Kilele cha Siku ya Sheria 2022: Rais Samia ataka Utu kuzingatiwa katika utoaji wa Haki. Anuani za makazi kukamilika kabla ya Sensa ya Watu na Makazi

Kilele cha Siku ya Sheria 2022: Rais Samia ataka Utu kuzingatiwa katika utoaji wa Haki. Anuani za makazi kukamilika kabla ya Sensa ya Watu na Makazi

The Sheriff

JF-Expert Member
Joined
Oct 10, 2019
Posts
747
Reaction score
2,112
Leo Februari 02, 2022 katika ukumbi wa Chinangali Park, Dodoma Mhe. Samia Suluhu Hassan ameshiriki kwenye kilele cha maadhimisho ya Siku ya Sheria nchini akiwa kama Mgeni Rasmi.

Kauli Mbiu ni: Zama za Mapinduzi ya Nne ya Viwanda, Safari ya Maboresho Kuelekea Mahakama Mtandao



UPDATES:

RAIS SAMIA SULUHU HASSAN

Maboresho ya Teknolojia katika Mahakama

Mmeonesha nia thabiti na ya dhati kuonesha kuwa Tanzania na Wadau wote wa Haki sasa, hasa wale wanaopata changamoto kufikia huduma za Haki mahakamani wanazipata kwa wakati na kwa gharama nafuu.

Wakati nikilihutubia Bunge la 12 hapa Dodoma Aprili 2021 niliahidi kuwa, pamoja na miundombinu migumu, Serikali itaimarisha miudombinu laini – hususani ya teknolojia.

Nimefurahi kuwa kaulimbiu ya siku ya leo ni Zama za Mapinduzi ya Nne ya Viwanda, lakini specifically, Safari ya Maboresho Kuelekea Mahakama Mtandao.

Nawapongeza kwa hatua za kutafuta teknolojia yenye program za kisasa, ambazo si tu zitakuza matumizi ya Kiswahili katika kutoa huduma za Kimahakama, bali pia zitatoa nafasi kwa Kiswahili kupata unukuzi (transcription) kwa lugha nyingine lakini hasa Kiingereza.

Kupitia wimbi la 4 la mapinduzi ya Viwanda, nchi yetu kwa sifa zake imeendelea kupokea wawekezaji na wafanyabiashara kutoka nchi mbalimbali. Kwa kuzingatia ukweli huo tunaendelea kuimarisha teknolojia ya habari na mawasiliano kwa kiasi kikubwa ili tuendane na ulimwengu.

Tanzania hatuwezi kubaki nje ya Mapinduzi ya Nne ya Viwanda ambayo yanaendelea kubadilisha kabisa mizani ya ushindani katika shughuli zote za kibinadamu zikiwemo za uwekezaji na mazingira ya biashara.

Tupo tayari kutumia njia za kisasa kujenga uwezo na uchumi imara unaoweza katika masoko ya ndani, ya nje na yale ya kikanda.

Ili kufanikisha lengo hilo, ni lazima kuiboresha sekta ya Sheria na utoaji haki nchini ili iweze kukabiliana na migogoro ya na mashauri ya biashara na kutoa ufafanuzi wa kisheria katika masuala ya uwekezaji na biashara wakati wowote.

Kama mwekezaji amezongwa saa 8, 6 usiku aingie tu kwenye mtandao apate majibu kutoka mahakama zetu.

Kila palipotokea mapinduzi ya viwanda pametokea mabadiliko siyo tu yamebadilisha binadamu anavyofanya kazi na aina za kazi ambazo zimekuwepo katika mwakati wa mapinduzi husika, bali hata katika mifumo ya elimu inayotlewa na vyuo na namna wahitimu wanavyotayarishwa.

Ni matumaini yangu kuwa, usimamizi na ufuatiliaji wa shughuli za Mahakama utaendelea kuimarika au kuimarika zaidi kutokana na matumizi ya Mifumo ya TEHAMA ambayo tayari imeshaanzishwa ndani ya Mahakama zetu

Upunguzaji wa gharama ndani ya mahakama
Suala la upunguzaji wa gharama ndani ya mahakama ni muhimu sana kwasababu tutakapoweza kupunguza gharama katika matumizi mengine ndipo tutakapopata fedha ya kuweka kwenye yale muliyoyaomba.

Kwa bahati mbaya serikali haiwezi kutoa haki bila Mahakama zetu zilizopewa jukumu kisheria. Hapa niendelee kusisitiza kwa watendaji wa mahakama wenye dhima ya kutenda haki kuendelea kufanya hivyo bila kufungwa sana na masharti ya kiufundi.

Utu uzingatiwe katika utoaji wa Haki
Na hapo masharti ya kiufundi nina maana gani? Kwamba Mwananchi anapoleta kesi yake mahakamani, hajui chochote, hajui apite njia gani. Anategemea Wakili kwa mwenye uwezo wa kuweka Wakili na asiye na uwezo Serikali tuna jukumu la kumpatia Wakili lakini sidhani kama wote wanapata mawakili.

Anayedhulumu, anayeshitakiwa ana uwezo wa kuweka wakili. Kwahiyo mawakili hawa hutumia njia zao za kiufundi – jinsi ya kukwepa vipengele – na kuweza kumtia hatiani, au kumnyima haki mwenye haki.

Kwahiyo, niseme tu kwamba Mahakama pamoja na kutumia vifungu vya sheria kiufundi mahakamani, kubwa kwa wewe unayetoa haki ni kuisikiliza nafsi yako, je, hapa natenda haki au sitendi haki?

Na imesemwa hapa na “Jaji” Hoseah kwamba katika kutoa maamuzi, Utu nao utazamwe. Na tunapozungumzia utu wa mtu ni yule unayemhukumu lakini na wewe unayetoa hukumu. Utu wako unakutumaje. Uchukue fedha udhulumu haki ya mtu au umpe aliyetumia umahiri na ufundi wa vifungu kumnyima haki mwenye haki.

Kwahiyo, utu wa mtu ni component muhimu katika kutoa maamuzi yenu. Niwaombe sana mkafanye hivyo.

Upungufu wa watendaji wa mahakama
Jambo lingine ni upungufu wa watendaji wa mahakama katika ngazi zote. Na nilikuwa na numbers. Nadhani tupo vizuri kwenye Mahakama ya Rufaa; wanatakiwa 28 wapo 26. Tuko vizuri.

Lakini tunavyozidi kwenda chini namba inapungua. Hilo tutaliangalia.

Rushwa bado ipo ndani ya sekta ya Mahakama
Bado kuna vijipesapesa vinatembea. Inawezekana si katika ngazi za juu, lakini huko ngazi za chini bado vijipesa vinatembea ambavyo vinansababisha mwenye Haki anyimwe Haki. Au kwa lugha rahisi niseme Rushwa -- bado ipo ndani ya sekta ya Mahakama.

Anuani za makazi kukamilika kabla ya Sensa ya Watu na Makazi, 2022
Umesema suala la anuani za makazi na postcodes likamilishwe na kwamba hii itasaidia sana sekta ya mhimili wa Mahakama hasa tunapotumia Mahakama Mtandao kwasababu watu wanaoleta mashauri lazima wajulikane wapo wapi. Hili nalo nikuhakikishie tunalifanyia kazi sasa hivi na tutakamilisha kabla Sensa ya Watu kwasababu ni component muhimu kwenda kwenye Sensa ya Watu na Makazi.
 
Tunamuombea abadilike leo aoneshe nia ya kutenda haki na kudumisha utawala bora
 
Leo Februari 02, 2022 katika ukumbi wa Chinangali Park, Dodoma Mhe. Samia Suluhu Hassan ameshiriki kwenye kilele cha maadhimisho ya Siku ya Sheria nchini akiwa kama Mgeni Rasmi...
Mbona mama anapozungumzia suala hili la rushwa huwa hatoi way forward? anazungumza tu halafu inaishia hapo hapo kwenye mdomo tu?

Kama ana hakika rushwa ipo kwanini hachukui hatua hapo hapo?
 
Mnaoshughulika na kesi ya Mbowe na zingine huko mahakamani, bila shaka mmemsikia mheshimiwa Rais Samia akisisitiza kutenda haki huko mahakamani. Sasa kazi kwenu. Hakika tendeni haki.

Kumbukeni Rais amelisema hili, kwa kuwa anajua bayana kuwa haki haitendeki huko mahakamani. Sasa ukizingatia kuna kesi ya Mbowe, ambayo inavuta hisia Kwa watu wengi wanaoifuatilia ndani na nje ya nchi, Rais keshawambia tendeni haki.

Hofu yangu ni kwamba kama haki haitatendeka, na ikaonekana ikitendeka, kutazua mtafaruku katika mioyo ya watu ambayo itapelekea kujenga chuki Kwa serikali, jambo ambalo Kwa hakika halitakuwa na tija kwa yeyote.
 
Haki ni ngumu....2025 wakimwambia, kama tukifuata haki hapa hata asilimia 25 hatufikishi ila tukipiga makalatee tunafikisha 57.....atachagua haki au makalatee?.
 
Back
Top Bottom