Kilichonitokea jana baada ya kuamka kula daku saa10, sitakuja kurudia

Kilichonitokea jana baada ya kuamka kula daku saa10, sitakuja kurudia

Mliofunga kama mimi poleni na mfungo muda si mrefu tunafuturu, tuendelee kuwa wavumilivu.

Juzi usiku nilikuwa nimepika futari nikala mida ya nne usiku nikasema ntaamka saa10 kula daku, nikaweka alarm ya saa kumi na nusu, kweli ilivyolia nikaamka kula.

Hadi kufikia saa11 nikaingia kulala nikaweka alarm ya saa1 asubuhi ili niwahi kibaruani, usingizi kila nikiutqfuta hauji nimekuja kulala saa 12 kasoro.

Alarm ya saa1 na nusu niliyoweka ilivyolia nikaizima nikasema nitaamka saa2, 🥲🥲si nikapitiliza mpaka saa4 asubuhi.

Nimeamua sitakula tena Daku maana nilishindwa hata kwenda kibaruani ikabidi nibaki tu ndani nagalagala.

Haya ndugu zangu tuwe na mfungo mwema, , uzi wa mapenzi mwezi huu tuachane nayo😁😁
Si Bure ulifakamia sana we jamaa
 
Back
Top Bottom