Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Siku moja kabla ya kufunga ndoa Mwenyekiti wa TLP Taifa, Dk. Augustino Mrema amesema kuwa atajaribu kujikokota kuelekea Kanisani na kama itatokea ataishia njiani kutokana na afya yake kutokuwa sawa, anaamini Paroko atajua nini cha kufanya.
Mrema amesisitiza kuwa huduma ya Kanisa inapatikana popote, ikitokea hata ameshindwa kwenda Kanisani anaweza kufungishwa ndoa chumbani kwake au hata kitandani kwake ilimradi wahusika wameridhia.
Kuhusu kuoa akiwa mtu mzima, Mrema amesema: “Dhumuni la ndoa ni kupata watoto kama hawapatikani si basi, kwani kuna ugomvi?”
Mrema anatarajiwa kufunga ndoa Alhamisi Machi 24, 2022 katika Parokia ya Uwomboni kijijini kwake Kiraracha mkoani Kilimanjaro.
Mrema ambaye ana umri wa miaka 77 akiwa pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya PAROLE Tanzania, amekuwa akijinadi kupata mrembo mwenye umri mdogo na mweupe, anafunga ndoa baada ya kumpoteza aliyekuwa mkewe Rose Mrema aliyefariki dunia mwaka jana.
Amesisitiza kuwa kilichomsukuma kuoa ni kumpata msaidizi wa kumsaidia katika maisha yake kwani yeye ni mzee na anahitaji mtu wa karibu wa kumwangalia na kumsaidia kwa ukaribu, akisisitiza familia yake kumpa ruhusa ya ndoa hiyo.
“Kuhusu jina la mke wangu mtarajiwa mtalijua siku ya ndoa, pia kutakuwa na sherehe nyumbani kwangu pamoja na ibada ambapo Paroko pia atazindua sanamu ya mtakatifu Augustino hapohapo nyumbani kwangu,” alisema Mrema.
Pia soma...
Augustino Mrema kufunga ndoa Machi 24, 2022. Amepata kimwana mdogo