Kilimanjaro: Waliohusishwa na utekaji wa watu na kujitambulisha kama Usalama wa Taifa watiwa mbaroni

Hii si Tanzania ninayeijua mimi. Huku ndiko serikali iliyoko madarakani inakotupeleka.

Nasikia kuna swala humu Jamii F "Kama kuna anayejua hii serikali inakotupeleka". Majibu yapo tofauti ila uhakika ni kuwa ushahidi wa wapi dereva anatupeleka umo katika THREAD HII.
 
Ni ngumu kuamini kuwa walifanya haya bila baraka kutoka juu.
Waache watu wadanganyike. Hao watakuwa ni hawa TISS mazwazwa wa siku hizi. Wamewakana kiuongo. Mambo yataisha na watapangiwa kazi nyingine. Hivi ni vile vikosi vinavyozunguka kutesa na kuua watu wenye misimamo tofauti na Magufuli. Nadhani huenda walikuwa wanamfuatilia Mbatia kumkumbusha maagano na fedha aliyopewa alipoenda ikulu ili atengeneza upinzani fake. Kipindi hicho Magufuli na watu wake walishapiga mahesabu wakaona waitumie CUF na Lipumba na NCCR na Mbatia kutengeneza upinzani fake huku wakidhani Chadema imeshakufa na haitafufuka tena. Mbatia asipoangalia wanaweza kumuua kwani inaoneka ameshindwa kutimiza aliyoahidi wakati fungu alishakatiwa.
 
"Kitengo cha Maadili na Usalama Ofisi Ndogo ya CCM Lumumba" halafu wanateka watu!?

Hiyo ndo CCM mpya, yaani imejaa woga, uzandiki, unafiki, chuki, uongo, na kila aina ya ukatili.

Na hii imetokana na silika na hulka aliyonayo kinara wao wa chama yaani Meko.
Nadhani aliekimbia ni YEHODAYA.
 
Waache watu wadanganyike. Hao watakuwa ni hawa TISS mazwazwa wa siku hizi. Wamewakana kiuongo. Mambo yataisha na watapangiwa kazi nyingine. Hivi ni vile vikosi vinavyozunguka kutesa na kuua watu wenye misimamo tofauti na Magufuli. Nadhani huenda walikuwa wanamfuatilia Mbatia kumkumbusha maagano na fedha aliyopewa alipoenda ikulu ili atengeneza upinzani fake. Kipindi hicho Magufuli na watu wake walishapiga mahesabu wakaona waitumie CUF na Lipumba na NCCR na Mbatia kutengeneza upinzani fake huku wakidhani Chadema imeshakufa na haitafufuka tena. Mbatia asipoangalia wanaweza kumuua kwani inaoneka ameshindwa kutimiza aliyoahidi wakati fungu alishakatiwa.
Yeye anapewa hela za usajili anaenda kumsainisha Joseph selasini?
Yeremia Maganja?

Hawapati mbunge hata moja hawa Nccr mageuzi pia Cuf
 
Watu watatu waliokuwa wakimfuatilia mgombea ubunge jimbo la Vunjo kwa tiketi ya NCCR-Mageuzi, Ndg. James Mbatia wakiwa na gari aina ya Toyota Prado namba DFP 788 wamekamatwa na Jeshi la Polisi mjini Moshi jana saa 10 alasiri eneo la KDC baada ya Polisi kufukuzana na gari hilo na kufanikiwa kulidhibiti (block).

Mmoja wao alifanikiwa kukimbia baada ya kuona wamedhibitiwa lakini wawili walidhibitiwa na Jeshi la P

Watu hao waliokuwa wakijitambulisha maeneo mengi kuwa wao ni Usalama wa Taifa na wakati mwingine wakidai wao Askari wa Jeshi la Polisi hatimaye baada ya kukamatwa na kuhojiwa imedaiwa ni watu kutoka kitengo cha ‘Maadili na Usalama’ ndani ya CCM kutoka ofisi ndogo ya CCM Lumumba.

Baada ya kupekuliwa, watu hao walikutwa na nambari za magari tofauti tofauti na silaha mbalimbali zikiwamo koleo zinazodaiwa kutumika kuwatesa makada wa upinzani waliotekwa Vunjo na Moshi Vijijini na kuzua taharuki mkoani Kilimanjaro.

Wanaendelea kushikiliwa Central Police mjini Moshi.

View attachment 1599427
Hawa ndio walioweza kukamatwa

View attachment 1599428
Hizi ni nambari za magari zilizokutwa ndani ya gari lao

Mbatia akiongelea vitendo hivi [emoji1484]

View attachment 1599436

Ilivyotokea: Mnamo majira ya saa 10 za jioni kulitoka kurupushani katika ya msafara wa James Mbatia pamoja na watu waliokuwa na gari hilo hali iliyozua taharuki kubwa. Nguvu ya ziada iliongezwa na Jeshi la Polisi kituo kidogo cha Himo na kuanza kulifukuza gari hilo ili kuli-block jambo ambalo pia halikufua dafu kwani almanusura gari hilo liligonge gari la OCS wa Kituo cha Polisi Himo.

Polisi walilazimika kuongeza nguvu zaidi ya magari kutoka Kituo Kikuu cha Polisi Moshi - Kilimanjaro ndipo walipofanikiwa kulizuia gari hilo kwa kuziba barabara zote na kuwakamata watuhumiwa wawili kati ya watatu ambapo mmoja alifanikiwa kutoroka kwa kuruka Dirishani. Baada ya purukushani hizo zilizodumu kwa zaidi ya saa 2 ndipo gari hilo lilikutwa na Mapanga, Marungu, Sime, Mikuki, Jambia na plate number nne za magari tofauti.

Watuhumiwa wamejitetea kwamba wao ni usalama wa Taifa hata hivyo Idara hiyo imewakana haiwafahamu.

=====

Baadhi ya matukio wanayohusishwa nayo:

Septemba 9, 2020:

Watu wasiojulikana wakiwa na gari aina ya Toyota Prado lenye namba za DFP wanadaiwa kuwateka nyara makada wawili wa NCCR-Mageuzi jimbo la Vunjo kisha kuwatesa na mmoja kukatwa sikio lake la kulia.

Taarifa za uhakika zimewataja makada hao kuwa ni Yolanda Lyimo ambaye ni mgombea udiwani viti maalum na Deogratius Mosha ambaye ni kampeni Meneja wa mgombea udiwani kata ya Kilema kati, Gibras Riwa.

Vyanzo vya habari vinadai kuwa tukio hilo lilitokea juzi kati ya saa 12:00 na 1:00 usiku katika kijiji cha Mkyashi huko kata ya Kilema ambapo watu wasiojulikana, wakiwa na bunduki waliwateka makada hao.

Inadaiwa kuwa watu hao waliokuwa na gari aina ya Prado, walijitambulisha kwa makada hao waliokuwa na mazungumzo yao binfasi na watu wengine watatu, kwamba wao ni maofisa wa Jeshi la Polisi.

Kwa mujibu wa taarifa hizo, waliwachukua Yolanda na Deogratius na kuwaamuru wapakie kwenye gari kuwa wanakwenda kufanya nao mahojiano, lakini badala yake walilazwa kwenye gari hiyo.

Baadae katika eneo ambao hawakulitambua, watu hao walianza kuwatesa kwa kuwapiga ambapo Deogratius alikatwa sikio lake la kulia na baadae kutelekezwa kwenye pori lenye miba katika msitu Ghona.

Hata hivyo, waliweza kujikongoja umbali wa kati ya kilometa 3 hadi 4 hadi kijiji cha Ghona ambapo wananchi waliweza kuwapa msaada ikiwamo kupiga simu polisi Himo, ambao walifika na kuwachukua.

Yolanda kwa sasa ni mgombea udiwani viti maalum na katika mchakato wa uchaguzi mkuu 2020, alishiriki kura za maoni CCM kuwania Udiwani kata ya Kilema Kati lakini hakuteuliwa ndipo akajiunga na NCCR-Mageuzi.

Pia ni Diwani aliyemaliza muda wake katika kata hiyo hiyo lakini kupitia chama cha Tanzania Labour Party (TLP) wakati Deogratius yeye ni kampeni Meneja wa mgombea udiwani kata ya Kilema Kati

>>>>>

Tarehe 6 Oktoba 2020:

Vitendo vya kiharamia vya kuteka makada wa vyama, kuwatesa na hata kuwaua vimeanza kutikisa nchi baada ya makada wawili wa CHADEMA Wilaya ya Hai, kutekwa na kufanyiwa mateso makubwa.

Miongoni mwa mateso hayo ni kuingiziwa mti sehemu ya haja kubwa, kuminywa korodani kwa koleo, kujaribu kuwang’oa meno kwa koleo, mmoja kukatwa sikio na wote kuteswa kwa kupigwa na shoti ya umeme.

Makada hao walitekwa kata ya Narumu juzi na watu waliokuwa na magari ya kiraia matatu wakidaiwa kuwa na bunduki mbili na bastola moja, na baada ya mateso hayo, waliwatupa maeneo tofauti wilayani Arumeru.

>>>>>

Matukio wanayohusishwa watu ni mengi, tusubiri kuona mwisho wao utakuwaje
Hawa wanafanya kazi kwenye kitengo sawa na cha sabaya.
Sabaya mkuu wa wilaya ya hai aliwahi kamatwa kama hawa ila cha ajabu sasa hivi eti ni mkuu wa wilaya.
Kwa Tanzania ya leo niseme tu kwamba Idd Amini alikuwa na afadhali kwa sababu ya zama alizoishi.
 
Tuko busy kidogo na JamboLetu hapa Kawe
Kawe kuna nini tena huko?
mbona Gwajima anajilipua hajui maana ya Askofu ni Kiongozi wa Kiroho
anajifananisha na Alhaji Ali Hassan Mwinyi aliyeenda Hijja
Gwajima anajua majina ni kujipachika tu
Kawe mmeshikwa pabaya na Halima, hao wote wa Tanganyika Parkcers sio wapiga kura , mmepelekwa na magari
wenye vichionjio wanawaona subirini tarehe yenu
 
Ni kweli kumekua na utaratibu wa kila office ya CCM za kila mtaa kuandaa costa zinazotosheleza wanachama wake kuwapeleka kwenye shughuli za kichama na kuwarudisha majumbani

Wamejipanga kweli kweli
 
Watu watatu waliokuwa wakimfuatilia mgombea ubunge jimbo la Vunjo kwa tiketi ya NCCR-Mageuzi, Ndg. James Mbatia wakiwa na gari aina ya Toyota Prado namba DFP 788 wamekamatwa na Jeshi la Polisi mjini Moshi jana saa 10 alasiri eneo la KDC baada ya Polisi kufukuzana na gari hilo na kufanikiwa kulidhibiti (block).

Mmoja wao alifanikiwa kukimbia baada ya kuona wamedhibitiwa lakini wawili walidhibitiwa na Jeshi la P

Watu hao waliokuwa wakijitambulisha maeneo mengi kuwa wao ni Usalama wa Taifa na wakati mwingine wakidai wao Askari wa Jeshi la Polisi hatimaye baada ya kukamatwa na kuhojiwa imedaiwa ni watu kutoka kitengo cha ‘Maadili na Usalama’ ndani ya CCM kutoka ofisi ndogo ya CCM Lumumba.

Baada ya kupekuliwa, watu hao walikutwa na nambari za magari tofauti tofauti na silaha mbalimbali zikiwamo koleo zinazodaiwa kutumika kuwatesa makada wa upinzani waliotekwa Vunjo na Moshi Vijijini na kuzua taharuki mkoani Kilimanjaro.

Wanaendelea kushikiliwa Central Police mjini Moshi.

View attachment 1599427
Hawa ndio walioweza kukamatwa

View attachment 1599428
Hizi ni nambari za magari zilizokutwa ndani ya gari lao

Mbatia akiongelea vitendo hivi [emoji1484]

View attachment 1599436

Ilivyotokea: Mnamo majira ya saa 10 za jioni kulitoka kurupushani katika ya msafara wa James Mbatia pamoja na watu waliokuwa na gari hilo hali iliyozua taharuki kubwa. Nguvu ya ziada iliongezwa na Jeshi la Polisi kituo kidogo cha Himo na kuanza kulifukuza gari hilo ili kuli-block jambo ambalo pia halikufua dafu kwani almanusura gari hilo liligonge gari la OCS wa Kituo cha Polisi Himo.

Polisi walilazimika kuongeza nguvu zaidi ya magari kutoka Kituo Kikuu cha Polisi Moshi - Kilimanjaro ndipo walipofanikiwa kulizuia gari hilo kwa kuziba barabara zote na kuwakamata watuhumiwa wawili kati ya watatu ambapo mmoja alifanikiwa kutoroka kwa kuruka Dirishani. Baada ya purukushani hizo zilizodumu kwa zaidi ya saa 2 ndipo gari hilo lilikutwa na Mapanga, Marungu, Sime, Mikuki, Jambia na plate number nne za magari tofauti.

Watuhumiwa wamejitetea kwamba wao ni usalama wa Taifa hata hivyo Idara hiyo imewakana haiwafahamu.

=====

Baadhi ya matukio wanayohusishwa nayo:

Septemba 9, 2020:

Watu wasiojulikana wakiwa na gari aina ya Toyota Prado lenye namba za DFP wanadaiwa kuwateka nyara makada wawili wa NCCR-Mageuzi jimbo la Vunjo kisha kuwatesa na mmoja kukatwa sikio lake la kulia.

Taarifa za uhakika zimewataja makada hao kuwa ni Yolanda Lyimo ambaye ni mgombea udiwani viti maalum na Deogratius Mosha ambaye ni kampeni Meneja wa mgombea udiwani kata ya Kilema kati, Gibras Riwa.

Vyanzo vya habari vinadai kuwa tukio hilo lilitokea juzi kati ya saa 12:00 na 1:00 usiku katika kijiji cha Mkyashi huko kata ya Kilema ambapo watu wasiojulikana, wakiwa na bunduki waliwateka makada hao.

Inadaiwa kuwa watu hao waliokuwa na gari aina ya Prado, walijitambulisha kwa makada hao waliokuwa na mazungumzo yao binfasi na watu wengine watatu, kwamba wao ni maofisa wa Jeshi la Polisi.

Kwa mujibu wa taarifa hizo, waliwachukua Yolanda na Deogratius na kuwaamuru wapakie kwenye gari kuwa wanakwenda kufanya nao mahojiano, lakini badala yake walilazwa kwenye gari hiyo.

Baadae katika eneo ambao hawakulitambua, watu hao walianza kuwatesa kwa kuwapiga ambapo Deogratius alikatwa sikio lake la kulia na baadae kutelekezwa kwenye pori lenye miba katika msitu Ghona.

Hata hivyo, waliweza kujikongoja umbali wa kati ya kilometa 3 hadi 4 hadi kijiji cha Ghona ambapo wananchi waliweza kuwapa msaada ikiwamo kupiga simu polisi Himo, ambao walifika na kuwachukua.

Yolanda kwa sasa ni mgombea udiwani viti maalum na katika mchakato wa uchaguzi mkuu 2020, alishiriki kura za maoni CCM kuwania Udiwani kata ya Kilema Kati lakini hakuteuliwa ndipo akajiunga na NCCR-Mageuzi.

Pia ni Diwani aliyemaliza muda wake katika kata hiyo hiyo lakini kupitia chama cha Tanzania Labour Party (TLP) wakati Deogratius yeye ni kampeni Meneja wa mgombea udiwani kata ya Kilema Kati

>>>>>

Tarehe 6 Oktoba 2020:

Vitendo vya kiharamia vya kuteka makada wa vyama, kuwatesa na hata kuwaua vimeanza kutikisa nchi baada ya makada wawili wa CHADEMA Wilaya ya Hai, kutekwa na kufanyiwa mateso makubwa.

Miongoni mwa mateso hayo ni kuingiziwa mti sehemu ya haja kubwa, kuminywa korodani kwa koleo, kujaribu kuwang’oa meno kwa koleo, mmoja kukatwa sikio na wote kuteswa kwa kupigwa na shoti ya umeme.

Makada hao walitekwa kata ya Narumu juzi na watu waliokuwa na magari ya kiraia matatu wakidaiwa kuwa na bunduki mbili na bastola moja, na baada ya mateso hayo, waliwatupa maeneo tofauti wilayani Arumeru.

>>>>>

Matukio wanayohusishwa watu ni mengi, tusubiri kuona mwisho wao utakuwaje
Watu hao waliokuwa wakijitambulisha maeneo mengi kuwa wao ni Usalama wa Taifa na wakati mwingine wakidai wao Askari wa Jeshi la Polisi hatimaye baada ya kukamatwa na kuhojiwa imedaiwa ni watu kutoka kitengo cha ‘Maadili na Usalama’ ndani ya CCM kutoka ofisi ndogo ya CCM Lumumba.

Baada ya kupekuliwa.......
 
Safi sana police wetu. Wachunguzwe waeleze kila kitu na wengine wanaohusika wakamatwe woteee
 
Miongoni mwa mateso hayo ni kuingiziwa mti sehemu ya haja kubwa, kuminywa korodani kwa koleo, kujaribu kuwang’oa meno kwa koleo, mmoja kukatwa sikio na wote kuteswa kwa kupigwa na shoti ya umeme.
 
Baada ya kupekuliwa, watu hao walikutwa na nambari za magari tofauti tofauti na silaha mbalimbali zikiwamo koleo zinazodaiwa kutumika kuwatesa makada wa upinzani waliotekwa
 
Back
Top Bottom