John Haramba
JF-Expert Member
- Feb 4, 2022
- 365
- 1,374
Ofisa Habari wa Ruvu Shooting, Masau Bwire amezungumzia kifo cha mchezaji wao, beki Ally Mtoni 'Sonso' aliyefariki jana akiwa njiani kupelekwa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dar es Salaam.
Imeelezwa kuwa kabla ya kukutwa na umauti huo, Sonso nyota wa zamani wa Lipuli,Yanga, Kagera Sugar na Ruvu Shooting alikuwa akiuguza majeraha ya mguu tangu Oktoba, mwaka jana.
Bwire amesema Sonso beki huyo alipata majeraha mara baada ya mchezo wao wa Ligi Kuu dhidi ya Simba, uliopigwa Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
"Mke wake ndiye alianza kunipigia akitoa kilio, baadaye Baba yake aliniambia hivyo na muda huu naelekea nyumbani kwao kwa taratibu za mazishi hapo kesho Jumamosi sambamba na timu nzima kwa ujumla, hakika tutamkumbuka," amesema Bwire.
Tangu kutangazwa taarifa za msiba huo kumekuwa na idadi kubwa ya wachezaji na klabu mbalimbali zimetumia mitandao yao ya kijamii kuelezea kusikitishwa na msiba huo.
Source: Mwananchi