Kilimanjaro: Mwanamke mmoja Amuua mama yake mzazi ili arithi shamba

Kilimanjaro: Mwanamke mmoja Amuua mama yake mzazi ili arithi shamba

Kuna event sawa na hii ilitokea miaka 2 ama 3 iliyopita binti alimuua mama yake ili arithi mali huko huko Kilimanjaro.

Hivi mambo za urithi nilifikiri watoto ambao wana nafasi kubwa ya kuyatenda ni wa kiume ila naona kwa wachaga wa kike ndio wako vizuri.

Haya mambo ya wazazi kuuwawa na watoto sababu ya urithi, mali, bima za maisha nimrkua nikizisikia na kuxiona sana nchi zilizoendelea lakini naona sasa zinashamiri hata huku kwetu.

Huyo mama apumzike kwa amani na huyo binti apate haki yake.

 
Mwanamke mmoja ajulikanae kwa jina la Rosalia Chuwa mwenye umri wa miaka 59 kutoka katika kijiji cha Utaruni ,mkoani kilimanjaro amemuua mama yake mzazi ajulikanae kwa jina Anastasia Shio mwenye umri wa miaka 89 ili arithi shamba.

Mwenyekiti wa ukoo huo amesema ya kuwa tangu Muda mrefu Rose amekuwa na tamaa ya kurithi shamba hilo na alishasikika akisema kuwa ipo siku atamuua mama yake ili arithi shamba.

Nae dada wa mtuhumiwa ajulikanae kwa jina la Getrude amethibitisha kuwa ni kweli dada yake alishwahi kusema mara kadhaa atamuua mama yake ili arithi shamba hilo.

Mwili wa marehemu baada ya kufanyiwa uchunguzi utazikwa kesho jumatano nyumbani kwake.

Soma Pia:

59 yrs bado anagombea urithi? Inasikitisha Sana.
 
Hakumbuki kale kamfuko alikokalia miezi 9 ndani ya tumbo la mama? Inasikitisha, tunaishi na mashetani bila kujua. Ikithibitishwa anyongwe ili akaonane na mama.
 
Binti aliona Bi Mkubwa wake amechelewa kufa (miaka 89) ili awahi urithi 🙌

Wazazi tuna changamoto kubwa ya tishio la kuuawa na Watoto wetu ili warithi mali.

Tujitahidi kuwapatia Elimu bora watoto wetu ili waweze kujitambua kwamba hata Mimi Baba yake, hizo Mali nilizonazo nimezipata Kwa kufanya kazi Kwa bidii pamoja na kujinyima vingi
 
Back
Top Bottom