Kilichotokea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, ndicho kitakachofanyika 2020 ikiwa ni mpango wa Rais Magufuli kubadili Katiba kuondoa ukomo wa Urais

Kilichotokea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, ndicho kitakachofanyika 2020 ikiwa ni mpango wa Rais Magufuli kubadili Katiba kuondoa ukomo wa Urais

King Kisali

JF-Expert Member
Joined
Nov 20, 2019
Posts
1,041
Reaction score
1,349
Vitimbi na vituko vikivyotokea katika uchaguzi wa serikali za mitaa, mpaka kupelekea CCM kudai kushinda kwa asilimia mia moja serikali za mitaa na 99.8 vijiji.

Hizo ni njama zilizopangwa kuwahadaa Watanzania na ulimwengu wa kimataifa ionekane kuwa CCM na Rais Magufuli wanakubalika sana hivyo mwakani 2020 watafanya kila wawezalo ili ionekane CCM imeshinda over 95%.

Baada ya hapo bunge litakuwa na wabunge wengi wa CCM ndipo utapelekwa mswada wa sheria kubadili ukomo wa urais, vyanzo vya habari ambao ni wabunge waliopewa kazi ya kuzunguka nchi nzima kuwashawishi watu maarufu ili baadaye liibuke kundi la watu kumuomba Rais Magufuli aendelee na urais hata baada ya muda wake kuisha, mark my words.
 
Nimewaona wabunge wengi wa ccm ambao wameanza kujirejesha kwenye majimbo yao baada ya kupotea kwa takribani miaka minne, wanasema eti wao wataenda kumuomba rais JPM aendelee na urais licha muda wake kuwa umeisha ili akamalishe mambo na miradi aliyoianzisha.
 
IMG_20191125_194601.jpg

Haya matokeo ya kubumba kama yanavyoonyeshwa hapa ndio mkakati wenyewe wa kujifanya JPM na ccm wanakubalika kumbe ni ulaghai mtupu.
 
Watanzania tutaumia zaidi.Dr.Mpango anawakati mgumu sana wahisani bajeti. Mwakani ccm hawana mbadala kuwaumiza zaidi wanaichi kwa kodi zaidi, hivyo kufanya hila uchaguzi usifanyike ama wachukue madaraka kama walivyofanya serikali za vijiji na mitaa.
 
Usivuke mto kabla ya kuupima kina chake kwa fimbo,Kama maji ni mafupi unavuka pasina wasi wasi lakini kama ni marefu usithubutu.
 
IMG_20191124_100636.jpg

Mkakati mwingine huu hapa wa kununua wabunge, madiwani na wapinzani kwa gharama yoyote ile.Refer madiwani watano waliohama Chadema juzi na manunuzi bado yanaendelea.
 
IMG_20191123_132614.jpg

Mkakati mwingine ni huu wa wabunge kuzunguka katika majimbo yao wanawashawishi watu maarufu.
 
IMG_20191128_182838.jpg

Huyu anatumika kujaribu kuwazuia wahisani na mataifa ya n'je kutoingilia mambo ya ndani, kumbe ni kisingizio he is creating environment, rejea kauli ya juzi juzi kuhusu wafadhili.
 
Kishindo cha kumng'oa jiwe kitakuwa kikubwa sana kama atajichanganya kuongeza muda wa urais.
Kweli ana mpango huo maana kuna mbunge ambaye ni mwenyekiti wa moja ya kamati matata sana ya bunge ndio alituita mwanzoni mwa wiki hii kutushawishi.
 
IMG_20191126_190649.jpg

Mbinu nyingine inayotumiwa ni kuwafungulia kesi za kubambika wapinzani wote wanaokataa kuunga mkono juhudi ili kuua upinzani.
 
Back
Top Bottom