Kili Music Awards 2011

donlucchese

JF-Expert Member
Joined
Mar 23, 2011
Posts
17,128
Reaction score
21,885
Unafkiri ni kina nani wataibuka vinara?

UPDATES:

20% kashinda tuzo 5 kwa mpigo!
 
Wasanii wote wa THT wataibuka vinara sababu ya Kina Kavishe wana waabudu kina Ruge. Unadhani mtuwa kijini kama Kavishe kaja mjini halafu kukaa table moja na Ruge unadhani jama hajaona kaukata? .tuone uchakachuaji utakavyo tawala .
 
Ila maneno yako ya kweli,cku hz wanachakachua sana
 
Naona ITV wanaonesha live............Ila picha zimefifia ile mbaya
 
Wimbo bora wa Asili tuzo imekwenda kwa SHANGAZI wa Mpoki.........

Ukisikia Ujinga wa tuzo hizi ndio huu....dah
 
Wimbo bora wa Asili tuzo imekwenda kwa SHANGAZI wa Mpoki.........

Ukisikia Ujinga wa tuzo hizi ndio huu....dah

Hawa jamaa wapuuzi sijapata kuona...........wimbo wa SHANGAZI!!!!!!!!!!!!..... My foot, eti Mpoki kawashinda Mpoto (Adella), Off Side Trick na Bi Kidude (Ahmada), Mataluma (Kariakoo) na Kimbelembelea
 
Hawa jamaa wapuuzi sijapata kuona...........wimbo wa SHANGAZI!!!!!!!!!!!!..... My foot, eti Mpoki kawashinda Mpoto (Adella), Off Side Trick na Bi Kidude (Ahmada), Mataluma (Kariakoo) na Kimbelembelea
Nilitarajia aidha Adela au Kariakoo mmojawapo unyakue zawadi. Ya Mpoki imenichekesha
 
Sasa nami naangalia... Wimbo wa Taarabu naamini atashinda mwenye wimbo wa MAMA NIPE RADHI
 
Wimbo Bora wa TAARAB ulioshinda ni;

wimbo wa JAHAZI MODERN Taarab,sijausikia jina
 
Jahazi Modern Taarab sijajua ni wimbo gani, taarabu imeniacha kando
 
Sasa nami naangalia... Wimbo wa Taarabu naamini atashinda mwenye wimbo wa MAMA NIPE RADHI

Hajashinda mkuu,mi mwenyewe nilijua ndo utashinda wimbo huo wa ISHA na mamaye RUKIA lakini eti wamempa mzoefu Mzee Yusuph na JAHAZI yake....lol
 
wimbo wa jahazi ulioshinda ni my valentine

huu hauna shaka binafsi naamini unastahili sana tu kushinda

ila maneno ya mzee yusuph akipokea tuzo yameniacha nikitafakari maana yake, amesema ANAEOMBA CHUMVI,HUOMBEA MBOGA YAKE

HAKUSEMA LOLOTE JUU YA NSIBA WA WANAMUZIKI WENZIE NA MIND YOU WENGI WA HAO WALIOFARIKI WALITOKA KWAKE
MAY BE HAMAANISHI HAYO
 
Wasanii hawa wa BONGOFLEVA ni BURE kabisa......Hawawezi kuimba 'live' hata kidogo
 
Huyu bwana mdogo DIAMOND anahema mpaka anatia huruma................Hawezi kuimba kwa kupigiwa vifaa moja kwa moja yaani
 
Mbona sauti kwa tv zinafade sana? Mpaka ladha flan inakosekana

ukijumlisha mc wenyewe wanakosa mvuto na tuzo kwenda kusikostahili kama ile ya mpoki basi tuzo zimeanza kwa dullness
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…