Kilichomkuta rafiki yangu kazini kwake

Kilichomkuta rafiki yangu kazini kwake

kante mp2025

JF-Expert Member
Joined
Nov 11, 2022
Posts
631
Reaction score
1,192
Rafiki yangu mmoja kanipa kisa chake kaomba nimshauri nimemwambia anipe muda nikakumbuka wazee wa busara wako hapa nitashare kisa chake ili nipate hoja imara za kumshauri.

Rafiki yangu huyu anafanya kazi katika kampuni Z. Juzi akiwa kazini kwake ambako wanaingia saa moja asubuhi na kutoka saa moja na nusu jioni. Akiwa na kompyuta ya kazini kwao aliona tangazo la kazi sehemu basi bhana akataka kutuma maombi ya kazi maana aliona huko wanamaslahi bora kuliko alipo.

Akiwa katika harakati za kuandika barua ya kuomba kazi kampuni B, mwajiri wake wa kampuni Z si akamfuma akamwambia tu naona unafanya ma application ya kazi, jamaa kwa hofu na mshtuko akakaa kimya😁

Sasa jamaa yangu huyu hana raha tena maana mwajiri wake wa kampuni Z anaonekana kummind sana sasa hivi hata akimsalimia hajibiwi, kiufupi jamaa yangu kaonekana kama msaliti anasema boss wake hamchangamkii tena kama mwanzoni hapa anauliza aache kazi ama afanyaje.

Napokea mawazo wakuu ili nikampe namna ya kushinda hiyo pressure😁
 
Amwambie alikuwa anajaribu kutengeneza barua ya kikazi kumsaidia mdoko wake,sababu yeye tayari yuko ok na kazi yake ya sasa hahitaji kuzunguka juani Tena,lakini kazi yake anaipenda na hayuko tayari kuipoteza,kama aliona jina unasema angefuta baadae na kuandika jina la mdogo wake na kufuta sifa zake na kuweka za mdogo wake ambae amezituma kwa email hazijamfikia
 
Kwa hiyo ameshaogopa bosi wake alivyoona anachokifanya?Vema.Amwambie bosi amuongeze maokoto ili asiondoke.Msisitize kwamba,hajaja duniani kumfurahisha bosi wake huku yeye anaishi kwa sonona.Muda haumsubiri yeye ili aonewe huruma na dunia hii ya majahili.
 
Rafiki yangu mmoja kanipa kisa chake kaomba nimshauri nimemwambia anipe muda nikakumbuka wazee wa busara wako hapa nitashare kisa chake ili nipate hoja imara za kumshauri...
Atulie aendelee na kazi hivyo hivyo.Anakubalika kwa boss ndio maana bosi kayumba baada ya kugundua mwana anatafuta ajira.Aendelee kufanya kazi mpaka wakati sahihi utakapofika.

Tena itakuwa rahisi kuomba ruhusa siku ya usaili maana bosi tyr anaijua ishu.Ikifika wakati huo bosi akimwambia ukiendabusirudi basi asirudi.Ila pia kuanzia sasa awe makini afanye kazi kwa uadilifu ajiepushe na vitu vitakavyompa sababu ya kufurushwa ghafla.

Aendelee kutoa salamu ni suala la muda tu salamu itaendelea kuitikiwa.
 
Amwambie aliekuwa anajaribu kutenegeza barua ya kikazi kumsaidia mdoko wake,sababu yeye tayari yuko ok na kazi yake ya sasa hahitaji kuzunguka juani Tena,lakini kazi yake anaipenda na hayuko tayari kuipoteza,kama aliona jina unasema angefuta baadae na kuandika jina la mdogo wake na kufuta sifa zake na kuweka za mdogo wake ambae amezituma kwa email hazijamfikia
Huu ni uongo wa muda mfupi. Isitoshe dogo alipoulizwa alikaa kimya hivyo bosi aka conclude.
 
Mwanaume anatikiswa na kajambo kadogo hivyo!!!
Amevunja katiba ya nchi?
Amevunja kanuni za mkataba wake wa kazi?
Kama aliijiriwa bila mkataba sawa lakini kama ana mkataba anaogopa nini?
Mimi nimeandika barua za kuomba uhamisho mara kadhaa na nampelekea bosi asaini. Nikikosa maisha yanasonga, akikataa kusaini napiga Saini napiga muhuri maisha yanasonga
 
Kwa hiyo ameshaogopa bosi wake alivyoona anachokifanya?Vema.Amwambie bosi amuongeze maokoto ili asiondoke.Msisitize kwamba,hajaja duniani kumfurahisha bosi wake huku yeye anaishi kwa sonona.Muda haumsubiri yeye ili aonewe huruma na dunia hii ya majahili.
😂Huu ushauri wa kimamlaka sana shida ni alikuwa anatuma maombi kwa kompyuta ya ofisi
 
Mwanaume anatikiswa na kajambo kadogo hivyo!!!
Amevunja katiba ya nchi?
Amevunja kanuni za mkataba wake wa kazi?
Kama aliijiriwa bila mkataba sawa lakini kama ana mkataba anaogopa nini?
Mimi nimeandika barua za kuomba uhamisho mara kadhaa na nampelekea bosi asaini. Nikikosa maisha yanasonga, akikataa kusaini napiga Saini napiga muhuri maisha yanasonga
Huu ushauri wako nitampa ausome hope utampa sana nguvu
 
Back
Top Bottom