Kilimanjaro: Walimu shule nzima waomba uhamisho, kisa utata walimu wazawa

Huko huko Kilimanjaro vipo vijiji vina wakazi wake ni dini fulani wazazi hupenda zaidi watoto wao wafundishwe walimu wa dini yao. Sipati picha huko Pangani, Kilwa, Mafia, Mkuranga hali ikoje kwa mwalimu asiye wa dini ya wenyeji kufundisha watoto wao. Maeneo mengine ya nchi hali ni shwari hakuna ukabila wala udini, walimu ni changanyikeni
Watu wa Pwani ni wakarimu kwa kila mtu ila ubaya wao unakuja ikitokea umewachokoza au umewadharau kwa namna fulani ndio watataka wakuonyeshe jeuri ila kinyume na hapo ukiwa mtu peace utaenjoy sana hata vyakula utakuwa unaletewa bure na mke unapewa
 
Mambo haya kufanyika zama hizi, inasikitisha sana. Nimegundua hii shida ipo zaidi vijijini kuliko sehemu za mjini zenye mchanganyiko wa watu
Kwa upande wa mikoa ya kaskazini hadi mijini tabia zao ni hizo hizo.
Ukifungua biashara hawaji kununua hadi uwe mzawa wa huko na kama ni kazini hawakupi ushirikiano ili kazi uione ngumu uondoke.
Nilishawahi kuishi kaskazini tena maeneo ya town
 
Watu wa Pwani ni wakarimu kwa kila mtu ila ubaya wao unakuja ikitokea umewachokoza au umewadharau kwa namna fulani ndio watataka wakuonyeshe jeuri ila kinyume na hapo ukiwa mtu peace utaenjoy sana hata vyakula utakuwa unaletewa bure na mke unapewa
Umesema kweli
Watu wa Pwani hawana shida kabisa,
Utakaribishwa, hakuna fujo ni amani tu
 
Naunga mkono. Kaskazini sio mahali pazuri kwa wageni wa mikoa jirani kufanya kazi kwa uhuru. Wengi unakuta wanaongea kilugha muda wote.
 
Umesema kweli
Watu wa Pwani hawana shida kabisa,
Utakaribishwa, hakuna fujo ni amani tu
Exactly,kanuni yao hao huwa wanapenda tu uwe unawaongelesha hata kwa salamu hapo wanajisikia raha sana,hata kama uko bize basi angalau wikiendi ukiwa off upate muda wa kupiga nao stori hata masaa mawili hapo watakupenda sana na utalindwa hakuna atakayekuzingua hata kidogo
 
Naunga mkono. Kaskazini sio mahali pazuri kwa wageni wa mikoa jirani kufanya kazi kwa uhuru. Wengi unakuta wanaongea kilugha muda wote.
Wanaongea kilugha mara kwa mara na hawakuongeleshi na ukisema uwaongeleshe au kuwasalimia mtu anakuitikia huku amekunja ndita kwa sura ya makasiriko.
Yaani kule kaskazini ukiona mtu anaongea na wewe vizuri kwa ukarimu na tabasamu ujue anatokea Singida,Mbulu,au Tanga
 
walinishangaa lafudhi yangu kama wale wa Ngara mkoani Kagera, sikuwa mwalimu wa kiswahili japo naweza, nafundisha ngoma nzito maths na english
Bado uko ngara? Kuna jamaa anaitwa Mhina I guess alikuwa katoka Tanga alihamia shule moja nasoma huko bukoba, aisee alikuwa maarufu sana maana alivyokuwa anaongea kuanzia watoto hadi walimu alikuwa anawafurahisha kweli. Looking back tulikuwa tunafurahia anavyoongea hadi kumtania ila ndicho chanzo cha mtu kuhisi anabaguliwa ila ukweli ni kwamba si ubaguzi ila watu wanakuwa wanashangaa na kufurahia anavyo articulate maneno.
 
Kuna shule moja huko moshi vijijini kata ya Arusha Chini/TPC Mkoani Kilimanjaro mi na mwenzangu kutoka Lushoto mkoani Tanga, mwenzangu huyo ni msambaa tulipangiwa shule tukakuta walimu ni wachaga watupu wa Kibosho na Uru tu, Tulitishika kidogo ila tulipata moyo kwa kuwa hata hao walimu si wazawa wa kijiji hicho kilichopo ukanda wa Moshi Chini, kule ni waarusha chini na wamasai nako jamii ya pale ilitamani sana kupata walimu wazawa wa eneo hilo. Baadaye mwenzangu alirudi kwao kwa uhamisho wa kubadilishana wilaya nikabaki peke yangu katikati ya wachaga, Bahati nzuri staff iligawanyika pande mbili hasimu mi nikawa neutral katikati ya walimu wachaga sikuogopa kutengwa na kubaguliwa sababu nilikuwa mkali mno kwenye ubaguzi wa kikabila kwa hoja kuwa mi ni mtanzania napangwa kazi mahali popote Tanzania. Kule Kilimanjaro kuna shule utakuta walimu ni wachaga tu au wapare tu. Akitokea ofisa elimu ni mchaga walimu wachaga hufurahia hali kadhalika akiwa mpare walimu wapare hufurahia wanaona watasikilizwa shida zao
Sasa unafundisha wapi
 
Kila mtu arudi kwao ,dogo yuko Arusha eti nataka kufanya kazi mbali na nyumbani ..Anaumwa kaletwa anauguzwa hataki kurudi huko 😂😂unapendaje sehemu sio kwenu kama sio utumwa.
 
ukipangwa kazi usukumani utakula shushu, ni ofa kwa kwenda mbele, mara uletewe maziwa, mara nyama, mara matunda, each and everything they offering you.
Umesema wewe ni mwalimu wa English!!!!!! Hii ni hatari zaidi ya danger.

walinishangaa lafudhi yangu kama wale wa Ngara mkoani Kagera, sikuwa mwalimu wa kiswahili japo naweza, nafundisha ngoma nzito maths na english
 
Watu wa Pwani ni wakarimu kwa kila mtu ila ubaya wao unakuja ikitokea umewachokoza au umewadharau kwa namna fulani ndio watataka wakuonyeshe jeuri ila kinyume na hapo ukiwa mtu peace utaenjoy sana hata vyakula utakuwa unaletewa bure na mke unapewa
Hili la kukomeshwa na kufanyiwa jeuri ikiwemo vitendo vya kishirikina baada ya wenyeji kuona una dharau lipo sana tu huko vijijini. Wenyeji hawataki udharau mazingira yao. vyakula vyao, maji yao na hata mademu wao, watapenda ushiriki vitu vyao na upate demu wao kabisa watafurahi kuwa unawathamini
 
Huko huko Kilimanjaro vipo vijiji vina wakazi wake ni dini fulani wazazi hupenda zaidi watoto wao wafundishwe walimu wa dini yao. Sipati picha huko Pangani, Kilwa, Mafia, Mkuranga hali ikoje kwa mwalimu asiye wa dini ya wenyeji kufundisha watoto wao. Maeneo mengine ya nchi hali ni shwari hakuna ukabila wala udini, walimu ni changanyikeni
Wakati mwengine walimu dini flani wakisomesha shule zenye watu wa dini flani wengi kuna mambo wanafanya ya hujuma
 
Exactly,kanuni yao hao huwa wanapenda tu uwe unawaongelesha hata kwa salamu hapo wanajisikia raha sana,hata kama uko bize basi angalau wikiendi ukiwa off upate muda wa kupiga nao stori hata masaa mawili hapo watakupenda sana na utalindwa hakuna atakayekuzingua hata kidogo
hawanaga shida wale kama huwaoneshi dharau ila ukiwa unakulakula wake zao hovyohovyo watakushughulikia kwa njia yoyote wanayoona inafaa ikiwa ni pamoja na ushirikina
 
Wanaongea kilugha mara kwa mara na hawakuongeleshi na ukisema uwaongeleshe au kuwasalimia mtu anakuitikia huku amekunja ndita kwa sura ya makasiriko.
Yaani kule kaskazini ukiona mtu anaongea na wewe vizuri kwa ukarimu na tabasamu ujue anatokea Singida,Mbulu,au Tanga
mind kuwa Kilimanjaro yote si ya wachaga na wapare tu kuna vieneo vina makabila mengine kama wakahe, waarusha na wamasai huko ukanda wa chini moshi vijijini
 
Bado uko ngara? Kuna jamaa anaitwa Mhina I guess alikuwa katoka Tanga alihamia shule moja nasoma huko bukoba, aisee alikuwa maarufu sana maana alivyokuwa anaongea kuanzia watoto hadi walimu alikuwa anawafurahisha kweli. Looking back tulikuwa tunafurahia anavyoongea hadi kumtania ila ndicho chanzo cha mtu kuhisi anabaguliwa ila ukweli ni kwamba si ubaguzi ila watu wanakuwa wanashangaa na kufurahia anavyo articulate maneno.
Tulikuwa watatu tuliotoka chuo kimoja na eneo moja kupangiwa huko kwa Wahangaza. tuligeuka ni burudani kwao kwa rangi zetu na lafudhi ya kiswahili chetu. Msichana wetu tuliopangwa naye huko ndiyo walikuwa wanamshangaa zaidi kwa wajihi wake. Ngara wanaongea kiswahili cha lafudhi ya ajabu sana nasi tuliwashangaa vilevile
 
Back
Top Bottom