Tetesi: Kilichomponza Diamond ni Sakata la ATCL

Ww unaonekana ni nyampala mpuuzi labda kwakuwa ma vyeo yamekuwa ya kujichotea lkn pia szani ni kama umechelewa
 
Ndio maana ukifuatilia hili sakata hawakutaja muda kamili ambao Diamond alifika uwanjani...
Btw wanatetea matumbo yao tu...
Air Tanzania hawana haja ya kutaja muda ambapo mteja amefika airport. Inaeleweka reporting time kwenye check in counter. Sasa kama umekuja mapema na ukaanza kuongea na marafiki zako wakati wenzako waliokuja nyuma yako wana check in halafu wewe unapokuta desk limefungwa na makosa yako.
Kilichotakiwa kufanywa na huyo kijana, ni kufanya booking kwa siku nyingine na awahi airport ku-check kwa wakati. TUACHE SIASA ZA KITOTO
 
Nyie ndio mnafanya hizi taasisi za kiserikali zi zidi kuwa hovyo, hivi Jerry Muro alivyowa rekodi wale trafiki wakichukua rushwa ina maana alilidhalilisha jeshi la polisi?

Mimi 2015 baba yangu mdogo alikufa Muhimbili, kilitakiwa kibali cha damu mimi ndiye niliyekishughulikia na nikakipata, nikakipeleka pale kabla ya saa mbili nikaelekea kazini , wakaniambia watamwekea damu, saa sita mama yangu mdogo anafika anawauliza manesi vipi mgonjwa wangu kishawekewa damu, wanamwambia damu zimeisha wakati mimi waliniambia zipo, alfajiri ba mdogo kafa damu hajawekewa na kibali cha damu sijarudishiwa, sasa hawa watendaji ningewarekodi ningekuwa nafanya makosa?

Acheni kulea uzembe na wale manesi washukuru wazo la kuchukua video nilikuwa sina la sivyo nao wangekuwa tayari wapo mitandaoni.
 
tatizo shule hivyo uwezo wa kuona mbali haupo yeye anaona mwisho clouds wala hawezi kuona kuwa ATCL inaweza kuwa fursa ya kumpandisha chart siku zijazo. hivyo wale wanaowaalika wasanii inapaswa wawaambie kwao inaweza kuwa na manufaa gani si swala la wao kuuza sura tu.
 
Foolish fool!!!!You are too emotional!!!Kutokupenda matatizo ya serikali yajulikane!!!!Ulichoandika ni ujuha mtupu
 
Tafadhali fafanua hilo neno 'umama' ili utuonyeshe tofauti yako na Domo au ATCL.
 
Tafadhali fafanua hilo neno 'umama' ili utuonyeshe tofauti yako na Domo au ATCL.

Nimeitumia figuratively na sio its literal meaning!

Uende shule usome na uelimike sio unakula kodi zetu tu for nothing!
 
Acha undezi (nimeitumia figuratively). Ainisha sifa za umama na uzihusianishe na mada. Nataka kujua akina mama wakoje mpaka wafananishwe na hii mada.

Nandera,ni Mpare supposedly,mtani wangu if that make sense......

I think you want to dance,go ahead play yourself!
 
Yaani watu wanaongea mengi utadhani walikuwepo uwanjani.Sababu nyingi zitatafutwa kuhalalisha kiburi cha aliyechelewa kuwahi uwanjani.Tuache ubashiri usio na tija,kijana amekosea sana kuanika kwenye mitandao kisa cha yeye kutokusafiri kama alivyopanga safari yake.Hapa mtawalaumu ATCL bure kumbe mwenye kosa ni aliyechelewa ku-check in.Unakuja uwanjani,hu-check in,unapiga stori za kisharobaro na ubishoo halafu muda umepita unajifanya umeonewa.

Hakuna shinikizo lolote toka juu.BASATA wametimiza wajibu wao kwani ni mara nyingi wimbo huo umelalamikiwa,pia ulikuwa na katazo lakini mhusika hakutii.Sasa tunalaumu mamlaka kufanya kazi yake?

Kutoa video za aina hiyo na kulipotezea shirika uaminifu mbele ya jamii ni kutokujielewa hata kidogo wakati Serikali inapambana usiku na mchana kulipatia taifa identity mbele ya mataifa mengine.

Tuwe tunawaza nje ya box mara nyingine,badala ya ku-connect dot kuwa ameonewa na kupigwa marufuku ya ku-perfom.Kiburi/dharau/kuota mapembe haisaidii,tii sheria bila shuruti!!!Hakuna shinikizo lolote toka kokote@Abunwasi your right!!!!
 
Sijakuelewa
Umesoma uzi wangu vizuri? au ndiyo upotoshaji?
 


Diamond ni kioo cha jamii kwa wanayemfuatilia tu, yaani mimi nishindwe kupanda ndege kwa raha yangu kisa eti Diamond ana ugomvi na ATCL, to hell....sina ujinga huo hata siku moja. Only mazuzu ndiyo wanaweza fanya hivyo.
 
Kwenye Show za Mtwara,Iringa,Morogoro,Sumbawanga Wimbo wa Nyegezi haukuimbwa? Kama uliimbwa imekuaje wamechelewa kuwafungia.Halafu Mie nlidhani umefunguliwa,maana Mtaani Nyegezi unapigwa kama kawa
Huko kote haukuimbwa kabisa...
 
Yeah.....kama nawaona TRA nao wakimnyemelea!

Ni hatari kuwa sahihi vs serikali.
 
Acha kuingiza hisia na mapenzi katika mambo yanayohitaji taaluma zaidi.Unafikiri hao wasemaji wa ATCL walikuwa hawajui kama wakizungumza uongo kuwa watajulikana? Nchi hii kubwa mkuu.Acha ujuaji na ushamba wa kishabiki
 
Hivi kweli wewe ulitegemea ATCL waseme sorry? sijui wewe umesafiri na ATCL lini mara ya mwisho na mara ngapi au unapeperusha ngonjera hapa?.
Yaani tukio la Diamond limenikumbusha sana kauli ya JK kwamba Rais kafanya jambo zuri kuiimarisha ATCL lakini wasiwasi wake ni upande wa MANAGEMENT, yaani pale customer care ni sifuri; ukilinganisha na reception ya Precision, ATCL Mbaaado sana! Kasumba ya shirika la umma, haitawaacha salama hata kama Rais atawapa ndege nyingine 20! WABADILIKE!, vinginevyo ATCL itakuwa Mtoto NJITI
 
Mkuu mimi sijawahi kupanda ndege, hapa nachangamsha kijiwe tu, vipi nasikia ukipanda ndege huko juu panatisha sana ni kweli? Use your head.
 
Acha kuingiza hisia na mapenzi katika mambo yanayohitaji taaluma zaidi.Unafikiri hao wasemaji wa ATCL walikuwa hawajui kama wakizungumza uongo kuwa watajulikana? Nchi hii kubwa mkuu.Acha ujuaji na ushamba wa kishabiki
Hilo suala lilichunguzwa na team ilitumwa haraka mpaka pale, bahati nzuri CCTV huwa hazidanganyi kwenye suala zima la muda, utachezea kote lakini huwezi kubadilisha footage imechukuliwa muda gani, ukweli ukabainika
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…