Japo mimi si forex trader ila ukweli ni kuwa forex is real na inafanywa hata na mabenki ambayo wewe umesema kuwa hawafanyi hii biashara.
Kuna kitu kinaitwa interbank market ambapo mabenki hufanya biashara hii hii ya forex baina yao. Na hawa mabenki ndiyo wana ukwasi mkubwa kwenye forex market. Ukienda bank unakuta pale wameweka bei za kuuza na kununua fedha za kigeni...thats forex!.
The interbank market is a global network used by financial institutions to trade currencies among themselves. They use it to manage their interest rate risks.
www.investopedia.com
Again unazungumzia forex na unaiponda kuwa ni virtual money na kuwa haina dili sana kama physical money ambayo wewe unadhani ndiyo mtu akitumia kufanya biashara atatoboa. Currency ni ile ile whether iwe virtual or physical..ni the same na value yake ni ile ile.
Ni sawa na uiponde pesa uliyotumiwa kwa Tigopesa au Mpesa kuwa ile msg inayokutaarifu kuwa una kiasi fulani cha pesa kwenye akaunti yako ya Mpesa kuwa si real money.
It seems una little understanding on how money is transferred. Mtu anapofund account yake iwe ya forex au ya kawaida tu ya benki si zile tunazowekewa kuonesha deposit au withdrawal ni virtual digits tu..? Na pesa unayowapa benki unadhani kuna mahala wanatunza kila mteja anawekewa separately?
Ukitumiwa hela toka US kuja TZ unadhani zile hela huwa zinapandishwa ndege toka US mpaka Tz? Lakini si unapata notification kuwa hela imeingia kwenye account yako toka kwa mtumaji from US? Naam hii ni interbank forex market.
Kwa kifupi naona wewe uliingia kwenye forex ukiwa na expectations kubwa na ikakupiga sasa zile disappointments zinakufanya uipe majina mabaya.
Unasema kuwa hakuna mabilionea wanaofanya forex? Kweli? Hizi hedge funds kubwa za kina George Soros na Paul Tudor ambao ni mabilionea waliopata ukwasi kwenye forex huzifahamu?
Forex ipo na ni real...mchongo uliopo ni little understanding ya retail traders wengi on markets. Ikiwa wewe ulikuwa disappointed haimaanishi sasa kuwa forex ni scam...forex was there before you..and it will be there after you are gone.
Ukiambiwa kuwa unaweza kutrade masoko ya hisa makubwa duniani ambayo nayo yanafata kanuni zile zile za forex market napo si utasema ni utapeli?
Those who say it cannot be done should not interrupt those who are doing it.