Kilimanjaro: Mwanamke mmoja Amuua mama yake mzazi ili arithi shamba

Kilimanjaro: Mwanamke mmoja Amuua mama yake mzazi ili arithi shamba

Bushmamy

JF-Expert Member
Joined
Aug 18, 2019
Posts
9,140
Reaction score
15,963
Mwanamke mmoja ajulikanae kwa jina la Rosalia Chuwa mwenye umri wa miaka 59 kutoka katika kijiji cha Utaruni ,mkoani kilimanjaro amemuua mama yake mzazi ajulikanae kwa jina Anastasia Shio mwenye umri wa miaka 89 ili arithi shamba.

Mwenyekiti wa ukoo huo amesema ya kuwa tangu Muda mrefu Rose amekuwa na tamaa ya kurithi shamba hilo na alishasikika akisema kuwa ipo siku atamuua mama yake ili arithi shamba.

Nae dada wa mtuhumiwa ajulikanae kwa jina la Getrude amethibitisha kuwa ni kweli dada yake alishwahi kusema mara kadhaa atamuua mama yake ili arithi shamba hilo.

Mwili wa marehemu baada ya kufanyiwa uchunguzi utazikwa kesho jumatano nyumbani kwake.

Soma Pia:
 
Mwanamke mmoja ajulikanae kama Rosalia Chuwa mwenye umri wa miaka 59 kutoka katika kijiji cha Utaruni ,mkoani kilimanjaro amemuua mama yake mzazi ajulikanae kwa jina Anastasia Shio mwenye umri wa miaka 89 ili arithi shamba.
Mwenyekiti wa ukoo huo amesema ya kuwa tangu Muda mrefu Rose amekuwa na tamaa ya kurithi shamba hilo na alishasikika akisema kuwa ipo siku atamuua mama yake ili arithi shamba.

Nae dada wa mtuhumiwa ajulikanae kwa jina la Getrude amethibitisha kuwa ni kweli dada yake alishwahi kusema mara kadhaa atamuua mama yake ili arithi shamba hilo
Wa-Kibosho bhana.
 
Kuna event sawa na hii ilitokea miaka 2 ama 3 iliyopita binti alimuua mama yake ili arithi mali huko huko Kilimanjaro.

Hivi mambo za urithi nilifikiri watoto ambao wana nafasi kubwa ya kuyatenda ni wa kiume ila naona kwa wachaga wa kike ndio wako vizuri.

Haya mambo ya wazazi kuuwawa na watoto sababu ya urithi, mali, bima za maisha nimrkua nikizisikia na kuxiona sana nchi zilizoendelea lakini naona sasa zinashamiri hata huku kwetu.

Huyo mama apumzike kwa amani na huyo binti apate haki yake.
 
Ko miaka yote 59, alikua anabwetekaa, ili arithi shambaa? Hivi wachagaa mmeanza kurukwa na akili?
Woiiiiiih [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Back
Top Bottom