Kilimanjaro: Walimu shule nzima waomba uhamisho, kisa utata walimu wazawa

D___________Loy

Senior Member
Joined
Jan 21, 2020
Posts
190
Reaction score
205
SHULE ya Msingi Nkweshoo iliyoko Kijiji cha Nkuu Ndoo, Kata ya Machame Mashariki, Wilaya ya Hai, Kilimanjaro, ambayo ina walimu watatu pekee wanaofundisha wanafunzi 175, walimu wote wameandika barua ya kuomba uhamisho.

Walimu hao wanadaiwa kutoridhishwa na vitendo vya baadhi ya wazazi kutaka shule hiyo, wanafunzi wake wafundishwe na walimu wazawa.

Kutokana na madai hayo, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo, Dionis Myinga, amekemea vikali hali hiyo, akisema serikali haihitaji ukabila, na wala haiendekezi hali hiyo, kwa kuwa Tanzania ni ya wote, mtu yeyote anaweza akafanya kazi kokote.

Akizungumza jana na Nipashe, mmoja wa wananchi wa Nkuu Ndoo (jina limehifadhiwa), amesema Ijumaa ya wiki iliyopita, Halmashauri ya Kijiji hicho, wazazi na wananchi, walikutana kutafuta ufumbuzi wa malalamiko ya mmoja wa walimu kufanyiwa vitendo vya kishirikina.

Alipotafutwa kuzungumzia jambo hilo kama lina ukweli, Mwenyekiti wa Kamati ya Elimu, Kijiji cha Nkuu Ndoo, Elimwaria Mbora ameisema, hilo la kuomba kuhama, ni kweli waliomba; kwa sababu ya kero ambazo zilitokea.

Amesema kuna mzazi, mtoto alichapwa, baada ya huyo mtoto kuacha begi uwanjani Ijumaa. Mwalimu akaliokota, Jumatatu yake wakati anamkabidhi mtoto begi akamwadhibu.
 
Na Godfrey Mushi, Nipashe

"Tulikuja kubaini kwamba kuna mtu, ni mwanamke mmoja hivi, msichana tu; sasa si unajua watu wanapeleka maombi bwana! Sasa anapokataa kumbe ndo anafanyiwa vitendo hivyo. Imebainika iko namna hiyo.”

Alipotafutwa kuzungumzia jambo hilo kama lina ukweli, Mwenyekiti wa Kamati ya Elimu, Kijiji cha Nkuu Ndoo, Elimwaria Mbora ameisema, hilo la kuomba kuhama, ni kweli waliomba; kwa sababu ya kero ambazo zilitokea.

Amesema kuna mzazi, mtoto alichapwa, baada ya huyo mtoto kuacha begi uwanjani Ijumaa. Mwalimu akaliokota, Jumatatu yake wakati anamkabidhi mtoto begi akamwadhibu.

“Mzazi wake akaja juu akamshtaki kijijini, ndio ikabidi tuchukue hatua ya kulitatua kwa njia hiyo. Tukaweka siku, kwamba siku ya Ijumaa iwepo Halmashauri nzima ya kijiji na wazazi na walimu. Kwa hiyo ndio tukalitatua, tukaliongelea kwa pamoja.

Inaelezwa kuwa, walimu waliokuwa wameomba kuondoka, ni Mwalimu Mkuu, Mwalimu wa Taaluma na mwingine.

“Na ile shule tulikuta ina walimu watatu. Ndio tukamuuliza Ofisa Elimu wa Kata, inakuaje shule ina watoto 175 ina walimu watatu tu? Akatuambia hilo wameshalitatua, kuna walimu wawili watakuja, saa yeyote wataripoti,”amefafanua Mbora.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya hiyo, Dionis Myinga, alipoulizwa na Nipashe kwa njia ya simu kuhusu sakata hilo, ameonyesha kusikitishwa na madai ya wazazi hao kutaka walimu wazawa, amekemea vikali, akieleza sasa siyo zama za mtu anasema, namtaka huyu, simtaki huyu.

Cc: IPP Media
 
Serikali iwapangie kazi hao wajinga sehemu ngumu kuliko zote nchini wakajifunze tabia
 
Kuna shule moja huko moshi vijijini kata ya Arusha Chini/TPC Mkoani Kilimanjaro mi na mwenzangu kutoka Lushoto mkoani Tanga, mwenzangu huyo ni msambaa tulipangiwa shule tukakuta walimu ni wachaga watupu wa Kibosho na Uru tu, Tulitishika kidogo ila tulipata moyo kwa kuwa hata hao walimu si wazawa wa kijiji hicho kilichopo ukanda wa Moshi Chini, kule ni waarusha chini na wamasai nako jamii ya pale ilitamani sana kupata walimu wazawa wa eneo hilo. Baadaye mwenzangu alirudi kwao kwa uhamisho wa kubadilishana wilaya nikabaki peke yangu katikati ya wachaga, Bahati nzuri staff iligawanyika pande mbili hasimu mi nikawa neutral katikati ya walimu wachaga sikuogopa kutengwa na kubaguliwa sababu nilikuwa mkali mno kwenye ubaguzi wa kikabila kwa hoja kuwa mi ni mtanzania napangwa kazi mahali popote Tanzania. Kule Kilimanjaro kuna shule utakuta walimu ni wachaga tu au wapare tu. Akitokea ofisa elimu ni mchaga walimu wachaga hufurahia hali kadhalika akiwa mpare walimu wapare hufurahia wanaona watasikilizwa shida zao
 
😀😀😀
Halafu ndio ulikuwa mwalimu wa kiswahili na lafudhi yako hawakuelewi kabisa......
 
Mambo haya kufanyika zama hizi, inasikitisha sana. Nimegundua hii shida ipo zaidi vijijini kuliko sehemu za mjini zenye mchanganyiko wa watu
 
Huko huko Kilimanjaro vipo vijiji vina wakazi wake ni dini fulani wazazi hupenda zaidi watoto wao wafundishwe walimu wa dini yao. Sipati picha huko Pangani, Kilwa, Mafia, Mkuranga hali ikoje kwa mwalimu asiye wa dini ya wenyeji kufundisha watoto wao. Maeneo mengine ya nchi hali ni shwari hakuna ukabila wala udini, walimu ni changanyikeni
 
We kichwa panzi una udini sana
 
Kilimanjaro ina walimu wazawa wengi kwa sababu wanapopangiwa kazi kwa mara ya kwanza mikoani hurudi kwao kwa kubadilishana wilaya na walimu wa mikoani waliopangiwa huko uchagani/upareni, Uhamisho wa kubadilishana wilaya ni mrahisi sana kuliko ule wa kuomba kwa sababu maalumu. Walimu wasio wenyeji wa huko ni wa kuhesabu, wengi ni wazawa
 
Wafanyakazi wengi uchaggani hubaki wachagga kwasababu watu wengine hawaendi Kilimanjaro.

Hata wachagga wakipata mikoa mingime huwa hawarudi kufanya kazi kwao, labda kama wamepngwa Lindi, Mtwara au Kigoma, au Busokelo
 
Ila walimu nao hupenda sana kujitaftia matatzo wao wenyew sasa mtoto kusahau bag na kumkabidhi ni kitu cha kumchapa kweli mbna walimu wa tz wanapenda kuhamisha stress zao kwa wanafunzi me naona yote wanayapitia sawa tu Mungu nae anaamua kuwaadhibu kwa namna anayojua yeye
 
Kuhusu vitendo vya kishirikina kufanywa na wenyeji shuleni niliambiwa vipo ila sikuwahi kuona wala kufanyiwa zaidi ya kukuta material ya ushirikinikina chumba alipokuwa analala mwalimu mwenyeji niliyekuta amehama na mimi kulala hapo kwenye nyumba ya walimu, ikabidi nitoe material hayo ya kishirikina yaliyokuwa yanaaminika ni kinga ya wachawi kwa mwalimu aliyehama aliacha kinga zake alizoaminishwa na mganga wake. Mara niambiwe mti wa shule huwaka moto usiku wachawi huja kufanya kilinge hapo na kucheza ngoma zao ila sikuwahi kuona. Mambo ya kishirikina ukiyaedekeza yatakuathiri kisaikolojia kuwa unalogeka, utateseka bure
 
sasa kama mtoto ni mzembe asichapwe? Nitamchapa mpaka akili zimkae sawa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…