Chief-Mkwawa
Platinum Member
- May 25, 2011
- 31,559
- 42,179
- Thread starter
- #1,081
Zote zina gpu moja, mali 400mp2 so zilitakiwa ziwe sawa kwenye kila kitu, umecheki na version pia ni moja? version ya kodiYa wife ni TECNO BOOM J5
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Zote zina gpu moja, mali 400mp2 so zilitakiwa ziwe sawa kwenye kila kitu, umecheki na version pia ni moja? version ya kodiYa wife ni TECNO BOOM J5
Kariakoo sh 15,000Chief-Mkwawa nitapata wapii hii kitu![]()
sehemu gani?Kariakoo sh 15,000
Toka round about ya uhuru (barabara ya mnazi mmoja na msimbazi ), kama unaelekea msimbazi police, mtaa wa kwanza kushoto (maeneo hayo yana maduka mengi ya simu), ufuate huo mtaa mpaka duka la mwisho kushoto kwenye hilo jengo la kushoto. Usiingie vikorido vinavyoelekea maduka ya ndani, nenda moja kwa moja. Ni duka la vifaa vya simu.sehemu gani?
kwa muonekano tu ni adapter, umeitest inafanya kazi?Toka round about ya uhuru (barabara ya mnazi mmoja na msimbazi ), kama unaelekea msimbazi police, mtaa wa kwanza kushoto (maeneo hayo yana maduka mengi ya simu), ufuate huo mtaa mpaka duka la mwisho kushoto kwenye hilo jengo la kushoto. Usiingie vikorido vinavyoelekea maduka ya ndani, nenda moja kwa moja. Ni duka la vifaa vya simu.
![]()
![]()
Ni hapo pekee. Nilizunguka siku nzima hapo kkoo ndipo nikabahatisha kwenye duka hilo. Nimenunua siku nne zilizopita
Bahati mbaya simu yangu haina mhl technology. Hivyo nimekwama.kwa muonekano tu ni adapter, umeitest inafanya kazi?
sikuwa nafahamu kama hii ni technology yenye standard zake kabisa, nilifikiri ni adapter tu watu wanabadili tu hizo data.Bahati mbaya simu yangu haina mhl technology. Hivyo nimekwama.
greatand i will work on this as i settle, Mungu akubariki kwa knowledge uliyotumegeaTumezoea katika maisha yetu tukiangalia Tv basi huduma ile tunaipata kupitia madishi, cable au antenna. siku zinavyosogea mbele na technology ndivyo inavyokuwa na ndio jinsi madish na antenna vinavyopitwa wakati. leo kwenye uzi huu tutaangalia IPTV.
Ni nini hii IPTV?
IPTV ni kifupi cha Internet Protocal TeleVision. Hii ni aina ya uangaliaji TV kupitia mtandao wa internet ambapo kituo cha TV badala ya kutumia satelite dish au cable wenyewe wanarusha matangazo kwa internet.
Unawezaje kuangalia IPTV?
Utahitaji kifaa chenye internet na uwezo wa kustream ili kuweza kuangalia kama vile smartphone, tablet, laptop, desktop hadi TV zenye internet zinaweza kustream.
Internet yenye speed gani inahitajika?
Internet yoyote hata ya edge inaweza kustream ila iwe na latency nzuri, zipo stream zinahitaji speed ya 200kbps tu (25KBps). Kama una latency ndogo hata internet iwe na speed vipi huwezi kustream live utastream tu vitu ambavyo si live. Kujua zaidi kuhusu latency nenda thread hii
Je! mtandao ukiwa na download speed kubwa ndio mzuri ?
Je software gani inatumika kustream hizo TV?
Kikawaida browser yenye flash au html5 inaweza kustream tv lakini ukitaka kustream vizuri zaidi software kama VLC au KODI ni muhimu. Kutokana na uhaba wa links za VLC nitazungumzia zaidi jinsi ya kutumuia KODI kuangalizia IPTV.
KODI ni nini?
KODI ni software (media centre) ambayo hutumika kuubadili muonekano wako wa simu uwe kama TV na kuweza kuenjoy TV unazotumia na inapatikana kwenye simu, tablet, computer hadi TV.
![]()
Kuidownload nenda website yao hii hapa chini, ni bure haiuzwi
Downloads | Kodi
Nikishadownload kodi nini kinafuatia?
Utahitaji ku install plugin ili uweze kuangalia TV online. Click video add on halafu chagua watchmojo, install halafu ifungue tuone kama itafanya kazi.
![]()
KODI imefanya kazi, je siwezi angalia mpira na vipindi vyengine?
Unaweza angalia mpira chanel unayotaka kuanzia za ki-Africa kama Super sport, za Ulaya kama Sky sport, za Asia kama Bein sport hadi za kimarekani kama NBC cha muhimu uwe na plugin (add ons) husika, hizi plugin za mpira na michezo mengine zinapatikana tu internet mfano mimi plugin yangu ninayotumia inaitwa Vdtube25 ina channel nyingi sana kuanzia mpira hadi movie.
![]()
![]()
Hio hapo juu sky sport 3
Uzuri wa hizi plugin za kodi zipo TV ni HD na nyengine ni full HD kabisa hivyo internet yako tu.
Malipo?
Kila kitu kuanzia juu hadi hapa ulipofikia ni bure hutoi pesa, ila hizi plugin za bure haziaminiki zipo za kulipia ambazo hazikati ovyo. Mimi sijawahi kulipa natumia tu bure ila kama unahitaji service nzuri zaidi unaweza kulipa ila pia kuwa makini na matapeli
Tutorial ya kuweka na mahala pa kupatia plugins
kutokana na request nyingi za watu nita updates hapa mara kwa mara plugins ambazo zipo avtive
1.DNA TV
hii ipo active nimetest chanell kama BT sport na Sky sport zinafanya kazi vizuri tu. install toka hapa
Tutorial How to Install DNA TV for Kodi
ina tatizo la kuandika servel full sababu traffic ni kubwa hivyo ikiandika hivyo angalia chanell nyengine au endelea kuclick hadi ikubali.
pia kwenye repository yake kuna clone za IPTV stalker ila sijazitest.
2.PHOENIX TV
kama uli install phoenix kama .zip file pengine sasa hivi huoni kitu utahitajika kueka version mpya, tumia hii link
Tutorial How to Install Phoenix Kodi XBMC
nimetest chanell za movie na mpira zinafanya kazi
3.ISRAEL LIVE TV
sio mbaya ukiwa nayo kama backup kwenye chanell zake za sports kuna chanell za portugal huwa zinaonesha mpira japo quality si nzuri.
Tutorial How to Install IsraeLIVE Video Add-On Kodi
Kama una swali lolote usisite kuuliza chini
hio cable hapo juu ndio kazi yake, na pia kama tv ina miracast na simu ikiwepo utaconect bila wayaJamani me nahitaji kujua kama kuna kifaa naweza kutumia kuconect kutoka kwenye simu kwenda kwa tv na nikaangalia kwenye tv
Inaitwaje kaka na naipata wapi hapa tz?hio cable hapo juu ndio kazi yake, na pia kama tv ina miracast na simu ikiwepo utaconect bila waya
soma hapo juu post ya nyenyere inaitwa mhl bei sh 15,000 na inapatikana aggrey na likoma kwenye konaInaitwaje kaka na naipata wapi hapa tz?
Niliposoma maelezo ya hiyo adapter nilitafuta mtandaoni, karibu smart phones zote za miaka ya hivi karibuni zina mhl tech isipokuwa baadhi ya tecno, ambayo ndio natumia. Very sad. MHL inakuwa kwenye micro usb kusapoti hdmisikuwa nafahamu kama hii ni technology yenye standard zake kabisa, nilifikiri ni adapter tu watu wanabadili tu hizo data.
umehakiki vipi kama simu yako haina hio technology? naona kwenye site yao wana qr code ya kuscan ili kuhakiki
Mkuu chief mkwawa natafuta MHL 2.0 Adapter kwa ajili ya S4 yangu. Vipi hapo dar zinapatikana?. Mimi niko mkoani. Kwa maelezo ya web ya samsung kuna model huwa zinakataa kwenye s4. So naomba unijuze kama wajua hiyo ya samsung s4 naweza pata hapo dar na kwa bei gani.soma hapo juu post ya nyenyere inaitwa mhl bei sh 15,000 na inapatikana aggrey na likoma kwenye kona
ila hakiki kwanza kama simu yako ina hio technology ya mhl
Samsung j1 vipi inayo?soma hapo juu post ya nyenyere inaitwa mhl bei sh 15,000 na inapatikana aggrey na likoma kwenye kona
ila hakiki kwanza kama simu yako ina hio technology ya mhl
Hii hapa website ya wamiliki wa mhl technology wakiorodhesha simu zenye mhlSamsung j1 vipi inayo?
huwa mara nyingi technology kama hizi zinakuwa na backward compability, hivyo nahisi cable yoyote ya mhl itafaa hata hii tunayoizungumzia. kwa uhakika zaidi mwenye s4 atakuambiaMkuu chief mkwawa natafuta MHL 2.0 Adapter kwa ajili ya S4 yangu. Vipi hapo dar zinapatikana?. Mimi niko mkoani. Kwa maelezo ya web ya samsung kuna model huwa zinakataa kwenye s4. So naomba unijuze kama wajua hiyo ya samsung s4 naweza pata hapo dar na kwa bei gani.
Asante
VP na tunaotumia Windows Phone?nenda setting then video then acceleration kwenye render eka software, hio husaidia kama una gpu kimeo au driver huna
windows phone haina kodi, mimi hutumia youtube, universal streaming na live sports tv kuangalizia mpira.VP na tunaotumia Windows Phone?