Afisa wa Magereza amesema hayuko tayari kwa utaratibu wa virtual
Mheshimiwa Mrema wakili wa serikali anatambulisha jopo la mawakili wa serikali kwa upande wa jamhuri yupo pia Thawabu Issa, Cathbert Mbiringe, Harrison Lukosi.
Upande wa utetezi wapo mawakili wafuatao
1. Mpale Mpoki
2. Dr. Rugemeleza Nshala
3. Peter Kibatala
4. Hekima Mwasipu
5. Paul kisabo
6. Deus Sinda
7. Sisty Masawe
8. Gloria Ulomi
9. Fredrick Msaki
10. Jebra Kambole
11. Maria Mushi
12. Dickson Matata
13. Michael Lugina
14. Catherine Michael
15. Nashon Nkungu
16. Michael Mwangasa
17. Ikoti Lissu
18. Jacob Mogendi
19. Deogratias Mahinyila
Job Mrema, Wakili wa serikali anasema shauri hili lilikuja tar. 24/05 na lilipokuja upande wa jamhuri uliomba ahirisho kutokana na mazingira yaliyojitokeza kutokana na mshitaki Tundu Lissu kutofika mahakamani kama alivyotakiwa kufika na jamhuri kuomba ahirisho ili kupisha mawakili kuongea na mteja wao ili kufika mahakamani na kusomewa hoja za awali.
Hivyo basi baada ya utangulizi huo, siku ya leo upande wa jamhuri uko tayari kujibu hoja za upande wa utetezi. Na tuko tayari.
Mpale Mpoki na sisi kwa upande wa utetezi tuko tayari ila kuna preliminary issue moja lazima tuiseme maana muda huu nyumbani kwa mshitakiwa polisi wamezingira nyumba ya mshitakiwa lazima tuliweke sawa.
Hakimu anasema hilo tutalizungumza baadae kwa sasa acha tuendelee na upande wa serikali wajibu hoja zao.
Job Mrema anaanza anasema hoja ya kwanza, upande wa utetezi ulipinga ahirisho, tunaomba kusema kuwa msingi wa upande wa jamhuri kuomba ahirisho la siku 30 upo kwenye kifungu cha 225(2) cha CPA kwasababu kifungu kimeweka ukomo kuwa mahakama inaweza kuahirisha shauri kwa siku zisizozidi 30 kama mshitakiwa yuko nje ya dhamana. Na Mh. Lissu alipata dhamana tar. 10/04 mwaka huu hivyo tuliomba ahirisho hilo.
Mtobesya na Kibatala walipinga jambo hilo ambalo tuliomba lakini sisi tunaona kwamba mahakama itumie kifungu cha 225(2) cha CPA.
Wao hawakusema wanaomba ahirisho la siku ngapi kama wanapinga la siku 30.
Anaingilia Kibatala anasema anapingamizi na anasema nitaongea kwa kingereza kwasababu wapo mabalozi hapa. Huyu Mrema wakili wa serikali anadanganya sisi kukataa ahirisho la siku 30 tulitoa hoja za kisheria na sio maneno tupu. Mheshimiwa anasema Mrema zingatia hilo
Anaendelea sasa Job Mrema, kuhusu jambo la mawakili kuzuiwa kumuona mteja wao, kuzuia wananchi kuingia Kisutu na kuwazuia ndugu kumuona mteja mahakamani.
Majibu yetu ni kwamba tunaomba mahakama ipuuze hoja hizo kwasababu
1. Mahakama hii haina mamlaka kusikiliza hoja hizo kwasababu zinahusiana na tuhuma zinazotuhumu baadhinya watumishi wa umma kuwa wamekosea katika utendaji. Sisi tunaiomba mahakama ifahamu kwamba kama kuna hoja inahusu tuhuma za polisi au watu wengine basi wakachukuliwe hatua kwa kushitakiwa. The Law Reforms Fatal Accidents Miscellaneous Provision Act Cap. 310 R.E 2022 pamoja na kanuni zake.
Kwahiyo kwa hapa tuwaache polisi waendelee na mambo yao huko maana maana mahakama hii haina uwezo wa kusikiliza mambo wanayoyafanya sasa hivi Polisi huko nje. Acha waendelee tu.
Pia tunaomba kufanya marejeo ya shauri la Paul Kaunda vs Spika wa Bunge na Mwanasheria wa serikali Civil Appeal No. 167/2021.
Mahakama ilisema maana ya judicial review hivyo tuhuma kwa jeshi la polisi, jeshi la magereza na baadhi ya maafisa hivyo mahakama isiingie kwenye mtego huo.
Kwenye kumbukumbu za shauri hili Wakili Mpoki na Mtobesya na Kambole walikuwa sehemu ya shauri tulilosema sasa kwanini leo wanaomba jambo hili tena ni kama wanaitega mahakama.
Jamhuri tunasema haya ni matumizi mabaya ya mahakama na yamejikita katika kuondoa haki za mshitakiwa kusikilizwa kwa wakati. (Mawakili wanacheka) 😂
Wanashangaa kusikia wakili wa serikali anasema kuhsuu haki za mshitakiwa.
Anaendelea Job Mrema, Wakili wa Serikali. Pia tunaomba kuweka msisitizo shauri la John Mwombeki Byombalirwa vs Regional Commissioner and others, 1986 TLR na shauri la AG vs Rev. Christopher Mtikila 1995 TLR
Tumerejea mashauri haya kwa maana yameongelea msingi wa judicial review bila kuathiri hayo yote..
Mheshimiwa Hakimu anasema kwani hoja ya kwanza umemaliza au bado uko hapo kwenye hoja hiyo?
Anasema bado hoja ya kwanza. Na anaendelea Job mrema anasema
Majeshi haya yanafanya kazi kwa mujibu wa sheria na weledi mkubwa sana. Tunaomba kurejea kanuni Prison Regulations, 1968. Pia katiba ya Jamhuri ya Muungano ibara ya 30(1) ya 1977.
Hivyo hakuna haki inayokuja bila wajibu. Hoja yetu ni kwamba ili uweze kupata haki yako timiza wajibu pia.
Bwana Tundu Lissu kwa mujibu wa kanuni ya 10(2) hizo nilizosema zimetoa utaratibu wa kuwasiliana kwa njia ya kuandika barua.
Mrema amepotea kidogo anasema network ilicheza. 😂
Anaendelea Job mrema kuwa kwa mujibu wa kanuni hiyo na baadaa ya sisi kuwasiliana na Magereza ili kuuliza kama aliwasiliana kwa njia ya barua maana hapaswi kuwasiliana kwa njia nyingine hata mawakili wake hawajaonesha kuwa waliandika barua kokote maana ndio utaratibu.
Kwahiyo Magereza huwezi kwenda bila kufuata utaratibu wao ikiwemo huo wa kuandikiana Barua.
Hivyo basi barua tunayosema, Bwana Tundu Lissu alipaswa kuandika barua kutambulisha mawakili wake kwa jeshi la magereza.
Kwa kumbukumbu zetu hakuna barua iliyowahi kuandikwa na wakili au mteja wake kujitambulisha na Wakili Alute pia anasema alizuiliwa na yeye pia afahamu utaratibu wa magereza ambao wanahitaji kufahamu ujio wa Wakili.
Kwa kuhitimisha niseme upande wa jamhuri tunaomba mahakama izitupilie mbali na pia mawakili upande wa utetezi hawajasema kama waliwahi kutoa barua au kufuata taratibu za magereza na pia haki na wajibu vinakwenda sambamba.
2. Hoja nyingingine kuhusu kifungu cha 192(1) cha CPA kwamba mahakama haiwezi kuendelea kwa njia ya mtandao hasa ukizingatia kifungu cha 186 cha sheria hiyo. Tunaomba mahakama isizipe nguvu hoja zao kwa namna tutakavyoeleza hapa
Job Mrema anaendelea kueleza huku tunasikia kama mtu anagonga meza huko upande wake.
Anasema maelezo ya awali yatasomwa katika mahakama ya wazi akiwepo mshitakiwa. Tunaomba kuieleza mahakama kwamba usikilizwaji wa shauri hili kwa njia ya mtandao inawezekana na kwamba kupitia mtandao ni mahakama ya wazi pia.
Tumepitia mawasilisho haya tumeona wanachanganya kati ya mahakama ya wazi na mahakama kwa njia ya mtandao. Sio sahihi kwamba mtandaoni haitakuwa mahakama ya wazi.
Hivyo mahakama ya wazi sio majengo. Na jamhuri tumekwenda mbali zaidi upande wa Black's Law dictionary ukurasa 1263 inatoa tafsiri ya Open Court. Hasa ukisoma tafsiri ya pili acha ya kwanza hiyo.
Mheshimiwa kuhusiana na suala la utaratibu kuwa haiwezekani kwa nyaraka kusainiwa kwa nyaraka wakati mtuhumiwa hayupo. Utaratibu umeanishwa kwenye kanuni juu ya nyaraka zinavyoweza kuwasilishwa kwa pande zote kupitia mfumo wa mahakama.
Sasa upande wa Jamhuri tunaona mazingira yapo kwenye kanuni kabisa.
Tunaomba kuieleza Mahakama kwamba sheria ina namna mbalimbali unayoweza kuisoma na kupata maana yake. Huwezi kusoma kifungu hiki bila kusoma sheria nyingine ili kupata maana yake vizuri.
Tunasema hivyo kwasababu kifungu cha 4 cha Judicature and Applccation of Laws Act (JALA) Cap. 358 kimempa mamlaka jaji mkuu kutunga kanuni ambazo zinaifanya mahakama kutekeleza majukumu yake.
Hoja yetu ni kwamba hizi kanuni zinaeleza zinaweza kutumika kwenye mashauri ya madai na jinai pia. Sasa hoja yetu ni kwamba Wakili Kibatala aliposema kifungu hicho kinajitosheleza na alikuwa anapotosha.
Tunaomba kurejea shauri la Boniphace Kuandakira Tarimo vs R mahakama ilisema sio salama kutafsiri sheria kwa kuacha sheria nyingine.
3. Hoja ya tatu kuwa mahakama hii ni Functus Officio hii nayo tunapinga kwa shauri hili na amri zilizotolewa mahakama kwa nyakati tofauti ni amri halali kabisa.
Hakuna mahali kokote ambako mahakama imetengua au kurekebisha amri zake.
Job Mrema anasema mahakama hii pia ifuate uamuzi kama ukiofanywa kwenye kesi ya uhaini ya Mh. Lissu.
Kibatala anasema tunapinga hilo maana hiyo kesi hata haijaamuliwa.
Mrema anasema namuona Kibatala anataka kujaribu kuweka pingamizi. Kibatala anasema nimeweka pingamizi sio najaribu kuweka.
Kuna mwamba yuko online wanaofuatilia ameachia wimbo wa Chadema wa Naapa naahidi Mbele ya Mungu Chadema nitakulinda. Kicheko kimeibuka mahakamani hapa.😂😂 Wanashangaa watu walivyovurugwa huko. Watu wa IT wamemtoa. Job Mrema anaendelea sasa
Kuhusu kutolewa kwa Tundu Lissu kutoka Keko kwenda ukonga kuwa ilikuwa kinyume na sheria. Sisi wasilisho letu kuwa magereza inafanya kazi kwa weledi na wanafanya kazi kwa sheria na mahakama hii haikuwa na order kuwa mshitakiwa apelekwe wapi?
Naomba kuhitimisha kwamba, mahakama izingatie ombi la Jamhuri shauri liahirishwe kwa siku 30 ili mawakili wa utetezi waweze kuwasiliana na mteja wao na kujiandaa kwa ajili ya maelezo ya awali.
Mahakama ione hapakuwa na ukiukwaji wa sheria na hoja nyingine yale ambayo tumeeleza jamhuri kuomba siku 30 nalo pia likubaliwe kwa kuahirishwa.
Na kuhusu kanuni ya 10 kutoa notice ya siku 7 haki ya mshitakiwa haijazuiwa.
Huyu ndugu huku online amerudi tena anapiga zake wimbo wa naapa naahidi mbele ya Mungu Chadema nitailinda. Watu wanatikisa tu vichwa hapa.Job Mrema amemaliza upande wa Jamhuri sasa tunahamia kwenye rejoinder submission.Mpale Mpoki anaanza kwa kusema hapa, kabla ya yote pia naomba Wakili Jeremiah Mtobesya, Edward Heche nao pia waingie kwenye Corum. Mpale Mpoki anasema kuhusu Judicial Review as alternative remedy litajibiwa na Jebra Kambole.
Mimi Mpale Mpoki nitasema kuhusu suala la open justice. Dr. Nshala atasema kuhusu suala la kanuni za magereza na Kibatala pia. Peter Kibatala atasema kuhusu kuahirisha kesi hii kwa siku 30. Pia atasema kuhusu Functus Officio. Na mwisho Mtobesya atasema kuhusu jurisdiction ya mahakama hii kwenye committal proceedings.Jebra Kambole anaanza na watu wa mtandaoni wanashauri waongee Kiswahili.
Jebra anaongea Kiswahili. Anasema kuhusu maombi haya kufanywa kwa Judicial Review, mshitakiwa yupo gerezani na jambo hilo halibishaniwi. Kwa vile yuko gerezani mahakama hii ina mamlaka ya kuangalia nini kinamtokea huko gerezani. Ni wajibu wa mahakama hii. Mawakili wa utetezi hoja yetu ni kwamba mshitakiwa hapati huduma sahihi akiwa huko gerezani.
Wenzetu upande wa serikali wanasema tulipaswa kuyapeleka malalamiko yetu kwa njia ya Judicial review. Hili sio sahihi kwasababu zifuatazo.Wakati mawakili wa utetezi wanatoa submission hakuna wakili yoyote aliyeomba Judicial review hapa. Network imekatika hapa mheshimiwa anasema tusubir kwanza.
Jebra Kambole anasema sisi hatujaomba judicial review. Hatujaitaja hiyo sheria sio kwasbabu hatuijui kwanza mawakili wautetezi hiyo judicial review kwa wingi wetu hizo ndio kesi zetu huko ndio tulikobobea. Kwahiyo tunayafahamu hayo mambo vizuri. Wao kutushauri hilo ni kujielekeza vibaya kabisa. Mshitakiwa yuko Magereza kwahiyo welfare zake zinapaswa kulindwa na mahakama hii na sio kwenda kwenye judicial review Sisi upande wa utetezi hatuamini kwamba mahakama hii haiwezi kutoa summons.
Kwamba kuwataka maafisa wa magereza wanaokiuka taratibu za sheria twende tukafungue kesi ya judicial review. Lakini pia Mheshimiwa tufanye sisi ni waongo na Lissu hajanyimwa hizo haki zake. Sasa wanaogopa nini kuwaleta hao maafisa wa magereza ili waje kutoa ushahidi wa uongo wetu ni upi? Kwanini wanaogopa kuwaleta hao watu wa magereza waje watuambie ukweli kuhusu nini anafanyiwa Tundu Lissu huko magereza na je haki zake anapatiwa.
Kesi waliyoitoa hapa mahakamani inahusiana na haki za Mbunge nashangaa wao wanaileta kwenye mambo ya magereza na haki za watu waliopo kizuizini. Labda kama wenzetu wamechanganyikiwa. Lakini kesi hiyo na hata ile ya Mwombeki haihusiani kabisa. Mahakama hii hatujaiomba ifanye judicial review bali tunataka mahakama ilinde haki za mshitakiwa. Sasa hatujui uoga wa wenzetu unatoka wapi kwenye eneo hilo.
Mpale Mpoki anaanza anasema kutetea haki za Mshitakiwa na mtu aliyepo magereza sio kuharibu mwenendo wa kesi kwa mawakili. Kukaa kimya kuhusu haki za mteja wetu ni sawasawa na sisi mawakili kuwa hatuna maana yoyote kwake na tusingepaswa kuwepo hapa kumtetea lazima tuseme mambo haya. Sasa kuhusu mahakama ya wazi tulitaja kifungu cha 186 cha CPA. Mahakama ya wazi maana yake ni freely kwa public kuatteend hiyo freely maana yake sio kwamba hawalipia hela. Maana yake ni kwamba watu watahudhuria bila kusumbuliwa na polisi. Hiyo maana imetolewa kwenye Collins Dictionary.
Hiyo maana inatofautisha maana ya Chamber Court na Open Court ambayo umma unakuwa huru kushiriki.Ili kesi ifanyike kwa njia ya mtandao lazima tuangalie interest of justice na sio interest of justice ya serikali peke yake. Aliyefanya uamuzi wa kusema kesi hii isikilizwe kwa njia ya mtandao haipaswi mtu huyo aamue tu mwenyewe ofisini kwake bila kushirikisha pande zote. Na hapa sisemi kama wewe ndio uliamua hivyo. Watu wanacheka.
Hakimu anasema unajuaje kama sio mimi? Mpoki anajibu ninachosema yoyote aliyeamua hivyo hakuwa sahihi na sio sahihi kabisa kufanya hivyo. Ni muhimu pia kueleweka kuwa sheria ikisema mahakama itaamua on its own motion haina maana kuwa mahakama itaamua bila kusikiliza wahusika. Nasisitiza yeyote aliyetoa amri ya kwamba kesi isikilizwe kwa njia ya mtandao alipaswa kuwasikiliza pia na kutoa maelekezo hayo jambo ambalo halikufanyika kuna mtu alijiamulia akiwa mwenyewe na amekaaa mahali fulani huo sio utaratibu wa kuendesha kesi na mahakama zetu.
UPDATE