Kilimanjaro: Mwalimu agomea kuhama, vitu vyake vyatolewa nje Siha

Mwizukulu mgikuru

JF-Expert Member
Joined
Oct 21, 2021
Posts
6,788
Reaction score
16,227
Familia ya aliyekuwa mwalimu wa Shule ya Sekondari Karansi, Wilaya ya Siha mkoani Kilimanjaro, imelazimika kulala nje kwa siku sita baada ya nyumba waliyokuwa wakiishi kufungwa na mali zao kutolewa nje, kufuatia uamuzi wa kumtaka mwalimu huyo kuondoka katika nyumba hiyo.

​
Mwalimu huyo, Omary Salum Ally, alihamishwa kutoka Karansi kwenda Shule ya Sekondari Dahani Novemba 2025, lakini aliendelea kuishi katika nyumba ya shule akidai kuwa ana hofu kuhusu usalama wake katika kituo kipya alichopangiwa.

Omary amesema awali aliomba kuhamishiwa Jiji la Tanga, lakini ombi hilo lilikataliwa na badala yake akapangiwa Dahani.

Amesema katika kipindi hicho alikumbana na mashtaka ya kinidhamu, ikiwemo tuhuma za kutotii mamlaka, lakini amesisitiza kuwa ana hofu kuhusu usalama wake na watoto wake katika kituo alichopangiwa.

Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Siha, Alfred Myombo, amekiri kuondolewa kwa mwalimu huyo katika nyumba ya Shule ya Sekondari Karansi, akisema hatua hiyo ilichukuliwa kwa kuwa siyo tena mwalimu wa shule hiyo na nyumba ilihitajika kumpisha mwalimu mwingine aliyepangiwa kituo hicho.
 
kwa uelewa wangu nahisi ana changamoto ya kufili....majobles wameweza kupanga vyumba wewe na ajira yako unashindwaje😣
View attachment 3674514
Kabla sijafika Kilimanjaro, nilikuwa naamini ni sehemu ya watu walioelimika na kustaarabika sana. Kumbe nako hakuko nyuma kwa mambo ya kijinga, kiswahili na kishamba shamba.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…