Kilichomuua Ally Sonso hiki hapa, wachezaji, klabu zamlilia

Kilichomuua Ally Sonso hiki hapa, wachezaji, klabu zamlilia

Hakuna uchawi hapo. Ni kukosa maarifa au kujaa hofu kwa wachezaji wetu. Hilo ni tatizo ambalo linatibika vyema kabisa hospitali.
Inaonekana alishakuwa kwenye ‘Complication stage’ ndo akaenda Muhimbili.

Pia nina shaka na ‘Medical team’ ya Ruvu Shooting. It’s either hawajui ama wanafanya ‘Mazoea’ kwenye afya za wachezaji wao.
Makolo mnalo hilo

Sent from my TECNO LC6 using JamiiForums mobile app
 
Hakuna uchawi hapo. Ni kukosa maarifa au kujaa hofu kwa wachezaji wetu. Hilo ni tatizo ambalo linatibika vyema kabisa hospitali.
Inaonekana alishakuwa kwenye ‘Complication stage’ ndo akaenda Muhimbili.

Pia nina shaka na ‘Medical team’ ya Ruvu Shooting. It’s either hawajui ama wanafanya ‘Mazoea’ kwenye afya za wachezaji wao.
Kwahiyo ni ugonjwa gani huo wa ghafla?.maana alikua safarini na timu sasa sidhani kama angekua mgonjwa muda kidogo nyuma asingeonekana ata wakati wa mazoezi hadi timu iambatane naye kwenda mwanza.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Jamaa anadai kabla ya game ya ruvu vs Simba huko ccm kilumba alihisi maumivu wa mguu akaongea na daktari wao akampa dawa ya kutuliza maumivu ..

Kesho yake pia akaona maumivu yanazidi basi kwenye hiyo game hakupangwa.. lakini akaanza kuona mguu unavimba kama tende akaongea na daktari wao wakampeleka muhimbili kwa matibabu zaidi

Basi baada ya matibabu hapo muhimbili akaomba akatabiwe kwao.. maana taarifa alizo zipata ni kwamba katupiwa jini

Basi mguu ukaendelea kuoza na kuharibika kabisa.. huko kwa mtalaam

R I p sonso
Duh!!!, Witchcraft will kill we black people.
 
Simba wachawi sana!
 
Majeraha aliyopata siku walipocheza na Simba pale ccm kirumba mwanza elewa Hilo jeraha ndo Hilo limemtoa uhai
Unanikumbusha ...Prof.Ngware alisema kana umeanza kula protein ukubwani unawapa shida sana walimu ...yaan unasoma michango yote hujaelewa...au umeingia tu ukakimbilia kuchangia
 
Kwa mambo haya ya ushirikina ndo maana nikienda nyumbani likizo natembelea ndugu zangu giza likianza kuingia tu.... Mchana mzima nakua maenei ya nyumbani kwetu.
 
Daah..! Pole kwa familia na Ruvu shooting.
Japo maelezo ya chanzo hasa cha kifo chake hayajitoshelezi na tukidhani ni kifo cha ushirikina ila tunasahau kuwa kuna ugonjwa wa tetenasi.
 
Daah..! Pole kwa familia na Ruvu shooting.
Japo maelezo ya chanzo hasa cha kifo chake hayajitoshelezi na tukidhani ni kifo cha ushirikina ila tunasahau kuwa kuna ugonjwa wa tetenasi.
Tetenasi inaua haraka sana. Baba mkwe wangu kidogo imuondoe.

.. Utakuta hakuchoma Sindano ya Tetenasi na alipata infections.
 
Ndugu utani wa Jadi wa Simba na Yanga uishie viwanjani na sio kwenye familia za watu.....hamjui jinsi gani mnawaumiza wanafamilia kwa kauli zenu kishabiki.......
 
Ofisa Habari wa Ruvu Shooting, Masau Bwire amezungumzia kifo cha mchezaji wao, beki Ally Mtoni 'Sonso' aliyefariki jana akiwa njiani kupelekwa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dar es Salaam.

Imeelezwa kuwa kabla ya kukutwa na umauti huo, Sonso nyota wa zamani wa Lipuli,Yanga, Kagera Sugar na Ruvu Shooting alikuwa akiuguza majeraha ya mguu tangu Oktoba, mwaka jana.

Bwire amesema Sonso beki huyo alipata majeraha mara baada ya mchezo wao wa Ligi Kuu dhidi ya Simba, uliopigwa Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

"Mke wake ndiye alianza kunipigia akitoa kilio, baadaye Baba yake aliniambia hivyo na muda huu naelekea nyumbani kwao kwa taratibu za mazishi hapo kesho Jumamosi sambamba na timu nzima kwa ujumla, hakika tutamkumbuka," amesema Bwire.

Tangu kutangazwa taarifa za msiba huo kumekuwa na idadi kubwa ya wachezaji na klabu mbalimbali zimetumia mitandao yao ya kijamii kuelezea kusikitishwa na msiba huo.

Source: Mwananchi

View attachment 2117083
R.I.P kamanda we are ur back
 
Back
Top Bottom