KERO Kila siku TANESCO wanakata umeme jioni Pugu Majohe hadi imekuwa kero

KERO Kila siku TANESCO wanakata umeme jioni Pugu Majohe hadi imekuwa kero

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Joined
Dec 6, 2025
Posts
7
Reaction score
5
Pugu Majohe na Majohe yote ikiwemo kwa Ngozoma, Sondombwa, Halisi, Rada, Viwege, Bombambili na maneno ya jirani kuna changamoto ya kukatika umeme kila siku jioni kuanzia saa moja mpaka saa sita usiku.

Changamoto hii ilianza Mwezi Disemba 2025 na inaendelea hadi sasa, kuna muda unakatika mchana ila na jioni lazima ukatike.

TANESCO wanaweza toa taarifa ya matengenezo kwa kukata umeme kuanzia Saa tatu asubuh mpaka Saa 11 Jioni ila ikifika saa moja na nusu siku hiyohiyo wanakata tena yaani imekuwa kero sanaa.

Wananchi wa Majohe tumekuwa tukilalamikia kero hiyo, kuna muda tumewaza kutafuta namba ya Waziri au Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO ili kuweza kufikisha kero hii lakini hatujafanikiwa.

Kingine ni kwamba upande wa pili ambao kuna kambi huko haukatiki, sasa kwa nini iwe huku kwetu tu ambapo ndipo Wananchi wa kawaida tulipo?

Kuna muda unaweza kukatika kwa staili kama mtu anachezea switch hali ambayo imekuwa hatarishi kwa kuwa inaweza kusababisha madhara ikiwemo kuunguza vitu.

Kila ukikatika wao ni kuomba radhi na kisingizio ni matengezo, je ni matengezo gani ambayo hayamaliziki kwa miezi mitatu sasa?

Pia soma
~ Kigamboni kuna kero ya umeme kukatika mara kwa mara, tunaunguza vitu kila mara
~ Mkuranga, Pwani tuna tatizo la umeme unakatika mara kwa mara, ahadi ya TANESCO kushughulikia haijatimia
 
MAJIBU YA CHANGAMOTO YA HUDUMA YA UMEME KATIKA MAENEO YA GONGOLAMBOTO NA MAJOHE

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) lilipokea taarifa ya changamoto ya upatikanaji wa huduma ya umeme katika maeneo ya Gongolamboto na Majohe kupitia Mbunge wa Jimbo la Kivule, Mhe. Ojambi Massaburi. Kufuatia taarifa hiyo,

Shirika lilifanya tathmini ya kina na kubaini kuwa ongezeko kubwa la mahitaji ya umeme katika eneo hilo lilikuwa limeanza kuathiri ubora na uimara wa huduma kwa baadhi ya wateja.

Kutokana na hali hiyo, Serikali kupitia TANESCO ilitenga kiasi cha shilingi bilioni 1 kwa ajili ya utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa njia mpya ya umeme kutoka Kituo cha Kupoza umeme Gongolamboto, Mwisho wa Lami hadi Majohe kwa lengo la kuongeza uwezo wa usambazaji wa umeme, kuboresha uimara wa huduma na kupunguza changamoto za kukatika kwa umeme katika maeneo hayo.

Kwa sasa, utekelezaji wa mradi huo umefikia zaidi ya asilimia 80.Katika kuendelea na utekelezaji wa mradi huo, tarehe 18 Juni 2026

TANESCO ilifanya katizo la umeme lililopangwa katika laini inayolisha eneo la Majohe ili kuruhusu kazi za ujenzi wa njia mpya ya umeme kuendelea kwa usalama na ufanisi.Kazi za ujenzi zilikuwa zimekamilika mapema jioni ya jana. Hata hivyo, wakati wa kuvuta waya kwenye njia mpya, nguzo nne zilivunjika na kusababisha kazi kuanza upya. Hali hiyo ilitokana na ujenzi wa njia mpya kufanyika sambamba na laini iliyopo (double circuit), jambo lililohitaji umakini mkubwa wa kiufundi ili kuhakikisha usalama wa miundombinu na watendaji.

Aidha, utekelezaji wa kazi hizo uliongezeka muda kutokana na mazingira ya eneo husika kuwa na maji mengi, hali iliyosababisha changamoto katika uchimbaji wa mashimo na usimamishaji wa nguzo mpya za zege.

Baada ya kutokea kwa changamoto hiyo, TANESCO ilichukua hatua za haraka kwa kubadilisha nguzo zote nne zilizoharibika na kuweka nguzo mpya za zege. Hatimaye, kazi zote zilikamilika na huduma ya umeme ilirejeshwa katika laini zote mbili zinazohudumia eneo husika leo tarehe 19 Juni 2026 saa 1:20 asubuhi.

TANESCO inaomba radhi kwa usumbufu uliojitokeza wakati wa utekelezaji wa kazi hizi muhimu za kuboresha huduma ya umeme na inawashukuru wananchi wa maeneo ya Gongolamboto, Majohe na maeneo jirani kwa uvumilivu na ushirikiano wao.

Tangazo la katizo lililotolewa awali kwa wananchi (ambatishwa). Aidha, wateja wa eneo hilo wanashauriwa kujiunga na kundi la WhatsApp la TANESCO (8.B.26TANESCO HUDUMA MAJOHE ) ili kupokea taarifa za huduma, matengenezo yaliyopangwa au matengezo ya dharura na taarifa nyingine muhimu kwa wakati.

Imetolewa na;

KURUGENZI YA MAWASILIANO NA HUDUMA KWA WATEJA TANESCO MAKAO MAKUUDODOMA19 Juni 2026
 
Attachments

  • IMG-20260619-WA0030.jpg
    IMG-20260619-WA0030.jpg
    96.4 KB · Views: 9
Back
Top Bottom