Kilimanjaro: Mama amuua mtoto wake kwa kosa la kufungilia bomba la maji

Kilimanjaro: Mama amuua mtoto wake kwa kosa la kufungilia bomba la maji

Akilihuru

JF-Expert Member
Joined
May 20, 2022
Posts
1,512
Reaction score
2,980
Hii sasa ni hatari, hatujui dunia inaelekea wapi. Siku hizi ni kawaida kusikia mtoto kamuua mzazi wake au mzazi kamuua mtoto wake.

Ni kawaida kusikia mume kamuua mke wake au mke kamuua mume wake. Yani ni vurugu mechi kila iitwayo leo.

 
Haya mambo yalikuwepogi tangu zamani Sema tu Dunia ya Sasa ipo kiganjani tunapata Habari online on time
 
Haya mambo yalikuwepogi tangu zamani Sema tu Dunia ya Sasa ipo kiganjani tunapata Habari online on time
Ya ni kweli mkuu, wala haujakosea. Yalikuwepo toka enzi hizo ila yalikuwa hayaripotiwi kama ilivyo sasa.
 
Gharama za maisha,mama aliwaza bili ya maji itakuaje akapandwa na hasira akashindwa kujizuia.
Ndio maana wahenga walisema hasira hasara. Hili lililotokea ni moja ya hasara iliyosababishwa na hasira. Mama sasa anajuta kwa kile alichokifanya.
 
Rip mtoto jamani [emoji22]
Mwenye Enzi Mungu aingilie kati kwa kweli uwiii
 
Haya mambo ya kuuana mama na mtoto, mume na mke, baba na mtoto mbona hatuyasikii kwa jamii za Pwani kama wazaramo, wakwere, wandengereko etc
 
Mbona huwa mnasena Kilimanjaro ni wasomi na matajiri, kulikoni tena mtu anauliwa kwa sababu ya kufungua bomba la maji ?
 
Huku Pwani ni kuchambwa na kusutwa tu,hakuna muda wa kuweka mzigo rohoni
 
Back
Top Bottom