DOKEZO Kilimanjaro: Shule ya Msingi ya Serikali yaandikisha Wanafunzi watatu (3) kuanza Darasa la Kwanza

DOKEZO Kilimanjaro: Shule ya Msingi ya Serikali yaandikisha Wanafunzi watatu (3) kuanza Darasa la Kwanza

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

Inawezekana yakawa ni moja ya maajabu duniani yanayofaa kuingia katika kitabu cha maajabu cha Guiness, baada ya shule ya msingi Mlembeya iliyopo Rombo kuandikisha watoto watatu tu wa darasa la kwanza 2024.

Wakati kukiwa na shule nyingine za msingi katika baadhi ya mikoa zikiwa na zaidi ya wanafunzi 800 hadi 3,000, shule hiyo ambayo ni miongoni mwa shule 162 za msingi zilizopo wilayani Rombo mkoani Kilimanjaro, ina jumla ya wanafunzi 90.

Shule hiyo imekuwa gumzo katika mitandao ya kijamii kuanzia wiki iliyopita taarifa zake zilipoanza kusambaa kuwa imeandikisha wanafunzi watatu tu wa darasa la kwanza na watoto sita wa darasa la awali, na kufanya wanafunzi wapya kuwa 9.

Wakizungumza baadhi ya wazazi wamesema idadi ya wanafunzi iwa kupungua mwaka hadi mwaka shuleni hapo kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo uwepo wa mzunguko wa shule zaidi ya nne katika eneo hilo pamoja na baadhi ya wazazi kupeleka watoto katika shule za binafsi.

Akizungumza kwa njia ya Simu, Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya hiyo, Godwin Chacha amesema shule hiyo yenye jumla ya wanafunzi 90, imepanga kuandikisha wanafunzi wasiozidi11 wa darasa la kwanza mwaka huu.

Kwa upande wake mkuu wa Wilaya ya Rombo, Raymond Mwangwala alisema mpaka sasa katika Wilaya hiyo tayari wameandikisha wanafunzi 4,639 wa awali na wanafunzi 4,454 wa darasa la kwa kwanza katika Wilaya hiyo na kwamba watachukua hatua za kisheria ambao hawatapeleka watoto shule.

Mwananchi
 
Mbona sioni issue hapa. Ni kwamba supply imezidi demand.
Pia, uwiano wa mwalimu mmoja watoto watatu, kwa asilimia kubwa ufaulu lazima uwe juu.
 
Watafutwe vijana kumi wa kisukuma na kumi wa kingoni walazimishwe kuishi uko na wanawake hamsini wa rombo walazimishwe kuzaa na hao vijana watoto watano watano..iwe sheria
 
Back
Top Bottom