Kilichomponza mhadhiri ‘gaidi’ wa UDOM ni hiki hapa

tpaul

Platinum Member
Joined
Feb 3, 2008
Posts
27,843
Reaction score
29,350
Habari za chinichini zinapenya kutoka viunga vya UDOM na mitandao ya kijamii kwamba kitu kilichomponza mhadhiri wa UDOM, Dr Kaijage, na kujikuta akipewa kesi ya ugaidi, ni ujasiri wake wa kusimamia taaluma kiuweledi bila kumuogopa mtu yeyote. Habari kamili zinadai wakati mhadhiri huyo akiendelea kufundisha somo la Political Science, mada ya Types of Governments alitoa mfano wa nchi zilizoungana na kutengeneza Union Government, huku akiiondoa Tanzania kwenye orodha ya nchi hizo.

Wahadhiri siku zote ni watu wa facts and evidence. Hawapendi blaablaa! Katika kuthibitisha ukweli wa mambo wanayofundisha, hupenda kufanya citations kutoka kwenye vyanzo mbalimbali. Kwa hiyo, ili kukomelea hoja yake kwamba Tanzania is not a union government, Dr Kaijage alinukuu definition kutoka kwenye kitabu cha Civics cha O-level kama citation hiyo ilivyokuwa highlighted hapo chini (wataalamu mtatusaidia kutambua hiki ni kitabu cha kidato cha ngapi):

1786827019718.png

Kwa mujibu wa definition ya Union Government, kama ilivyoainishwa hapo juu, Dr Kaijage aliwaambia wanafunzi kwamba Tanzania haimo kwenye orodha hiyo kwa sababu Zanzibar haijapoteza madaraka yake. Yaani, kuna serikali inayoitwa ya Muungano (Union) na pia kuna serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, ambayo ina mamlaka yake kama nchi ndani ya muungano. Hivyo, aliwaambia wanafunzi kwamba kitabu hiki kilichoandikwa na kuhakikiwa na serikali, kinafundisha uwongo kwa kuwa Tanzania haikidhi vigezo vya kuitwa nchi ya Muungano.

Kana kwamba hilo halitoshi, Dr Kaijage alihamia kwenye kipengele kingine cha Democracy. Katika kipengele hicho alitoa mifano ya serikali ambazo aliziita za kidikteta, na kuitolea mfano Tanzania kama mojawapo ya nchi za kidikteta, hasa kufuatia sintofahamu kwenye chaguzi za 2009, 2020 na 2025. Aidha, alitumia kitabu kimojawapo cha O-level kutoa tafsiri hiyo kama inavyosomeka kwenye kipande kifuatacho:
1786827228217.png

Kama inavyoonekana, mhadhiri huyo ali-highlight vipande kwenye mafundisho yake ambavyo viliashiria kwamba Tanzania inaendeshwa kwa misingi ya kidikteta na uvunjivu mkubwa wa haki za binadamu.

Nini kilijiri?
Wakati akiendelea kufundisha, hakujua kuwa alikuwa anarekodiwa na mwanafunzi (chawa) mmoja ndani ya darasa lake. Baada ya kukamilisha kazi ya kurekodi, mwanafunzi huyo alituma video kwa wakubwa zake kwa ajili ya utekelezaji.

MAONI YANGU
Kitendo cha kumkamata Dr Kaijage na kumkandika kesi ya ugaidi, kitasababisha wahadhiri wengine waogope kufundisha kiuledi na badala yake kufundisha uongo ili tu kuifurahisha serikali. Hata kama mifano aliyotoa haiwafurahishi serikali, sio busara kumpa kesi mbaya kiasi hiki. Kibaya zaidi, inasemekana familia ya Kaijage imekatiwa huduma za maji na umeme na kupelekea familia hiyo kuishi kwa taabu na shida. Hii sio sawa.

Nawasilisha.
​
 
Attachments

  • 1786825254019.png
    1786825254019.png
    116.7 KB · Views: 23
Me nikiwa nakutana na habari hizi naumia ila sina cho chote chakufanya, Mungu awasaidie
Vya kufanya unavyo vingi tuu.

Kwanza nikuulize, Mungu awasaidie nani!?

Unaweza kufanya vifuatavyo;
1. Kupiga goti na kumuomba Mungu wako afanye jambo kuondoa hali hii.
2. Kukemea/kupaza sauti hata kimaandishi kama tufanyavyo humu ndani JF.
3. Kuwaambia ndugu, jamaa au marafiki (unaowaweza) ambao wapo upande wa watesi jinsi unavyochukizwa na maovu yafanywayo na huo upande.
4. Kuwaombea wale wote wanaopambana na mfumo huo ovu.
5. Kuchangia Tone Tone ili harakati za kuuondoa huu mfumo ovu zifanyike kwa effectiveness kubwa.
 
Kwa mujibu wa definition ya Union Government, kama ilivyoainishwa hapo juu, Dr Kaijage aliwaambia wanafunzi kwamba Tanzania haimo kwenye orodha hiyo kwa sababu Zanzibar haijapoteza madaraka yake. Yaani, kuna serikali inayoitwa ya Muungano (Union) na pia kuna serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, ambayo ina mamlaka yake kama nchi ndani ya muungano. Hivyo, aliwaambia wanafunzi kwamba kitabu hiki kilichoandikwa na kuhakikiwa na serikali, kinafundisha uwongo kwa kuwa Tanzania haikidhi vigezo vya kuitwa nchi ya Muungano.
Nawasilisha.
​
Kwa kawaida binadamu anapokuwa kwenye matatizo na kwenye magumu, watu wenye roho za ubinaadamu, na utu, wanaumizwa na anayopitia, lakini watu wenye roho za kishetani, wanazidi kuchochea moto!, bandiko hili ni adding an insult to an injury!, kuna watu, mnajichumia laana bila kujijua kwa kumsingizia uongo kama, huu uliouleta hapa ili aonekane ni lecture kilaza!,

Kuna aina kuu tatu za miungano ya nchi,
  1. Muungano wa Union na kuunda a unitary gornment kwa kuunda union, nchi mbili au zaidi zinaungana kwa union na kuunda nchi noja. Hizi nchi zote zinapoteza its sovereignty na nchi mpya ya union. Kama GBRT.
  2. Muungano wa Federation, nchi moja au zaidi zinaungana kwenye baadhi tuu ya mambo, kunakuwa na federal government, lakini kila states inakuwa na utawala wake wa mambo yake ya ndani, kama US.
  3. Muungano wa Confederation, kama Ujerumani,
Muungano wa Tanzania na Zanzibar, ni muungano adhimu na adimu.
Kimataifa ni muungano wetu ni muungano wa Union, nchi mbili za Tanganyika na Zanzibar zimeungana kwa union, kuunda nchi moja ya JMT, nchi zote mbili zimepoteza sovereignty zake na JMT ndio the new sovereign.

Lakini ndani ya muungano, JMT ni moja ya JMT yenye muungano wa federation ya nchi mbili, nchi mama ya JMT, na nchi mtoto ya Zanzibar yenye utawala wake wa ndani, lakini hauna sovereignty. Kimaifa Tanzania ni nchi moja tuu, Zanzibar sio nchi, ni sehemu ya Tanzania yenye utawala wake wa ndani kama ilivyo Kwazulu Natal kwa Chief Mangosotho Buthelezi,

Kitendo cha kumsingizia uongo mtu aliyeko matatzoni ni kujichumia laana za bure bila wewe kujijua!.

P.
 
MAONI YANGU
Kitendo cha kumkamata Dr Kaijage na kumkandika kesi ya ugaidi, kitasababisha wahadhiri wengine waogope kufundisha kiuledi na badala yake kufundisha uongo ili tu kuifurahisha serikali. Hata kama mifano aliyotoa haiwafurahishi serikali, sio busara kumpa kesi mbaya kiasi hiki. Kibaya zaidi, inasemekana familia ya Kaijage imekatiwa huduma za maji na umeme na kupelekea familia hiyo kuishi kwa taabu na shida. Hii sio sawa.

Nawasilisha.
​
Umehitimisha kinyonge sana, kiTanganyika!

Tatizo la WaTanganyika lipo kwenye kuiamini mifumo ile ile inayoratibu udhalimu dhidi yao ndiyo iwaonee huruma na kuwatendea HAKI!

Kwamba mtesi yule yule mnufaika ndiye anaombwa awe Malaika wa nuru kubadilisha ama kuondosha madhila yanayomnufaisha!

Tukifanikiwa kubadilisha mitazamo hiyo na kuthamini uwezo wa WaTanganyika tutafika mbali. Untill then.

NB: Natamani Tundu Lissu aombe kuunganishwa kwenye hiyo keshi ya Ugaidi dhidi ya Dr. Kaijage.
 
Kama alisema kuna Tanzania haina Union Government anapotosha

Zanzibar haina total sovereignty.

Mamlaka yake ni kwa mambo ya ndani tu ila inapokuja kwa maswala ya nje yanayoliwasilisha Taifa yale mambo yanayotambulisha Taifa yamebakia kwa serikali ya JMT.
 
Habari za chinichini zinapenya kutoka viunga vya UDOM na mitandao ya kijamii kwamba kitu kilichomponza mhadhiri wa UDOM, Dr Kaijage, na kujikuta akipewa kesi ya ugaidi, ni ujasiri wake wa kusimamia taaluma kiuweledi bila kumuogopa mtu yeyote. Habari kamili zinadai wakati mhadhiri huyo akiendelea kufundisha somo la Political Science, mada ya Types of Governments alitoa mfano wa nchi zilizoungana na kutengeneza Union Government, huku akiiondoa Tanzania kwenye orodha ya nchi hizo.

Wahadhiri siku zote ni watu wa facts and evidence. Hawapendi blaablaa! Katika kuthibitisha ukweli wa mambo wanayofundisha, hupenda kufanya citations kutoka kwenye vyanzo mbalimbali. Kwa hiyo, ili kukomelea hoja yake kwamba Tanzania is not a union government, Dr Kaijage alinukuu definition kutoka kwenye kitabu cha Civics cha O-level kama citation hiyo ilivyokuwa highlighted hapo chini (wataalamu mtatusaidia kutambua hiki ni kitabu cha kidato cha ngapi):

View attachment 3651108
Kwa mujibu wa definition ya Union Government, kama ilivyoainishwa hapo juu, Dr Kaijage aliwaambia wanafunzi kwamba Tanzania haimo kwenye orodha hiyo kwa sababu Zanzibar haijapoteza madaraka yake. Yaani, kuna serikali inayoitwa ya Muungano (Union) na pia kuna serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, ambayo ina mamlaka yake kama nchi ndani ya muungano. Hivyo, aliwaambia wanafunzi kwamba kitabu hiki kilichoandikwa na kuhakikiwa na serikali, kinafundisha uwongo kwa kuwa Tanzania haikidhi vigezo vya kuitwa nchi ya Muungano.

Kana kwamba hilo halitoshi, Dr Kaijage alihamia kwenye kipengele kingine cha Democracy. Katika kipengele hicho alitoa mifano ya serikali ambazo aliziita za kidikteta, na kuitolea mfano Tanzania kama mojawapo ya nchi za kidikteta, hasa kufuatia sintofahamu kwenye chaguzi za 2009, 2020 na 2025. Aidha, alitumia kitabu kimojawapo cha O-level kutoa tafsiri hiyo kama inavyosomeka kwenye kipande kifuatacho:
View attachment 3651110
Kama inavyoonekana, mhadhiri huyo ali-highlight vipande kwenye mafundisho yake ambavyo viliashiria kwamba Tanzania inaendeshwa kwa misingi ya kidikteta na uvunjivu mkubwa wa haki za binadamu.

Nini kilijiri?
Wakati akiendelea kufundisha, hakujua kuwa alikuwa anarekodiwa na mwanafunzi (chawa) mmoja ndani ya darasa lake. Baada ya kukamilisha kazi ya kurekodi, mwanafunzi huyo alituma video kwa wakubwa zake kwa ajili ya utekelezaji.

MAONI YANGU
Kitendo cha kumkamata Dr Kaijage na kumkandika kesi ya ugaidi, kitasababisha wahadhiri wengine waogope kufundisha kiuledi na badala yake kufundisha uongo ili tu kuifurahisha serikali. Hata kama mifano aliyotoa haiwafurahishi serikali, sio busara kumpa kesi mbaya kiasi hiki. Kibaya zaidi, inasemekana familia ya Kaijage imekatiwa huduma za maji na umeme na kupelekea familia hiyo kuishi kwa taabu na shida. Hii sio sawa.

Nawasilisha.
​
Pole nyingi kwake na familia yake
 
Kwa hiyo aliweka interpretation zake kwenye vitabu vya watu wasomi wengine
Hujui maana ya kuwa profesa ni kitu gani; halafu unakuja kuuliza swali la kijinga kabisa.

Huyu ni mfano wa profesa mzuri sana kwa haya yaliyoelezwa hapa kama ndiyo kweli.

Wewe inawezekana hata darasa la Chuo Kikuu hujawahi kuingia, au kama uliingia, basi ulikutana na walimu wa high school na siyo maprofesa.
 
Habari za chinichini zinapenya kutoka viunga vya UDOM na mitandao ya kijamii kwamba kitu kilichomponza mhadhiri wa UDOM, Dr Kaijage, na kujikuta akipewa kesi ya ugaidi, ni ujasiri wake wa kusimamia taaluma kiuweledi bila kumuogopa mtu yeyote. Habari kamili zinadai wakati mhadhiri huyo akiendelea kufundisha somo la Political Science, mada ya Types of Governments alitoa mfano wa nchi zilizoungana na kutengeneza Union Government, huku akiiondoa Tanzania kwenye orodha ya nchi hizo.

Wahadhiri siku zote ni watu wa facts and evidence. Hawapendi blaablaa! Katika kuthibitisha ukweli wa mambo wanayofundisha, hupenda kufanya citations kutoka kwenye vyanzo mbalimbali. Kwa hiyo, ili kukomelea hoja yake kwamba Tanzania is not a union government, Dr Kaijage alinukuu definition kutoka kwenye kitabu cha Civics cha O-level kama citation hiyo ilivyokuwa highlighted hapo chini (wataalamu mtatusaidia kutambua hiki ni kitabu cha kidato cha ngapi):

View attachment 3651108
Kwa mujibu wa definition ya Union Government, kama ilivyoainishwa hapo juu, Dr Kaijage aliwaambia wanafunzi kwamba Tanzania haimo kwenye orodha hiyo kwa sababu Zanzibar haijapoteza madaraka yake. Yaani, kuna serikali inayoitwa ya Muungano (Union) na pia kuna serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, ambayo ina mamlaka yake kama nchi ndani ya muungano. Hivyo, aliwaambia wanafunzi kwamba kitabu hiki kilichoandikwa na kuhakikiwa na serikali, kinafundisha uwongo kwa kuwa Tanzania haikidhi vigezo vya kuitwa nchi ya Muungano.

Kana kwamba hilo halitoshi, Dr Kaijage alihamia kwenye kipengele kingine cha Democracy. Katika kipengele hicho alitoa mifano ya serikali ambazo aliziita za kidikteta, na kuitolea mfano Tanzania kama mojawapo ya nchi za kidikteta, hasa kufuatia sintofahamu kwenye chaguzi za 2009, 2020 na 2025. Aidha, alitumia kitabu kimojawapo cha O-level kutoa tafsiri hiyo kama inavyosomeka kwenye kipande kifuatacho:
View attachment 3651110
Kama inavyoonekana, mhadhiri huyo ali-highlight vipande kwenye mafundisho yake ambavyo viliashiria kwamba Tanzania inaendeshwa kwa misingi ya kidikteta na uvunjivu mkubwa wa haki za binadamu.

Nini kilijiri?
Wakati akiendelea kufundisha, hakujua kuwa alikuwa anarekodiwa na mwanafunzi (chawa) mmoja ndani ya darasa lake. Baada ya kukamilisha kazi ya kurekodi, mwanafunzi huyo alituma video kwa wakubwa zake kwa ajili ya utekelezaji.

MAONI YANGU
Kitendo cha kumkamata Dr Kaijage na kumkandika kesi ya ugaidi, kitasababisha wahadhiri wengine waogope kufundisha kiuledi na badala yake kufundisha uongo ili tu kuifurahisha serikali. Hata kama mifano aliyotoa haiwafurahishi serikali, sio busara kumpa kesi mbaya kiasi hiki. Kibaya zaidi, inasemekana familia ya Kaijage imekatiwa huduma za maji na umeme na kupelekea familia hiyo kuishi kwa taabu na shida. Hii sio sawa.

Nawasilisha.
​
Huyu ni profesa mzuri sana.

Ana-stmulate akili za wanafunz watumie uwezo wao wa kufikirii na siyo kuwa-'spoonfeed'

Unamfungulia kesi mtu kama huyu, amabaye anafanya kazi yake vizuri kabisa. Kichwani mwako utakuwa umejaza madudu.
 
Back
Top Bottom