Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Dah...hili ni somo jingine tena...hasa kwa wale wote wasiotaka kuelewa nguvu ya aliyempiga Goliath...[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Haaaa.....hii kweli kabisaTanzania hatupendi kuambiwa ukweli ila unanifiki tu.
Mahaba na kutokujitambua vinamsumbua huyo JamaaTupe ushahidi kama kweli aliwahi airport?
Wapi pasipo na mapungufu kwa 100% kama siyo kukurupuka kwako hapa we naye?ATCL ni jipu kubwa mashirika mengi ya serikali utendaji wao huwa ni zero na sasa washindani fast jet wanaongoza ndo tutegemee madudu ya kutosha humo
Umeona sasa !! ... walio sema pata pesa tuijue Tabia yako hawakukosea
Mbona amekuambia, kwamba katika watu aliofika nao wakati mmoja airport kuna waliochukuliwa, pale walipoambiwa tuna nafasi za watu wawili tu kwenye kundi lenu?
Kukiwa na overbooking mnaweza mkawa watano mmefika wakati mmoja akaondoka mmoja tu kati yenu
Kwani ile nyimbo ya nyegezi haiwezi kuwa kigezo ashikishwe adabu?Sio kumfungia Ila according to mleta mada anadai chanzo kilichosababisha diamond kufungiwa ni issue yake ya usafiri wa ndege, so basata wakatumia huo uchochoro kumnyoosha
Ubabeshow inaendelea mbele, mwisho wake ni uchungu mzito kwa watawala.
ATCL haitafika popote zaidi ya kufa tena maana wanalazimisha tuamini uongo wao badala ya kujirekebisha kwa kosa walilomfanyia Diamond,
tatizo kubwa na chanzo cha maamuzi ya kibabe ni JIWE.
Duuu kumbe diyamondi bado hajafanikiwa
Baraza la Sanaa la Taifa (Basata) limetangaza kumfungia msanii Diamond Platnumz na mwenzake Rayvanny kufanya maonesho yoyote ndani au nje ya nchi kwa muda usiofahamika. Si hivyo tu, bali pia wamelifutilia mbali Tamasha la Wasafi Festival ambalo limekuwa gumzo kubwa katika siku za hivi karibuni.
Sababu zinazotolewa na Basata, ambazo zina ushahidi wa wazi, ni kwamba msanii huyo amekiuka maelekezo aliyopewa na Basata, ya kuacha kuperform wimbo wa Nyegezi (Mwanza) uliofungiwa na Basata kwa kile kilichoelezwa kwamba ni kukiuka maadili ya Kitanzania.
Tukio la Diamond kupigwa pini na Basata, limekuja muda mfupi baada ya Mbongo Fleva huyo kusababisha hali ya sintofahamu katika Uwanja wa Ndege wa Mwanza baada ya video kusambaa kwenye mitandao ya kijamii, ikimuonesha 'bwa mdogo' huyo akiwatemea mbovu wafanyakazi wa uwanja huo, kwa kile alichodai kwamba wamemchezea rafu kwa kuuza tiketi alizozifanyia booking mapema na kusababisha ashindwe kusafiri kurejea Dar baada ya kumalizika kwa shoo yake jijini Mwanza.
Madai hayo yalililazimu shirika la ndege la ATCL kutoa tamko rasmi na kukanusha madai ya Diamond ambapo taarifa ilieleza kwamba hakuna aliyeuza tiketi yake isipokuwa yeye ndiye aliyefanya makosa kwa kuchelewa kufika uwanja wa ndege hivyo kwa mujibu wa kanuni na taratibu, alipoteza sifa za kusafiri na ndege hiyo hivyo kuomba kupangiwa siku iliyofuatia.
Kabla ya ATCL kutoa ufafanuzi huo, watu wengi waliotazama video hiyo, waliamini kwamba kweli ATCL wamefanya uzembe, wamepiga dili kwa kuuza tiketi ya Diamond na kundi lake kwa watu wengine, kwa lugha nyepesi Diamond aliwaaminisha watu kwamba ATCL si waaminifu kwa wateja wake na ndiyo maana wameuza tiketi ambazo zilishafanyiwa booking kwa watu wengine.
Ikumbukwe kwamba ATCL ni shirika la serikali na serikali ya awamu ya tano imewekeza nguvu kubwa kulihuisha shirika hilo lililokuwa mahututi kwa kununua ndege mpya na kulifanya sasa angalau liwe na uhai baada ya kudoda kwa muda miaka mingi. Tayari ndege tano zimeshafika nchini na zinafanya kazi na matarajio ni kuleta mashine kubwa zaidi, Airbus mapema mwezi huu.
Wakati serikali ikihangaika kuhakikisha ATCL inapata wateja wa uhakika na kujiendesha kwa faida, anatokea 'mwehu' mmoja na kuibua tuhuma ambazo zinawafanya wateja wapoteze imani na shirika hilo na hivyo kulikosesha wateja na mapato.
Diamond ambaye kwa heshima na taadhima, alialikwa wakati moja kati ya ndege hizo ikiwasili nchini, badala ya kuwa balozi wa kuwahimiza watu wengine watumie huduma za ATCL, yeye anahujumu kwa kuibua tuhuma za uongo zenye lengo la kuikosesha ATCL wateja na mapato.
Fyekelea mbali ili siku nyingine ajifunze kuwa na adabu na uzalendo! Siku zote serikali inaweza kuwa inajua kwamba unafanya makosa lakini kwa sababu hugusi maslahi yake, ikakuacha uendelee kukosea! Ndiyo, kwani Diamond ameanza kuidharau Basata leo kwa kuimba Nyegezi? Upo ushahidi wa mpaka video akiwa Zanzibar na kwingineko, alionekana akiwaimbisha mashabiki kijanja.
Kama ishu ingekuwa ni hiyo tu, Basata wangeweza kuweka pamba masikioni au kuitana kishkaji, Mngereza alikuwepo kwenye uzinduzi kule Mtwara, kwa hiyo kwao siyo adui tena bali mlezi, wangeweza kunena kwa lugha moja wakayamaliza ili kuepusha hasara ya mamilioni ambayo sasa ataipata kwa kufungiwa.
Diamond, man up! Don't mess with the government!
Nilivyoona ile video, halafu ATCL wakakanusha madai yake nilijua kuna kitu kitafata, Diamond ambacho hajui ni kwamba kazi yake anaifanya kwenye nchi ambayo anahitaji cover kubwa sana na kuinyenyekea serikali.
Sasa kufanya kile alichofanya na wao wakiamua wammalize ni rahisi, watakuja na issue za vibali, ulinzi, kodi, nk.
Anatakiwa kuujua msemo wa "ukila na kipofu usimshike mkono".
Kwahiyo Basata ni chombo cha kukomoa wasanii pale maslahi ya serikali yanapoguswa? Anyway, yule mama aliyeruhusiwa kupita si na yeye alikuwa amechelewa? Kwanini aliruhusiwa?
Diamond alishapandwa na kiburi sababu alikariri kila siku ni Jumamosi kama vile alivyokuwa kashazoeshwa kwenda ikulu kupiga stories na Muheshimiwa Mstaafu.Diamond akumbuke serikali ya jiwe na watumishi wake ni watu wa visasi
Tatizo kubwa ni kwamba wengi mnaochangia hapa kama wewe mnachangia kama wasafiri wa labda mabasi au wasafiri wa humu humu nchini.
Jiulize; Hivi wajua kuwa safari za ndege huhusiana kote ulimwenguni?? Kwa vipi? Kama nina safari kutoka Mza kwenda Jberg, naweza fanya booking yangu nikasafiri bila kulala Dar na nikaenda kulala home Jberg siku hiyo hiyo??
Sasa ndio maana unaambiwa, Fika even 2 hrs before departure time. Hii inakusaidia na pia inawasaidia wasafirishaji wanaokusafirisha kurekebisha mambo kama kweli walizidiwa na abiria.
Kivipi; Wakiona kuna msongamano au wamezidiwa wanafanya mpango kukodi ndege nyingine iliyopo jirani ili kukuwahisha dar chini ya nusu saa 7a muda uliokuwa umepangiwa kuingia. Unafika unaendelea na safari yako in time.
Mnaposema Mondi kaonewa, hakufanyiwa haki, Je, kuchelewa kwake ati nusu saa kabla ya departure time ndio kuiharibie sifa ATCL kwa sababu ya "Ujuha wake?"
Next time, akodi bus au ndege yake binafsi