Bushmamy
JF-Expert Member
- Aug 18, 2019
- 9,140
- 15,963
Mlembea, ni moja ya Shule ya Serikali iliyopo Wilaya ya Rombo katika Tarafa ya Mashati Mkoani Kilimanjaro ambapo kwa Mwaka huu wa 2024 imeandikisha Wanafunzi watatu tu (3) kuingia darasa la kwanza kitu ambacho sio kawaida.
Shule hiyo ya Msingi Mlembea jumla ya idadi ya wanafunzi katika shule nzima Kuanzia chekechea hadi darasa La saba inakadirwa kuwa na wanafunzi tisini (90) tu.
Sababu kuu mbili za shule hiyo kuwa na idadi ndogo ya wanafunzi kuliko shule nyingine inatajwa kuwa ni mambo ya kishirikina yaliyotokea miaka ya nyuma ambapo wanafunzi walikuwa wanadondoka wawapo shuleni hivyo kufanya wazazi kuhamisha watoto wao na kuwaandikisha katika shule nyingine. Ndani ya Tarafa hiyo.
Pia soma:

- Mkurugenzi Rombo: Shule iliyoandikisha Wanafunzi Watatu hakuna imani za kishirikina ni maamuzi ya wazazi tu
- Kilimanjaro: Baada ya Shule kuandikisha Wanafunzi Watatu tu, Serikali yaanzisha msako kutafuta Watoto waliopo mtaani