Kilele cha maadhimisho ya siku ya mtoto wa wa Africa, yapi maoni yako?

Kilele cha maadhimisho ya siku ya mtoto wa wa Africa, yapi maoni yako?

Sipendi Uchawa

JF-Expert Member
Joined
Dec 19, 2016
Posts
8,119
Reaction score
12,929
Habarini za leo ndugu zanguni. Natumai hamjambo na mapambano ya kila siku yanaendelea, kila mmoja anapambana kuhakikisha anapata riziki yake.

Kama tujuavyo kuwa kila ifikapo 16/06 ya kila mwaka huwa kuna maadhimisho ya siku inayofahamika kama siku ya mtoto wa Afrika ili kuenzi mauaji ya watoto yaliyofanyika nchini South Africa katika maandamano yaliyofanywa na watoto hasa wanafunzi kudai usawa katika elimu na mambo muhimu katika jamii. Hii ni siku ambayo imejaa kumbukumbu ya majonzi hasa kwa watu waliopoteza ndugu zao katika mauaji hayo.

Swali ambalo nimekuwa nikijiuliza mara nyingi ni, Je! Kwanini hii siku badala ya kutumika kumjenga mtoto, imekuwa ikitumika kumufanya mtoto kuwa kiumbe duni ambacho hutegemea huruma badala ya kufundishwa jinsi ya kujisimamia ili baadaye kuwa na jamii bora? Utakuta watoto wanaelezewa haki zao na jinsi zinavyokandamizwa bila kuelezwa wajibu wao katika kupata haki yao.

Yapi maoni yako kama mdau wa malezi na mzazi pia? Karibuni katika mjadala huu ili ikiwezekana siku za usoni siku hii itumike kuwajenga watoto ili kutengeneza kizazi cha Afrika imara isiyotegemea siku moja katika mwaka kutekeleza wajibu wake katika malezi.
 
Back
Top Bottom