Kilimanjaro: Pombe ya Simba yatajwa kusababisha vijana kuvimba mashavu

Nimesoma habari kuwa RC wa kilimanjaro kafungia kiwanda kinachozalisha pombe aina ya simba kwakuwa si nzuri kwa afya ya binadamu kwakuwa ina asidi nyingi.

Anadai alifika pale kiwandani akachukua sample akaipeleka TBS na majibu yakaja kuwa ile pombe ina asidi kwa kiasi kikubwa.
Sasa najiuliza hawa TBS kazi yao nini?

Yani mpaka RC ajiongeze achukue sample ndo waje na majibu. Na bila shaka hiyo pombe ina nembo ya TBS na wakati wanafungua kiwanda walifuata procedures zote ikowemo TBS na TMDA.

Lakini ina maana hawakukagua hizo sample. Jana tu nilikuwa naongea na jamaa namwambia TZ taasisi nyingi hazifanyi kazi zipo tu kutoa vibali na kukusanya pesa ni kama formalities tu.
 
Taasisi za serikali ni wanataka watafuniwe na kulishwa wao wameze tu
Hizi kazi hata kama mnaekana wekaneni na watu wenye uwezo tupo dorooo
 
Waweke na nguvu huku Arusha matejoo,juzi nimepita hiyo mitaa ya matejo yani mtaa mzima unanuka gongo na mitambo ya kuchemshia gongo zipo kabisa.ukicheki vijana,wazee wamevimba mashavu kwakubugia gongo inamana mapolisi hawaoni na ni town Kati!?
 
Taasisi za serikali ni wanataka watafuniwe na kulishwa wao wameze tu
Hizi kazi hata kama mnaekana wekaneni na watu wenye uwezo tupo dorooo
Same kama pccb, mpaka waagizwe na raisi, mkuu wa mkoa, waziri ndo wachunguze
 
Rombo Ndo kisima Cha ulevi Tanzania[emoji2]

Hii wilaya haiwez pita miez 3 ujapata kiss kinachotokana na pombe
 
lazima rushwa imetembea hapo.
Hao Simba kwanza wana nembonya TBS.

Pili, ukiachana na TBS ambao wana ofisi za kanda, watu wanaohusika na masuala ya Afya ni kitengo cha Afya cha Halmashauri, hasa Afisa Afya wa Wilaya.

Tatizo vurugu nyingi, muingiliano wa majukumu haijulikani nani ni nani ???!!!

Na hapa kuna vita ya kibiashara.

Kampuni kubwa inayozlisha hizi pombe za aina hii ni Raha Poa ambao kiwanda chao kiko Arusha.

Hao watu inawezekana wamehonga huko, ili kupambana kuwaondoa Simba sokoni.
 
both simba na hao raha wanauza uchafu kwa watz.
 
Kumekucha
 
Ilipaswa TAKUKURU waichunguze TBS kwanini wamepigwa ganzi kwenye hili hadi Mkuu wa Mkoa anafanya kazi yao.
TBS kutakuwa na ombwe la uongozi, sidhani kama shirika hili muhimu kwa afya na uchumi wa watanzania linao viongozi weledi. Tatizo la viongozi wengi katika tanzania hii ya leo wanawekwa kindugu na kikabila
 
Sasa hadi uzalishaji umeanza bidhaa imeingizwa sokoni TBS walikuwa wap? Ila hii nchi niya ovyo sana
tbs ni shirika linalofanya kazi kikabila sana, karibia viongozi wote wakuu wanatokea kanda moja . hapa hamna wa kumwajibisha mwingine
 
Ilipaswa TAKUKURU waichunguze TBS kwanini wamepigwa ganzi kwenye hili hadi Mkuu wa Mkoa anafanya kazi yao.
viongozi wabovu wanafukuzwa baada ya muda wanarudishwa na kuendelea na uozo uleule, tatizo la tbs ni uongozi, sasa usalama wa chakula hauna mwenyewe, mpaka mkuu wa mkoa agundue bidhaa haina usalama hangali wenye mamlaka tbs wapo?
 
Bora TFDA irudi katika majukumu yake.

#MaendeleoHayanaChama
 
Kuvimba mashavu ni tatizo...

Ila kutelekeza familia siyo hoja ni binadamu mwenyewe hata asipotumia pombe anaweza telekeza...
Kutelekeza familia ni matokeo ya kunywa pombe zisizo bora na salama zinazoharibu nguvu za kiume na kusababisha mwanaume asione tena faida ya mke
 
Rusha picha tuone mashavu ya akina mroso na lyarukwa
usiombee yakukute, unashangaa kijana ananenepa mashavu tu huku sehemu nyingine ya mwili ikiwa nyembamba, nadhani siyo haki na ubinadamu kuweka picha ya mwathirika hapa
 
Tangu tarehe 1 mwezi huu hii kampuni imeanza kuzalisha tena pombe hizohizo kwa kiwango kilekile!

Yani ukiziweka dukani kuna saa zinalipuka kama baruti.... Wanatumia ndizi kidogo sana, sukari nyingi, maji na hamira.
TBS wakakague hiki kiwanda maana pombe inazalishwa mazingira hatari sana.
Kibaya zaidi wafanyakazi wanalewa hovyo na hizo pombe kwa kuwa wanalipwa Tsh 6,000 kwa siku baada ya kufanya kazi masaa 12 au masaa 13... Yani unaingia kazini saa moja na nusu asubuhi unatoka saa moja na nusu jioni 🤔
 
Mbona sijasikia kama wanapelekwa mahakamani lini, au hayo madhara wamepata ng’ombe na sio binadamu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…