Soulja boy
JF-Expert Member
- Oct 3, 2015
- 4,052
- 7,375
Duh mwalimu tayar kala Mvua.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Profesa Adolf Mkenda ‘ waziri wa Elimu na Mbunge waJimbo la Rombo , sasa umebipiwa!!Mwanafunzi wa darasa la kwanza, shule ya msingi Samanga, Wilaya, ya Rombo, mkoani Kilimanjaro, Sistus Aristid Kimario. (7) amefariki dunia kwa kile kinachodaiwa ni kuchapwa viboko na mwalimu wake kwa kosa la kupiga kelele darasani.
Inadaiwa baada ya mwalimu huyo, James Urassa kutekeleza adhabu hiyo alitoroka kusikojulikana baada ya kubaini mwanafunzi huyo amefariki dunia.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Simon Maigwa alisema tukio hilo limetokea Julai 17, mwaka huu, baada ya mwalimu huyo kumtandika viboko mwanafunzi huyo na kusababisha umauti wake.
"Jeshi la Polisi tunaendelea kumsaka mwalimu huyu kwa sababu baada ya kubaini mwanafunzi huyo amefariki amekimbia," alisema Kamanda Maigwa.
Alipotafutwa Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Charles Chavunike, alikiri kutokea kwa tukio hilo Julai 17, mwaka huu saa tatu asubuhi.
Mwalimu huyo alisema akiwa darasani aliona walimu wawili wa shule hiyo wakiwa wamembeba mwanafunzi huyo akitolewa darasani na alipowauliza nini kimetokea alijibiwa mwanafunzi kaanguka darasani
"Baada ya hapo niliita watoto wawili wa darasa la kwanza nikawahoji ni kitu gani kimetokea darasani, ndiyo wakanieleza mwalimu alimchapa mwenzao kwa sababu ya kupiga kelele darasani," alisema.
Alisema baada ya tukio hilo alilazimika kufuata taratibu zote na kutoa taarifa kwa viongozi wa wa kata na vyombo vingine vya dola.
Naye babu wa mwanafunzi huyo, Patricky Kachomba alise-ma mpaka anaondoka kwenda shule alikuwa haumwi popote.
Huko Kilimanjaro Mwalimu amempiga mwanafunzi wa darasa la kwanza mwenye umri wa miaka saba mpaka kifo kwa kosa la kupiga kelele darasan 🥲
Kwenye picha huyo ni Mama yake Mzazi wa huyo mwanafunzi ameeleza kwamba Mwalimu
Alimpiga sana mwanafunzi huyo mpaka alijikojolea baada ya hali kuwa mbaya ya mwanafunzi alifariki dunia, Mwalimu amekimbia na jeshi la polisi linaendelea kumtafuta huyo Mwalimu na kufanya uchunguzi wa shitaka hili.
#VibokoSioLazima
Credit: UTV Habari
---
Mwanafunzi wa darasa la kwanza, shule ya msingi Samanga, Wilaya, ya Rombo, mkoani Kilimanjaro, Sistus Aristid Kimario. (7) amefariki dunia kwa kile kinachodaiwa ni kuchapwa viboko na mwalimu wake kwa kosa la kupiga kelele darasani.
Inadaiwa baada ya mwalimu huyo, James Urassa kutekeleza adhabu hiyo alitoroka kusikojulikana baada ya kubaini mwanafunzi huyo amefariki dunia.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Simon Maigwa alisema tukio hilo limetokea Julai 17, mwaka huu, baada ya mwalimu huyo kumtandika viboko mwanafunzi huyo na kusababisha umauti wake.
"Jeshi la Polisi tunaendelea kumsaka mwalimu huyu kwa sababu baada ya kubaini mwanafunzi huyo amefariki amekimbia," alisema Kamanda Maigwa.
Alipotafutwa Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Charles Chavunike, alikiri kutokea kwa tukio hilo Julai 17, mwaka huu saa tatu asubuhi.
Mwalimu huyo alisema akiwa darasani aliona walimu wawili wa shule hiyo wakiwa wamembeba mwanafunzi huyo akitolewa darasani na alipowauliza nini kimetokea alijibiwa mwanafunzi kaanguka darasani
"Baada ya hapo niliita watoto wawili wa darasa la kwanza nikawahoji ni kitu gani kimetokea darasani, ndiyo wakanieleza mwalimu alimchapa mwenzao kwa sababu ya kupiga kelele darasani," alisema.
Alisema baada ya tukio hilo alilazimika kufuata taratibu zote na kutoa taarifa kwa viongozi wa wa kata na vyombo vingine vya dola.
Naye babu wa mwanafunzi huyo, Patricky Kachomba alise-ma mpaka anaondoka kwenda shule alikuwa haumwi popote.
Kilimanjaro tu?Walimu wenzangu tuna stress ila majuto no mjukuu.
Na Kwa Nini Kilimanjaro tu?
- Moshi: Mwalimu mbaroni akituhumiwa kusababisha kifo cha mwanafunzi kwa kumpiga mateke
- Tume yatua Kilimanjaro uchunguzi kifo tata cha Nusura
Ahse nitawalima walimike manina zao[mention]Mpwayungu Village [/mention] apewe ukiranja kwa hawa walimu ili awanyooshe
[emoji28][emoji28][emoji28]Ebu pitia hapa tafadhali mwalimu Mpwayungu Village
Tatizo kubwa ni kwamba bado serikali inaruhusu adhabu ya viboko. Najua kuna utaratibu wameweka wa kuchapa wanafunzi lakini hakuna mwalimu au shule inayoufuata na serikali iko reluctant kukazia au kufuatilia. Dunia ya sasa iliyostaarabika viboko ni adhabu ya kikatili mno. Hebi fikiria mtoto wa miaka 7 anaanza kupata kipigo kikali namna hiyo!Tukikataza kupiga watoto tunaitwa wakina mama Junia [emoji24][emoji24][emoji24]
Rest in Peace Angel, [emoji885]
Huyo bazazi atahangaika na Dunia na atakufa kifo cha kikatili sana.