Siri ya sifuri
JF-Expert Member
- Sep 21, 2018
- 2,335
- 1,967
Mnasherehekea Rais Assad kuondolewa madarakani, huku mkisahau hao watakaochukua nchi hawana tofauti na Wataliba
Marekani,Israel pamoja na washirika wao wa magharibi wamepata goli la kujifunga, kusherehekea ni uendawazimu.
Kwa mtazamo wangu , serikali itakayofuata Syria italeta changamoto na usumbufu zaidi ya serikali iliyopinduliwa ya Assad.
Urusi na Iran watalazimika kurudi Mezani na serikali mpya ya Syria ili kuweka sawa mitazamo yao na kuishi kwa mwongozo wa ujirani mwema. Lakini ni dhahiri Marekani na washirika wake hawataendana na mipango ya Serikali mpya ya taifa huru la Syria, labda wafanikiwe kuweka kibaraka wao madarakni.