Kuna shule moja huko moshi vijijini kata ya Arusha Chini/TPC Mkoani Kilimanjaro mi na mwenzangu kutoka Lushoto mkoani Tanga, mwenzangu huyo ni msambaa tulipangiwa shule tukakuta walimu ni wachaga watupu wa Kibosho na Uru tu, Tulitishika kidogo ila tulipata moyo kwa kuwa hata hao walimu si wazawa wa kijiji hicho kilichopo ukanda wa Moshi Chini, kule ni waarusha chini na wamasai nako jamii ya pale ilitamani sana kupata walimu wazawa wa eneo hilo. Baadaye mwenzangu alirudi kwao kwa uhamisho wa kubadilishana wilaya nikabaki peke yangu katikati ya wachaga, Bahati nzuri staff iligawanyika pande mbili hasimu mi nikawa neutral katikati ya walimu wachaga sikuogopa kutengwa na kubaguliwa sababu nilikuwa mkali mno kwenye ubaguzi wa kikabila kwa hoja kuwa mi ni mtanzania napangwa kazi mahali popote Tanzania. Kule Kilimanjaro kuna shule utakuta walimu ni wachaga tu au wapare tu. Akitokea ofisa elimu ni mchaga walimu wachaga hufurahia hali kadhalika akiwa mpare walimu wapare hufurahia wanaona watasikilizwa shida zao