montana zayumba
JF-Expert Member
- Nov 9, 2014
- 225
- 31
Maisha siku zote ujifunze kuingiza kitu kigeni akilini kikuongezee ufahamu,Asante mtoa post hii!
Nonsense,,,, maelezo kibao NA tutorial za kufa mtu,,, at the end nothing.Dunia ya sasa iko simple sana na clear ndo maana hata job interviews zimepungua masaa,,,;sasa umeapload movie ya 2hrs kwenye somo? Sasa mtihani si itakuwa TB au XB?
Unamaanisha LazyIPTV au Kodi?
Kama ni Kodi je umeinstall version ipi?
Kodi v 4.2
nikifungua vdubt25 channel zake inasema one or more item failed to play chek the log file
Natumia Android , kupata add- ons wadau wengi wametoa link kwenye post za kwanza
Ila unaweza Google phoenix TV au paki India TV ukapata link yakupakua
Tumezoea katika maisha yetu tukiangalia Tv basi huduma ile tunaipata kupitia madishi, cable au antenna. siku zinavyosogea mbele na technology ndivyo inavyokuwa na ndio jinsi madish na antenna vinavyopitwa wakati. leo kwenye uzi huu tutaangalia IPTV.
Ni nini hii IPTV?
IPTV ni kifupi cha Internet Protocal TeleVision. Hii ni aina ya uangaliaji TV kupitia mtandao wa internet ambapo kituo cha TV badala ya kutumia satelite dish au cable wenyewe wanarusha matangazo kwa internet.
Unawezaje kuangalia IPTV?
Utahitaji kifaa chenye internet na uwezo wa kustream ili kuweza kuangalia kama vile smartphone, tablet, laptop, desktop hadi TV zenye internet zinaweza kustream.
Internet yenye speed gani inahitajika?
Internet yoyote hata ya edge inaweza kustream ila iwe na latency nzuri, zipo stream zinahitaji speed ya 200kbps tu (25KBps). Kama una latency ndogo hata internet iwe na speed vipi huwezi kustream live utastream tu vitu ambavyo si live. Kujua zaidi kuhusu latency nenda thread hii
https://www.jamiiforums.com/tech-ga...iwa-na-download-speed-kubwa-ndio-mzuri-2.html
Je software gani inatumika kustream hizo TV?
Kikawaida browser yenye flash au html5 inaweza kustream tv lakini ukitaka kustream vizuri zaidi software kama VLC au KODI ni muhimu. Kutokana na uhaba wa links za VLC nitazungumzia zaidi jinsi ya kutumuia KODI kuangalizia IPTV.
KODI ni nini?
KODI ni software (media centre) ambayo hutumika kuubadili muonekano wako wa simu uwe kama TV na kuweza kuenjoy TV unazotumia na inapatikana kwenye simu, tablet, computer hadi TV.
Kuidownload nenda website yao hii hapa chini, ni bure haiuzwi
Downloads | Kodi
Nikishadownload kodi nini kinafuatia?
Utahitaji ku install plugin ili uweze kuangalia TV online. Click video add on halafu chagua watchmojo, install halafu ifungue tuone kama itafanya kazi.
KODI imefanya kazi, je siwezi angalia mpira na vipindi vyengine?
Unaweza angalia mpira chanel unayotaka kuanzia za ki-Africa kama Super sport, za Ulaya kama Sky sport, za Asia kama Bein sport hadi za kimarekani kama NBC cha muhimu uwe na plugin (add ons) husika, hizi plugin za mpira na michezo mengine zinapatikana tu internet mfano mimi plugin yangu ninayotumia inaitwa Vdtube25 ina channel nyingi sana kuanzia mpira hadi movie.
Hio hapo juu sky sport 3
Uzuri wa hizi plugin za kodi zipo TV ni HD na nyengine ni full HD kabisa hivyo internet yako tu.
Malipo?
Kila kitu kuanzia juu hadi hapa ulipofikia ni bure hutoi pesa, ila hizi plugin za bure haziaminiki zipo za kulipia ambazo hazikati ovyo. Mimi sijawahi kulipa natumia tu bure ila kama unahitaji service nzuri zaidi unaweza kulipa ila pia kuwa makini na matapeli
Tutorial ya kuweka na mahala pa kupatia plugins
Plugin yangu ninayotumia ya vdtube25
https://seo-michael.co.uk/how-to-install-vdubt25-add-on-kodi-xbmc
Website hio hio pia utapata plugins nyingi.
Kama una swali lolote usisite kuuliza chini
Nawezaje kuistall KODI kwenye TV ?
hahaahha , ametype UKAWA huyo , sisi tunapeta somo limeongezeka kwenye ku add on , yeye bado yuko kwenye installation
Tafadhari wana jamvi mtu yoyote mwenye link za tv za hapa nyumbani dondosha link hapa....
Nonsense,,,, maelezo kibao NA tutorial za kufa mtu,,, at the end nothing.Dunia ya sasa iko simple sana na clear ndo maana hata job interviews zimepungua masaa,,,;sasa umeapload movie ya 2hrs kwenye somo? Sasa mtihani si itakuwa TB au XB?
Haya madude nayakubali sana. Nataka niwatest wale jamaa wa kulipia wapoje?
Njunwa Wamavoko nipe maujanja ya kupatia fake credit card maana nakwama kwenye security code.
naulizia swala la bundle kwasababu hamjaongelea kabisa! mfano nikiwa na 1GB naweza kustrem kwa mda gani kama nacheki football?@chief
Sportsdevil tv zake ni zile zinazopatikana site maarufu za mpira kama firstrow, livetv.ru na rojadirecta. Zenyewe zina quality ndogo sana kwa wale wenye internet isio na speed. Mfano rojadirecta ana chanell ambazo ni chini ya 200kbps. Ukiwa na network ya edge unaweza streamNilikua Offline kwa siku kadhaa nimekuta new ideas hapa
TV Directo
SportsDevil
Nimeinstall sportsDevil ila sijaona faida yake maana Content zake naona ni sawa na zile za Phoenix,vdtube25 etc
Hiyo TV directo nime google sijaelewa
Inategemea na quality na stream pia. Ni vizuri ukafanya research mwenyewe kaka.
Tv nyingi zina quality za aina tatu
SD au 480p
HD au 720p
Full HD au 1080p
Kama wewe unabania mb zikimbie hizo chanell za hd na pendelea za sd.
Utajuaje ipi ni hd au sd? Ukishaplay tv ukistop kodi inatambua quality ya ile stream hivyo kwa mbele inakuandikia kama ni hd au sd
Kwa mahesabu ya haraka haraka mpira na mapumziko na dakika za nyongeza ni kama masaa 2 (dk 120)
Dakika 120 ni sekunde 7200
Internet yako ni mb 1000
Roughly kila sekunde unaweza tumia kilobyte 140 ambayo ni zaidi ya 1mbps.
Kama umesoma post ya juu njunwa anasema amestream hd kwa net ya 1mbps tu, mimi pia nimewahi fanya hivyo.
Hivyo jibu ni ndio kaka gb1 unaweza stream mpira wote hadi unaisha make sure huchagui tu full hd
Tatizo lako la pale juu umelitatua?
Maana yake link unayoifungua ipo dead (ni mfu) hivyo haiwezi funguka...
Inabidi usubiri hadi developer wa vdubt25 atapofanya update...
Pia huenda huna connection ya internet au upo geo-restricted
Yap la mwanzo nilifanikiwa...... Lkn hilo la kuto play bado lipo kwa channels nying.
Hii vidubt ndo linasumbua lkn nyingne zipo poa