Kile kichaka cha CAF ranking kinakaribia kufyekwa rasmi na Yanga ndiyo maana stress na uoga ni mwingi upande wa pili

Kuwaangalia ndege angani wakiimba nikafurahi nimetumia sh ngapi? Wakorubu wanaoishi Amazon huko hawajui hata pesa ni nini lakini wanafurahia maisha na familia zao wakiwinda na kuvua samaki huko! Usilazimishe pesa iwe furaha ya kila mtu!
 
Kuwaangalia ndege angani wakiimba nikafurahi nimetumia sh ngapi? Wakorubu wanaoishi Amazon huko hawajui hata pesa ni nini lakini wanafurahia maisha na familia zao wakiwinda na kuvua samaki huko! Usilazimishe pesa iwe furaha ya kila mtu!
Sasa boss kwani upo Amazon? Hata nyani si wapo porini na wana furaha wanaruka kwenye miti? Tunamuongelea binadamu wa kawaida wa kileo shabiki wa mpira wa miguu.
 
Sasa hivi mme elewa umuhimu wa kusubiri matokeo wakati mna anzisha nyuzi za Yanga hatoki kwa Al Hilal mlikua hamjui hayo?
 
Kwamba unabisha, hautaki, hauelewi au una maana gani?
Acheni kudanganyana. Hesabu hazitaki hisia na nyie mnapiga mahesabu kwa hisia hadi mnafumba macho. Unajua katika ranking za 2025-26 Simba ina nafasi ya kuwa hata namba 3?
 
Acheni kudanganyana. Hesabu hazitaki hisia na nyie mnapiga mahesabu kwa hisia hadi mnafumba macho. Unajua katika ranking za 2025-26 Simba ina nafasi ya kuwa hata namba 3?
Sasa kisichoeleweka hapo ni kipi? Hata Yanga ina nafasi ya kupanda zaidi ikifika fainali CAFCL, hapa tunazungumzia kwa sasa ambapo Simba ana jumla ya alama 38 na Yanga 34 au 39 endapo atavuka robo fainali. Huko mbele hatufahamu itakuwaje.
 
Ungengoja tufuzu kwanza
 

Attachments

  • IMG_20211005_154748.jpg
    607.4 KB · Views: 4
Sasa kisichoeleweka hapo ni kipi? Hata Yanga ina nafasi ya kupanda zaidi ikifika fainali CAFCL, hapa tunazungumzia kwa sasa ambapo Simba ana jumla ya alama 38 na Yanga 34 au 39 endapo atavuka robo fainali. Huko mbele hatufahamu itakuwaje.
Rank za CAF hazipangwi kutegemea utabiri. Zinapangwa kulingana na kile ambacho kimeshafanyika na zaidi ili uwe sahihi zaidi ni kuangalia pale kila timu ilipofikia mwishoni mwa msimu. Mnaignore rank za msimu husika ambazo Simba ni ya 7 na haziwezi kubadilika mnakimbilia kutabiri rank za msimu ujao.

Mnaishia kuangalia hadi robo kwa sababu hisia zenu zinawaambia Simba itafika mbali zaidi na nyie mnaweza kukomea hapo.
 
Ranking ni process sio hivo unavofikiria, hadi jana simba amepanda nafasi ya 5
 
Sasa hapo usichokielewa ni kipi? Hiyo rank inayosema Simba ni ya 7 inajumuisha points za msimu wa 2019/2020 na kwa CAF 5 year ranking hazihesabiwi tena, na kwa mujibu wa CAF ukitoa alama za msimu wa 2019/2020 Simba anabaki na 28 Yanga anabaki na 24, ukijumlisha za msimu huu mpaka sasa hata kama msimu haujaisha inajulikana simba ameshavuna alama 10 (5×2) ma Yànga alama 10 endapo hatavuka robo ila akivuka ni alama 15 (5×3) ukichukua 24+15=39, Japo msimu unaendelea wote wanaweza kuongeza alama zaidi ya hapo, ila mpala hapo mahesabu yapo hivyo, sasa unachobisha ni kipi? Kwamba 1+1 sio mbili au?
 
matatizo ya kutembea na calculator
 
Samahani kumbe mnateseka kwa SIMBA kuwa juu yenu huko CAF
 
Mahesabu ya rank za MSIMU HUU wa 2024-25 zinakomea msimu wa mwaka jana lakini bado tupo msimu huu kwa hiyo hata mshabiki wa Simba akitoka akajigamba yupo sahihi. Hizo ndiyo rank ambazo hesabu zake zimekamilika na ndiyo rank zinazohesabika kuwa ni za msimu huu.

Kuhusu rank za msimu wa 2025-26, bado mahesabu hayajakamilika maana inahitaji kujua timu zitaishia wapi mwisho wa msimu huu.

Narudia tena, katika mahesabu yenu mnaishia kuangalia hadi robo kwa sababu mnajua Simba ina nafasi zaidi ya Yanga kwenda mbali zaidi ya hapo.

Tuchukulie kama mnavyotamani Simba na Yanga zote zimeishia robo fainali mwisho wa msimu, je Berkane na USMA nao hawatavuka kwenda nusu fainali au zaidi? Je Pyramids au Al Hilal hawawezi kufika fainali? Unadhani yote hayo yakitokea Yanga bado itakuwa namba 5?

Mnaignore factors nyingi ili kufurahisha calculators zenu.
 
Jipe muda wa kutafakari hata mambo mengine
We Toka asubuhi unabishania rankings za Simba
Hizo rankings zitakupa ada ya mtoto, biashara. K
Unakaza sana kwenye ushabiki wa Simba.
Jadili kidogo, Fanya harakati zingine
 
Wewe tulia mbona wenge sana,,subilia kinachofata utapata majibu yako vizuri shida nini!
 
Mkuu utakesha kumuelewesha uyo wajiandae tu kisaikolojia ni suala la muda tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…