Kilichojiri mahakamani kwenye kesi ya Tundu Lissu, leo Aprili 28, 2025

Kilichojiri mahakamani kwenye kesi ya Tundu Lissu, leo Aprili 28, 2025

Hii kesi inaingia katika historia ya mapambano ya kudai mabadiliko na uhuru wa watanzania kutoka tawala dhalimu za CCM.

Lissu anaingia katika historia kama ambavyo Mandela na wanaharakati wengine duniani walivyoingia katika historia za kupigania uhuru na haki za watu katika mataifa yao.

Vitukuu na vilembwe wa Samia, Wasira, Nchimbi na wa watawala wengine wa sasa, ni miongoni mwa watu wataokuja kusoma historia ya anguko la CCM na matendo ya babu zao walipokuwa madarakani. .

Ni historia ambayo kwa namna moja au nyingine, ni lazima itagusa kesi kama hizi za wazalendo hawa wa leo wanaojitoa kuongoza mapambano ya kuondoa utawala huu katili wa CCM.

Halikadhalika, picha za wote waliovunjwa mikono na miguu na Polisi kwa kwenda mahakamani kufuatilia hii kesi, zitatumiika kama kumbukumbu mbaya na ya fedheha ya utawala huu wa sasa kwenye mapambano ya kudai haki na uhuru wa watanzania chini ya tawala hizi za CCM.

Yapo mazingira ambayo kesi inaweza kusikilizwa kwa njia ya mtandao, sababu yoyote ya msingi haijaelezwa kwanini mahakama haijasema sababu yoyote hadi leo.Kwahiyo nasisitiza takwa la kutolewa notice ya siku saba kusikiliza kesi kwa njia ya mtandao ni haki kabisa yenye msingi wa kikatiba. Sasa kutoa uamuzi kutoka kwenye droo na bila kuwashirikisha pande zote ni kinyume kabisa na haki za msingi katika kusikilizwa hizi kesi.

Athari za maamuzi yoyote yanayofanyika bila kusikiliza pande zote ni maamuzi batili kabisa.Na kwa vile mtuhumiwa pia ni mwanasheria na anajua haki zake. Ndio maana hataki kushiriki kuja mahakamani kusikiliza kesi yake.Na ukisema public itasikiliza kesi hii kupitia kuingia kwenye link.

Sasa na wale ambao wanatumia simu za vitochi wanaingiaje? Unawanyima haki yao ya kufika na kushuhudia namna kesi inavyoendeshwa. Hata tungesema wafuatilie kupitia waandishi wa habari. Hao waandishi wenyewe humu mahakamani siwaoni na wanakatazwa kuingia mahakamani pale Getini. Haya ni mambo ya ajabu kabisa.Wako watu wanaweza kutembea kwa miguu kutoka wanapoishi hadi hapa mahakamani. Ukisema waingie mtandaoni unawanunulia bando wewe?

Na je kama hawana simu au Laptop. Haya yote maana yake ni kwamba mteja wetu hajatendewa haki. Huyu Mzee Mpale Mpoki anachapa sana hapa. Anaonekana ana hasira angeweza kupiga hata mtu makofi isingekuwa mahakamani. Anaendelea kusema tunaomba Mteja wetu aruhusiwe kuja mahakamani kusikiliza kesi yake.

Huyu mwenye hofu kesi hii isikilizwe mtandaoni sijui ana hofu gani na kama anataka iwe hivyo atuite tuje tuzungumze hilo na aseme kuhusu hofu yake hiyo.Dr. NSHALA anaanza hapa amepewa nafasi na Mpale Mpoki. Dr. RUGEMELEZA NSHALA anasema ile tone ya Job Mrema wakili wa serikali alikuwa anazungumza kama anatufokea. Sasa kwanza Job Mrema ajifunze namna ya kuzungumza. Mimi nina miaka 30 ya uwakili napaswa kumfundisha mambo kama haya madogo madogo ajifunze. Amesema polisi wanafanya kazi yao kwa weledi. Nimeshangaaa.

Kuna ukiukwaji mkubwa wa kanuni za magereza na sheria za nchi kwa hao polisi. Anasema mteja wetu alipaswa kuwaandikia magereza barua. Sasa usomaji wangu wote wa hizi sheria ukisaidiwa na miwani pia sijawahi kuona huo utaratibu wa kuandika barua kwa mshitakiwa aliyeko magereza kwa kuelezea majina ya mawakili wake na ndugu zake watakaokwenda kumuona.

Mahakama kama kweli inaona na ina macho basi itaona sharti hilo la kuandika barua kuwatambulisha mawakili wake halipo na halijawahi kuwepo.Dr. Nshala anasema kanuni ya 12 ya kanuni za magereza inasema mfungwa au mahabasu ana haki ya kutembelewa. Na wao wamekiri kuwa mshitakiwa yupo na dhamana sasa magereza walipaswa kumleta. Hii kesi iliyopo kwako mshitakiwa ana dhamana.

Haki ya Wakili lazima ilindwe na utaratibu wa wakili kupewa simu akienda magereza ili azungumze na mteja wao. Si tungebaki nyumbani tuwapigie simu magereza halafu watupe hiyo simu tuongeee nae. Sio kwenda pale magereza halafu tunapewa simu tena. Huyu Tundu Lissu alipigwa Risasi 16 nani miongoni mwetu amewahi kupigwa hizo risasi?

Sasa huyu mtu anapaswa kupewa uangalizi wa msingi kabisa wa huduma za kiafya na uangalizi wake.Sheria zetu zinapaswa kuheshimiwa na kila mtu hadi serikali. Sasa serikali isipoheshimu hizo sheria maana yake hakuna haja tukawa na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kila mmoja aendelee kivyake kwenye hili taifa. Naomba kumkaribisha Wakili Kibatala.

Anaanza Kibatala sasa, Mheshimiwa kwanini Magereza tulipoanza leo hapa wametujoin na umewauliza mshtakiwa yuko wapi? Maana ya hilo zoezi ni kwamba magereza wanawajibika kwenye mahakama hii. Hivyo maombi yetu yanaelea kwenye misingi hiyo. Kwamba mahakama hii ina wajibu wakulinda haki za mshitakiwa ndio maana wapo hapa kujibu kuwa mshitakiwa amekataa kuja mahakamani.

Job Mrema anasema tunastahili mawakili kunyimwa haki ya kumuona mteja wetu kama mteja hatakuwa ameandika barua. Na amesema kuwa kwa mazoea aliyonayo ndio utaratibu. Sasa sisi hatujui ana mazoea gani na magereza. Lakini hoja ni kwamba wanakiri kuwa mimi waliniruhusu nionane na mteja sasa swali ni kwamba waliniruhusu kwasababu ya barua gani iliyokuwepo? Mbona waliniruhusu bila barua kama hoja ya barua ni ya maana?

Sasa nianze hoja ya Functus Officio ambayo wenzetu pia wamejaribu kuisemea. Katika mwenendo huu kulikuwepo na amri ya mahakama na pia kuna mabadiliko ya amri hiyo. Mahakama hii iliahirishwa na kusema tukutane tarrhe fulani hiyo ni amri tayari. Sasa amri ilitakiwa kuwa halali na kutekelezwa na sio kubadilika juu kwa juu bila pande zote kufahamu nini kinaendelea.

Sheria imetumia maneno open court hilo neno open sio nyimbo ya Zuchu ni mahakama ya wazi na kama ingekuwa haina maana ya kila mtu kuifikia basi neno open lisingekuwepo ingekuwa ni Court peke yake.

Baada ya ile Order (amri) kutolewa maana yake tulipaswa kukutana kama tulivyokutana siku Tundu Lissu amesomewa mashtaka. Wenzetu wanasema hakuna kilichobadilika, sasa mimi namuuliza kama hakuna kilichobadilika kwanini tuko hapa na haya mavideo na macamera na wao tunawaangalia kwenye matv yao haya.

Sasa swali la msingi ni kwamba ilikuwa sahihi mahakama kuamua yenyewe kuwa tusikilize kesi kwa mtindo huu? Jibu ni kwamba mahakama ilikosea kuamua bila kushirikisha pande zote na ina wajibu wa kujirekebisha na ikiona iliteleza itakuwa imelinda sana heshima yake kwa umma.

Kuhusu hoja ya ahirisho, ngoja nimkumbushe kuhusu kifungu cha 225 alichotaja yeye. Kwamba mshitakiwa akipewa dhamana atatakiwa kufika kwa muda na mahali. Maana yake ni kwamba mtuhumiwa akipewa dhamana atapaswa kufika mahali husika na tarehe husika aliyoambiwa. Haya tuseme asingekuwa Ukonga gerezani je angekuwa nyumbani kwake Tegeta angesema siji mahakamani mnisikilize kwa mtandao je mngekubali?

Hoja ahirisho la siku 30 na kifungu alichotaja kwanza kifungu hicho kinasema ahirisho lisizidi siku 30 sasa yeye anataka kutumia kifungu hicho ambacho msingi wake ni katazo. Na sheria iko wazi kwa mtu aliyepo magereza ahirisho halipaswi kuzidi siku 14. Na anaposema twende tukaongee na mteja wetu mtupatie hizo siku 30 nayo pia ni kama kuchanganyikiwa tu. Sisi tunasema magereza wanatuzuia kumuona wewe unasema tukaongee na mteja. Tunaongea nae kwa style gani?

Kuhusu hoja ya notice ya siku 7 kuwa haijatolewa wao wanasema kuwa ukiahirisha tutakuwa tumepata hizo siku 7 za notice. Nafikiri nalo ni kujielekeza vibaya kabisa. Tumeshaweka pingamizi ndio anasema sasa hivi kuwa notice tuchukulie ndio imetolewa kwa mtindo huo.

Anaendelea Kibatala, amesahau kujibu hoja kuhusu baada ya kufanya PH mshitakiwa anapaswa kusign sasa je atasign vipi? Wakati hayuko mahakamani. Au askari magereza atapanda bodaboda kwenda kusign halafu arudi hapa.

Anaingilia Mrema anasema kibatala anasema hatujajibu ila sisi tumejibu hizo hoja zake. Mheshimiwa anamwambia hilo pingamizi lako halina msingi wowote. Tutaangalia kwenye mwenenedo tulionao hapa.Ni wasilisho letu kuwa kitu pekee kwa leo kinapaswa kupuuzwa ni hoja za Job Mrema, Wakili wa Serikali kwasababu hoja zetu ni za msingi na mahakama inapaswa kujilinda na kulinda hadhi yake na mahakama iwe na wivu huo. Mrema anasema Kibatala anaitisha mahakama kwenye maneno yake hayo kwahiyo yasiwe kwenye mwenendo.

Kibatala amemjibu kuwa Mrema hayamuhusu kabisa na lingekuwa ni kosa mahakama ingesema sio yeye. Kwa kifupi Kibatala anasema Mrema aache kiherehere. Anaingia Mtobesya sasa.Kuhusu Jurisdiction ya mahakama kuendelea kwa mtandao naomba kusema kwamba proceedings za mahakama ni mali ya mahakama. Ukisema nyaraka itumwe au ikasainiwe huko mitaani. Sasa hiyo ni kinyume kabisa ni misingi ya kisheria.

Mahakama inao wajibu wa kulinda haki za mshitakiwa hadi siku anahukumiwa na kesi yake kumalizika. Malalamiko yoyote tunayoleta hayaelei hewani kwasababu hili ndio eneo la msingi kuleta hoja hizo kuhusu haki za Tundu Lissu akiwa huko magereza.

Na mimi naomba kurudia judicial review tunazifahamu vizuri kwahiyo haiwezi kuondoa mamlaka ya hii mahakama hapa. Mtobesya amemaliza na Dr. Nshala kiongozi wa japo amechukua nafasi baada ya Mpale Mpoki kutoka kidogo anaomba kuwa mahakama izingatie maombi ya upande wa utetezi.

Muda huu hakimu anaandika hapo. Tusubiri kama atasoma uamuzi mdogo leo au atatoa tarehe ya kusoma huo uamuzi. Hakimu anasema kwamba mara baada ya kusikiliza hoja za pande zote, na kwa vile mapingamizi yamekuwa marefu na mimi napaswa kupata muda tar. 06/05/2025 majira ya saa nne asubuhi. Nitasoma huu uamuzi mdogo.
We zombie usimlinganishe kibaraka anayetaka kuuza nchi yake na stateman. We kwl ni mwehu
 
Kutokana na mambo ya kijinga kama haya, sasa nimegundua ni kwa nini kuna baadhi ya watu huwa wanafurahia sana wasikiapo vifo vya polisi, viongozi wa chama tawala na serikali, nk.

Inakera sana.
Laana nyingi visomo vingi Alibadiri nyingi zitawaandama Polisiccm
 
Moderator JamiiForums naona wakati mna-update huu uzi, mmeingilia comment yangu. Yaaani badala ya ku-update kwenye uzi husika, mme-update kwenye comment yangu ambayo ni comment ya pili(comment ya kwanza ya huu uzi).

Kuanzia aya ya 6 na kuendelea, sio maneno yangu.

Naomba mrekebishe.
Hata hivyo haikuathiri chochote mkuu 'Slip'.
Komenti yako imetisha sana.
 
Aliyesababisha watumie kiingeleza kibovu ni nani kama siyo CCM
Kingereza cha utetezi siyo kibovu bali ccm hawajui kingereza vizuri hivyo kuona kila jambo linalokataa ushetani wao halipo sawa
 
Huu Uzi ni WA kusoma ukiwa huna stress na unakunywa juice.
 
Kupitia uonevu kwa chadema ndipo Polisiccm wanavuna posho nyingi toka ccm kwa ajili ya kuwambikia kesi za uhaini na pia kuwapiga sana kuwateka kuwafanyia kila vitengo haramu vya kishetani
 
Hakuna mabaya yasiyo na mwisho ilikuwepo KANU ya kenya pia Zambia Ghana Senegal misri vyama vikongwe vilikufa kwa sababu ya kukumbatia Udikiteta kama ccm na Polisiccm wake
 
Sahihi
Hii kesi wameihamisha kutoka kuwa ya watanzania kuwa ya watu wa nje
CHADEMA akili hawana.Eti wanataka watu wa nje wasikie

Waandishi wa habari wa nagezeti na TV zinazotumia kiswahili msiripoti hiyo kesi waachieni hivyo vyombo vyao vya habari vya nje ndio watangaze

Msigeule kuwa wakalimani wao .Wawalipe wakitaka ili mfanye hiyo kazi ya kukalimani walichoongea
Your wish is a vain
 
chadema wamegeuzwa billboard ya matangazo, kila wakili akitaka kujulikana anakimbilia kesi ya chadema, hadi sasa kesi ya msingi haijaanza kusikilizwa ni danadana za mawakili wanabadilishana technicalities.

yaani itafika october jamaa bado yuko ndani na urais ndo hatagombea tena
 
Back
Top Bottom