Kilichochelewesha mradi wetu wa LNG ni siasa nyingi, mimi naumia sana Msumbiji kututangulia kusafirisha LNG

Kilichochelewesha mradi wetu wa LNG ni siasa nyingi, mimi naumia sana Msumbiji kututangulia kusafirisha LNG

Meneja Wa Makampuni

JF-Expert Member
Joined
Jul 7, 2020
Posts
7,899
Reaction score
10,415
Screenshot_20221115_113257.jpg


Nimeanza kufuatilia mwenendo wa sekta yetu ya gesi tangu mwaka 2011.

Toka kipindi hicho mpaka leo yamezungumzwa mengi sana kuhusu sekta yetu ya gesi.

Sekta yetu inakasoro nyingi sana zinazokwamisha maendeleo ya miradi yetu.

Siasa iliyokua ikitumika ndio imechelewesha sisi kuanza mradi wa LNG mapema.

Kiukweli mimi nimeumia sana kusikia Msumbuji wao tayari wameshaanza kusafirisha LNG sisi ndio kwanza hata ujenzi hatujaanza. Na ujenzi unachukua miaka mingi.

Utoaji wa ajira kwa watoto wetu wanaosoma fani za mafuta na gesi nao sio rafiki. Watoto wetu waliofaulu vizuri wanalandalanda mtaani na kufanya kazi za ajabu.

Na kazi wanazowatolea watoto wetu ni moja, mbili au tatu. Na hizo kazi haziwalengi walengwa wa hiyo sekta ilimradi tu watu wapate ulaji. Ndio maana tunashindwa kusimamia mambo haya.

Ajira zimeshikwa na wachache miradi inazidi kuchelewa siku zinaenda tu.

Ukifuatilia yanayo endelea Msumbiji huwezi ona mtalaamu wa mafuta na gesi analandalanda mtaani. Sera zimewekwa vizuri wataalamu wa mafuta na gesi wananufaika na ajira zao za mafuta na gesi na wanafanya kazi.

Tunakupongeza sana waziri Makamba tunaelewa unafanya kazi nzuri sana kwenye sekta yetu ya mafuta na gesi asilia hapa nchini.
 
Tatizo ni CCM kila mradi wenye tija kwa Taifa wanaona dili na kuficha ficha, sijui wakiwaambia watanzania undani wa mikataba, volume ya gasi na matazamio ya mapato ili na wao wakachangia mawazo sijui wanaonaje.

Kuna project ya LNG tunaambiwa wame sign sasa hatujui ndani yake kuna nini au ndiyo siri sirini.

CCM ni tatizo, ni donda ndugu la watanzania. Maji tu yametushinda itakuwa hiyo LNG.
 
Back
Top Bottom