Kila unalotakiwa kujua kuhusu IPTV (kuangalia TV kwa kutumia internet)

Kila unalotakiwa kujua kuhusu IPTV (kuangalia TV kwa kutumia internet)

Unamaanisha hizi add-ons zinazotajwa humu hakuna namna naweza kuzpata kama hazipo kwenye list ya get more kwenye Kodi yangu?

Unadownload kijana...angalia posts za nyuma wanaelekeza sehem ya kuzipata au maelekezo jinsi ya kuziinstal
 
Tumezoea katika maisha yetu tukiangalia Tv basi huduma ile tunaipata kupitia madishi, cable au antenna. siku zinavyosogea mbele na technology ndivyo inavyokuwa na ndio jinsi madish na antenna vinavyopitwa wakati. leo kwenye uzi huu tutaangalia IPTV.

Ni nini hii IPTV?
IPTV ni kifupi cha Internet Protocal TeleVision. Hii ni aina ya uangaliaji TV kupitia mtandao wa internet ambapo kituo cha TV badala ya kutumia satelite dish au cable wenyewe wanarusha matangazo kwa internet.

Unawezaje kuangalia IPTV?
Utahitaji kifaa chenye internet na uwezo wa kustream ili kuweza kuangalia kama vile smartphone, tablet, laptop, desktop hadi TV zenye internet zinaweza kustream.

Internet yenye speed gani inahitajika?
Internet yoyote hata ya edge inaweza kustream ila iwe na latency nzuri, zipo stream zinahitaji speed ya 200kbps tu (25KBps). Kama una latency ndogo hata internet iwe na speed vipi huwezi kustream live utastream tu vitu ambavyo si live. Kujua zaidi kuhusu latency nenda thread hii
https://www.jamiiforums.com/tech-ga...iwa-na-download-speed-kubwa-ndio-mzuri-2.html

Je software gani inatumika kustream hizo TV?
Kikawaida browser yenye flash au html5 inaweza kustream tv lakini ukitaka kustream vizuri zaidi software kama VLC au KODI ni muhimu. Kutokana na uhaba wa links za VLC nitazungumzia zaidi jinsi ya kutumuia KODI kuangalizia IPTV.

KODI ni nini?
KODI ni software (media centre) ambayo hutumika kuubadili muonekano wako wa simu uwe kama TV na kuweza kuenjoy TV unazotumia na inapatikana kwenye simu, tablet, computer hadi TV.
Kodi-devices-smudged.jpg


Kuidownload nenda website yao hii hapa chini, ni bure haiuzwi
Downloads | Kodi

Nikishadownload kodi nini kinafuatia?
Utahitaji ku install plugin ili uweze kuangalia TV online. Click video add on halafu chagua watchmojo, install halafu ifungue tuone kama itafanya kazi.
9vW4MHp.jpg


KODI imefanya kazi, je siwezi angalia mpira na vipindi vyengine?
Unaweza angalia mpira chanel unayotaka kuanzia za ki-Africa kama Super sport, za Ulaya kama Sky sport, za Asia kama Bein sport hadi za kimarekani kama NBC cha muhimu uwe na plugin (add ons) husika, hizi plugin za mpira na michezo mengine zinapatikana tu internet mfano mimi plugin yangu ninayotumia inaitwa Vdtube25 ina channel nyingi sana kuanzia mpira hadi movie.
zNbDtYR.jpg

PppArCw.jpg


Hio hapo juu sky sport 3

Uzuri wa hizi plugin za kodi zipo TV ni HD na nyengine ni full HD kabisa hivyo internet yako tu.

Malipo?
Kila kitu kuanzia juu hadi hapa ulipofikia ni bure hutoi pesa, ila hizi plugin za bure haziaminiki zipo za kulipia ambazo hazikati ovyo. Mimi sijawahi kulipa natumia tu bure ila kama unahitaji service nzuri zaidi unaweza kulipa ila pia kuwa makini na matapeli

Tutorial ya kuweka na mahala pa kupatia plugins
Plugin yangu ninayotumia ya vdtube25
https://seo-michael.co.uk/how-to-install-vdubt25-add-on-kodi-xbmc

Website hio hio pia utapata plugins nyingi.

Kama una swali lolote usisite kuuliza chini

Mkuu nmeinstall kodi lkn nikiifungua inanipa error na kufanya black.screen. wap nmekosea apo
 
Error gani? Ukituambia hio error ndio mtu atajua aanze wapi

Ilkua inasema "unable to create gui" bt nmeupdate vga now iko fine ss nisaidien plugins ambazo ntaweza stream supersport kwakua izo mlizoztaja nying nmezkosa kwny video plugins
 
Ilkua inasema "unable to create gui" bt nmeupdate vga now iko fine ss nisaidien plugins ambazo ntaweza stream supersport kwakua izo mlizoztaja nying nmezkosa kwny video plugins

Hazipo kwenye plugin za video, click link zinazotolewa na wadau, utazidownload kupitia hizo link
 
Natumia Tecno M5 imekubali naangalia baadhi ya tv though sijafatilia ile tutorial.

Nashukuru sana kwa uzi mzuri mkuu, nimefufahi sana maana hata warembo vihelehele kwenye huu uzi hawapo hata mmoja washazoea ,umbea jamii forum. Hii kitu noma sana, salute!!
 
Mie wakuu nimedownload hiyo application
Nimeinstall
But inanambia
Error - package sio compatible na device yangu
Natumia tablet
P9 Tecno mini pad

Sio mtaalam sana ila nahisi badilisha aina ya kodi uliyoinstall inaweza ikakubali. Niliexprience tatizo kama lako lakini nilivobadili kodi ikakubali. By th way nahisi simu yangu ni ndogo kuliko yako ingawa wanasema android version lazima ianzie 4.2 na kuendelea ndoninaweza kukubali. Narudia tena sio mtaalam ila nafikiri inaweza saidia ukifanya ivo
 
Msaada kwenye tuta!!
Nataka kuinstall vdubt25 lakini nikiselect Add source haileti option ya none ili nitype url inayotakiwa. Msaada please, nimejaribu kuattache picha ila imeshindikana.
 

Attachments

  • 1439277069220.jpg
    1439277069220.jpg
    22.6 KB · Views: 209
Msaada kwenye tuta!!
Nataka kuinstall vdubt25 lakini nikiselect Add source haileti option ya none ili nitype url inayotakiwa. Msaada please, nimejaribu kuattache picha ila imeshindikana.

click hapo hapo kwenye add source then chagua NONE utaona sehemu ya kuweka hiyo URL yako
 
Hakuna kitu kiliniudhi juzi kama speed ya voda kushindwa kustream kwenye Kodi..yaani nimechukia mpaka basi..
 
Back
Top Bottom