Kilichomkuta rafiki yangu kazini kwake

Kilichomkuta rafiki yangu kazini kwake

Angemjibu tu eee bwana mkubwa, haya maisha usipende kuwa mtumwa wa mtu kwa miaka mingi anagalia maslah
 
Rafiki yangu mmoja kanipa kisa chake kaomba nimshauri nimemwambia anipe muda nikakumbuka wazee wa busara wako hapa nitashare kisa chake ili nipate hoja imara za kumshauri.

Rafiki yangu huyu anafanya kazi katika kampuni Z. Juzi akiwa kazini kwake ambako wanaingia saa moja asubuhi na kutoka saa moja na nusu jioni. Akiwa na kompyuta ya kazini kwao aliona tangazo la kazi sehemu basi bhana akataka kutuma maombi ya kazi maana aliona huko wanamaslahi bora kuliko alipo.

Akiwa katika harakati za kuandika barua ya kuomba kazi kampuni B, mwajiri wake wa kampuni Z si akamfuma akamwambia tu naona unafanya ma application ya kazi, jamaa kwa hofu na mshtuko akakaa kimya😁

Sasa jamaa yangu huyu hana raha tena maana mwajiri wake wa kampuni Z anaonekana kummind sana sasa hivi hata akimsalimia hajibiwi, kiufupi jamaa yangu kaonekana kama msaliti anasema boss wake hamchangamkii tena kama mwanzoni hapa anauliza aache kazi ama afanyaje.

Napokea mawazo wakuu ili nikampe namna ya kushinda hiyo pressure😁
Mwambie amwambie bosi wake na yeye pia akuze ufahamu wao wakufikiri
 
Hakuna boss ambaye haelewi kuhusu green pastures if is real boss .

Kuhusu boss kutomchangamikia hiyo ni temporary situation ambayo itaondoka yenyewe .


Mwambie azingtie kufanya Kazi Kama zamani

Asijenge hofu - maana hofu inaua na kukufanya uishi kinyonge


Mwisho mwambie azingatie

Kujutuma kazini
Uaminifu
Kuwa positive
Hawa mabosi wa kiswahili hawana tofauti na wanasiasa, hawajawahi kuwa serious ktk majukumu na proffesionalism, zaidi wanapenda kulambwa miguu.
 
Hiyo sio kazi hiyo ni mishe mishe,kufanya kazi kwa wahindi unaita kazi,reputable organisation hawanaga hayo
Tatizo za ajira zisizokuwa rasmi na ambazo hazina mikataba, hapo bila kulamba viatu vya boss atalala njaa.
 
Boss samahani kuna kitu hapa ofisini hakipo sawa, wafanyakazi wengine wanashindwa tu kusema na ni muda mrefu sasa.... Ila naona kuacha kazi sio solution kuomba kazi kwingine sio solution, nimewaza Sana nikaona bora nikushirikishe huwenda unaweza fanya kitu!!!

Starting point tayari👆👆

Kamwe kwenye maelezo yake asiseme shida ni maslah maana hcho ndicho boss anachotegemea utamwambia,
Badala yake mpe sababu nyingine ambayo ni ya kiutendaji au management

Pia unaweza gusa swala la muda mnaoingia na kutoka n.k
(Note: hapa n unajitetea kwahyo hakikisha boss anatoa hii kauli
👉 Kumbe shida ndo hiyo, kwanini hukusema??
 
Huyo jamaa anaonekana ni wale wakung'ata na kupuliza, mwambie atimize wajibu wake na kilichompeleka hapo ni kazi na siyo tabasamu / kuchangamkiwa na bosi.
 
Back
Top Bottom