzee usisikie anavyopambwa, alituwachia na mabalaa ya kila kitu Kawacha nchi foleni kila kitu foleni.

Kwa mtazamo wangu, Nyerere hakuwa na baraka za Mwenyezi Mungu kabisa katika kipindi chake. Majanga mwanzo mwisho.

Naamini huwezi kudhulumu watu Mwenyezi Mungu akakubariki.
Mwalimu Nyerere aliwahi kutawala nchi hii kwenye kipindi kigumu zaidi kuliko maRais wote waliowahi na watakaowahi kuitawala Tanzania; usisahau hilo. Alichukua nchi kutoka kwenye mikono ya wakoloni, na ambao walikuwa hawataki atawale yeye, bali walikuwa wanataka mtawala kutoka kwenye Kabila kubwa ambalo ni wasukuma

Sasa kuanzia pale walipomwachia nchi wakawa wako standby wakiwa wanataka kuwatumia wanachi wenzake kumwondoa, na hiki ndicho kilichopelekea Army Mutiny ya mwaka 1964

Mbali na haya yote, wakati sisi tunapata Uhuru baadhi ya nchi za Afrika zilikuwa bado hazipata Uhuru wakiwemo majirani kabisa Msumbiji na Zimbabwe. Huko Afrika Kusini nako bado kulikuwa na shida ya Aparthedi rule

Nyerere asingeweza kuyavumilia matataizo haya yote yaendelee kuwepo Afrika, ukizingatia kuwa yeye pamoja na Nkrumah, walikuwa na mkakati wa kuja kuinganisha Afrika iwe USA (United Staes of Africa)

Kosa unaloweza kusema kuwa Nyerere alifanya, ni kuingia mno kwenye Siasa za Afrika baada ya Uhuru, wakati nchi yetu ilikuwa bado ni maskini mno. Pengine siasa hizo alienda nazo kwa umbali mrefu zaidi ya alivyostahili kwenda nazo, na hapo ndipo matatizo yalipoanza kujitokeza ndani kwake

Nampenda sana Nyerere kwa sababu hata makosa yake aliyowahi kufanya wakati wa utawala wake, alikuwa anakosea akiwa na nia njema ya kutafuta kitu kikubwa na chenye manufaa zaidi kwa wanachi wake. Na kwa sababu hakuwa Mungu, alikuwa anapanga jambo akiwa ametarajia neema zaidi kutoka kwenye jambo hilo lakini kwa bahati mbaya, mambo mengine yalikuwa yanageuka otherwise.

Hujuma pia zilikuwepo kutoka kwa baadhi ya wenzake waliokuwa wametarajia kutanua baada ya Uhuru, huku Nyerere yeye lengo lake likiwa kwa wananchi wake maskini

Nia njema iliyokuwa ndani ya Mwalimu, ilikuja kujidhihirsha tena hata kwa Marais wengine waliomfuatia, wakiwemo Mwinyi na Kikwete, na inaendelea kujidhihirsha hadi leo. Alipnada mbegu njema, anaendelea kuvuna kile alichowahi kupanda

Hapa sisemi kwamba watu hawa walifanya maajabu mno, hapana, ila najaribu tu kuilezea ile nia yao njema kwa nchi wakati wanaomba ridhaa ya kuongoza nchi kutoka kwa wanchi, na baada ya kuwa wamepata ridhaa hiyo. Kama kuna mahali walionekana kupwaya aua kukwama, basi pengine tatizo halikuwa wao, bali sisi wanachi.Wanachi wana nguvu kubwa mno kwa sababu wao ndiyo wanaoamua Rais kuwa madarakani
Unaweza ukaiona nguvu ya wanachi kwenye hili swala la uwekezaji Bandarini; dhahabu inayotaka kutpwa kwenye jalala kisa tu wanachi wanapotoshwa

Haipo nchi duniani ambayo Bunge lake na Serikali yake vyote vinaweza kushrikiana kuuza nchi au kuingia kwenye mkataba wa kuiumiza Nchi; nchi ya namna hiyo kwenye dunia hii haipo!
 
Mwalimu Nyerere aliwahi kutawala nchi hii kwenye kipindi kigumu zaidi kuliko maRais wote waliowahi na watakaowahi kuitawala Tanzania; usisahau hilo. Alichukua nchi kutoka kwenye mikono ya wakoloni, na ambao walikuwa hawataki atawale yeye, bali walikuwa wanataka mtawala kutoka kwenye Kabila kubwa ambalo ni wasukuma

Hili siyo kweli, wakoloni wangetaka hivyo asingetawala.

Wakoloni waliamini jabisa ndani ya Nyerere wamepata wakitakacho.

Itakuwaje utawala mgumu wakati kakabidhiwa nchi ikiwa ya kwanza kwa kusafirisha (export) mazao ya kilimo katika Afrika?

Itakuwaje na wakati mgumu wakati Alikuwa na backup ya miaka 10 ya Umoja wa Mataifa kupitia Muingereza?

Kama kuna nchi iliyopata uhuru wake kwenye "silver platter" basi ilikuwa ni Tanganyika.
 
Unafahamu kuwa kwa miaka yote aliyokuwepo Nyerere ikulu kulikuwa kuna padikizi la Kingereza, Joan Wicken, ambalo Nyerere alikuwa hafanyi kitu bila kupitia kwake?


View attachment 2735405


Hakuaminiwa hata alipokuja Malkia, ilibidi pandikizi linaloaminika liwepo hapo hapo:

View attachment 2735412
Kwani sasa Wana aminiwa? Mi naona tupo vile vile ila means zimebadilika, badala ya mapandikizo physical yapo mapandikizo invisible
 
Samia katuachia DPW, waje kujitawala ndani ya nchi yetu.
Samia bafonyupo na anaendelea na RRRR .

Keshokutwa tarehe 5/9/2023 kunw nchi za duniani zinafanya mkutano wao, zimekujankuunga mkono mpango wa mama Samia na Bashe wa BBT.

Huu mpango, licha ya Tanzania na Afrika, umelenga kuilisha dunia.

Mpaka sasa Bashe anauendesha vizuri sana kupita matarajio. Jionee👇🏾


View: https://youtu.be/ANlXmm6eBv8?si=kln8hr98T9PPYM4w
 
Kichwa cha habari kimeeleweka.

Kwa faida ya wengi, waliokuwepo na wasiokuwepo awamu zilizopita. kila mmoja wetu ana mtazamo wake tofauti na wa mwengine, tujadili mafanikio na madudu ya awamu zilizopita.

Binafsi nashukuru, nimeziishi awamu kadhaa za Tanganyika kuanzia tupo utawala wa Muingereza chini ya Umoja wa Mataifa.

Naikumbuka Tanganyika ya Muingereza kwa mbali, naikumbuka Tanganyika ya utawala wa Nyerere kwa ukaribu zaidi.

Kwa kuwa viongozi waliotuongoza ni wanaadam kama sisi, hawakosi mema yao na mapungufu yao, tuyajadili waliotuwachia.

Hata kama hukuwepo na umeyasoma au umehadithiwa tu, rukhsa kuyaleta ili tuchekeche na tuchambuwe mchele, chenga na chuya.

Bila kufahamu wapi tulipotoka na wapi tupo itakuwa vigumu kuelewa wapi tunaelekea.

Tujadili.
Mmhh kumbe we ni bibi kabisa!
 
Nakumbuka Mwinyi alituachia mkataba mbovu wa Loliondo... kipande cha ardhi ya TZ kiliuzwa kwa waarabu. Pia Mwinyi alituachia mkataba wa kinyonyaji wa IPTL & Tanesco.
 
Wote kasoro Magufuli , mpaka sasa mmoja ndo kakiri na kitabu kaandika.
Andika ueleweke, unaongelea nini, usiongee kimkato mkato ukafikiri wote tuna fikra kama zako.


Ongelea awamu moja imewacha nini, cha maana aua kibovu. Wacha watu wachangie waonavyo wao. Ukimaliza weka mwengine, una haraka ya nini? umeshikwa na tumbo la kuharisha?

Hivi hizo shule mlienda kusomea ujinga?
 
Back
Top Bottom