Walichukua Form watu 42 wenye uwezo wa kuongoza nchi ndani ya CCM . Na walizunguka mikoa yote kutafuta wadhamini.
Chadema walimwacha Mbowe awachagulie mgombea badala ya kuwashindanisha ili wanachama waone hoja zao wajue nani mwenye uwezo.
Mfano Mbowe leo alipaswa kustaafu uenyekiti ili aache nafasi kwa wengine wapige kampeni ya kujinadi kuwa watakifanyia nini Chama katika mazingira ya sasa ya mbinyo wa Demokrasia.
Kwa vyovyote angepatikana mtu mwenye roho ya ushawishi kwenye jamii. Mtu ambaye akisema kesho tuelekee Dodoma kudai Uhuru wa kisiasa watu wangetoka Pande zote za Tanzania kuelekea huko. Serikali ya mkoloni ilikua katili sana lakini Hoja na imani ya watanganyika kwa viongozi wa harakati za kupigania Uhuru ziliwashinda wakoloni.
Chama kinapukutika wabunge,chama kinapikutika madiwani,chama kimekosa hata mjumbe mmoja wa serikali za mitaa halafu Mbowe anatuambia yeye pekee ndiye anayeweza kupambana na serikali ya Awamu ya Tano. Wagombea wa Ubunge wanaporwa Fom mchana kweupe hakuna hatua kali ya kuwakatisha tamaa kabisa wanaofanya ushenzi huo.Wanachama na viongozi wanatekwa mpaka jimboni kwake ,wanapotea kama Saanane Mwenyekiti kimya anachoangalia ni uenyekiti wake tu usiguswe.
Hayo mapambano yake ni yapi?
Tafakari vizuri mkuu.