Abdul Said Naumanga
JF-Expert Member
- Jan 28, 2024
- 673
- 1,318
Mahakama ya Rufani ya Tanzania imebariki hukumu ya kunyongwa hadi kufa kwa washitakiwa watatu, Ibrahim Abubakar, Salima Abubakar, na Hadija Shio, ambao walikutwa na hatia ya kumuua kikatili aliyekuwa mjumbe wa nyumba kumi huko Kibosho Kirima, Moshi - Kilimanjaro, Mrh. Titus Sebastian Kimaro.
Kulingana na ushaidi uliotolewa katika kesi hii, tukio hilo la kusikitisha lilitokea mnamo tarehe 28 Aprili 2019, majira ya saa tisa alasiri katika eneo la Kibosho Kirima, Wilaya ya Moshi Vijijini, Mkoa wa Kilimanjaro. Mrh. Kimaro, ambaye alikuwa kiongozi wa kitongoji hicho kwa nyazfa ya mjumbe wa nyumba kumi, alifika katika eneo la tukio kwa lengo la kusuluhisha mgogoro wa ardhi baina ya familia ya washitakiwa na jirani yao aitwaye Joseph.
Pia soma: Mahakama Kuu yamhukumu Grace Mushi kunyongwa hadi kufa kwa kumchoma mpenzi wake ndani ya nyumba mpaka kufa
Hata hivyo, hali ilibadilika ghafla wakati washitakiwa walipohisi kuwa Mrh. Kimaro alikuwa na upendeleo upande wa mpinzani wao (Joseph). Wakiwa na hasira kali, washitakiwa walimshambulia kwa kutumia mapanga, mishale na mkuki, na kumsababishia majeraha mengi yaliyosababisha kifo chake.
Mashuhuda wa tukio hilo, akiwemo mke wa marehemu Regina Titus, binti yao Esther Titus Kimaro, na jirani yao Francis Ferdinand Mwacha, waliona kwa macho yao shambulio hilo la kinyama. Baada ya tukio hilo, polisi walifika katika eneo la tukio ambapo walikamata silaha zilizotumika ikiwemo panga, upinde, mishale 19, na mkuki. Mwili wa marehemu ulisafirishwa hadi Hospitali ya KCMC ambapo uchunguzi wa mwili ulifanyika na kubaini kuwa kifo kilisababishwa na kuvuja damu nyingi kutokana na majeraha ya kukatwa.
Washitakiwa, walipofikishwa mahakamani, walikana mashtaka dhidi yao na kudai kuwa walihusishwa kimakosa katika tukio hilo la mauaji, wakieleza kuwa walikuwa wakikabiliwa na mgogoro wa kidini na majirani zao ambao ulisababisha nyumba yao kuchomwa moto. Licha ya utetezi wao, Mahakama Kuu ilithibitisha hatia yao na kuwahukumu kunyongwa hadi kufa.
Tarehe 16 August mwaka huu, rufaa yao dhidi ya hukumu hiyo ilitupiliwa mbali na Mahakama ya Rufani ya Tanzania, ambayo iliunga mkono uamuzi wa Mahakama Kuu kwamba ushahidi uliotolewa ulikuwa wa kutosha kuwahusisha washitakiwa na mauaji hayo ya kikatili.