Kilimanjaro, Mtwara na Lindi zaongoza idadi kubwa ya wazee

Kilimanjaro, Mtwara na Lindi zaongoza idadi kubwa ya wazee

Riskytaker

JF-Expert Member
Joined
Mar 14, 2024
Posts
568
Reaction score
2,522
Matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022 yanaonyesha mikoa ya Kilimanjaro, Mtwara na Lindi inaongoza kwa idadi kubwa ya wazee wenye umri zaidi ya miaka 65.

Ripoti hiyo ilizinduliwa Zanzibar na Waziri Mkuu ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Sensa Kitaifa, Kassim Majaliwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar ambaye ni Mwenyekiti Mwenza wa Kamati hiyo, Hemed Suleiman Abdulah Aprili 15, 2023.

Ripoti hiyo, inaonesha Mkoa wa Kilimanjaro unaongoza kuwa na idadi kubwa ya wazee wenye umri wa zaidi ya miaka 65 kwa asilimia 7.3 ambayo ni sawa na wazee 135,921 ikifuatiwa na Mtwara yenye asilimia 6.4 sawa na wazee 104,636.

Aidha, Lindi yenye wakazi milioni 1.2, asilimia sita ni wazee wenye umri zaidi ya miaka 65 ambayo ni sawa na watu 71,641. Sawa na katika kila watu 10, wastani wa mtu mmoja ni mzee kwenye mikoa hiyo.

Kwa upande wa mikoa yenye idadi ndogo ya wazee, ripoti hiyo inautaja Mkoa wa Katavi kuongoza kwa asilimia 2.3 ukifuatiwa na mikoa ya Dar es Salaam, Mjini Magharibi na Geita yenye asilimia 2.4 kwa kila mmoja.

Hata hivyo, wastani wa kitaifa unaonyesha kati ya Watanzania milioni 61.7, wenye umri zaidi ya miaka 65 ni asilimia 3.8 pekee ambayo ni sawa na watu milioni 2.3.
 

Attachments

  • Screenshot_20240812-131140.jpg
    Screenshot_20240812-131140.jpg
    287.5 KB · Views: 5
Huna taarifa au ndo wale wa kupiga nyungu covid ilimaliza sana sio mijini wala vijijini, nilipoishi tu wakati ule ilikuwa ni misiba 8-14 kwa siku 3-7
Sio kiwango hiko, watanzania hasa wanaume wana kufa mapema toka miaka mingi ya nyuma. Changamoto za ugumu wa maisha, ukosefu wa bima za matibabu na kadhalika.
 
Umeamua kuwa mbishi naona na hiyo kazi siiwwezagi
Toa takwimu za kutetea hoja yako.. wewe una okoteza taarifa ambazo sio. Kipindi cha Covid walifariki wazee ndio lakini sio wengi hawawezi hata kufika 200k na wengi ni walio kuwa maeneo ya mjini.
 
Kumbe uzee ni kuanzia miaka 65.

Mzee Magoma mwenye 58 kumbe sio mzee!
 
Mkoa inayoongoza kwa wazee wengi Ni mkoa wa Pwani. Wilaya ya kibaha na Bagamoyo.
 
Mkoa inayoongoza kwa wazee wengi Ni mkoa wa Pwani. Wilaya ya kibaha na Bagamoyo.
Mikoa hiyo ni Kilimanjaro na Mtwara ndio ina ongoza kwa wezee wengi nenda Marangu na maeneo mengine ya uchagani wapo wazee wenye miaka 100 na zaidi wengi tuu wana tembea na akili zao bado zipo vizuri
 
Toa takwimu za kutetea hoja yako.. wewe una okoteza taarifa ambazo sio. Kipindi cha Covid walifariki wazee ndio lakini sio wengi hawawezi hata kufika 200k na wengi ni walio kuwa maeneo ya mjini.
Nimekupa takwimu za mtaa niliokuwepo umekataa,

Ok
 
Yani hii nchi kwa sasa Kikwete ndiye rais mstaafu pekee aliyebaki.

Ukifika miaka 50 unaitwa mzee.

Wakati Michael Jackson kafariki na miaka 50, Wamarekani wamelalamika kafariki mdogo sana.
Nami nashangaa,sema nini akishafikisha umri huo nae ataanza kuwalalamikia wenzie wanaomwita mzee
 
Back
Top Bottom