kayanda01
JF-Expert Member
- Feb 14, 2014
- 1,216
- 1,062
Na mimi nasubiri mwenye uzoefu aje aelezee
Yes mkuu. Ngoja wenye uzoefu waje watupe ABCs kuhusu hili zao
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Na mimi nasubiri mwenye uzoefu aje aelezee
Swali zuri lenye lengo zuri nitachangia ushauri.Mbegu nzuri kwa uzalishaji fika maduka ya pembejeo kariakoo ulizia mbegu za kampuni ya royal( holand). Sifa kuu ya mbegu hizi ni uzalishaji mkubwa.Kuna mbegu za kampuni nyingine zenye sifa ya kuzaa mapema Zaidi ila uzalishaji ni kidogo kulinganisha na nilizokutajia.Yes mkuu. Ngoja wenye uzoefu waje watupe ABCs kuhusu hili zao
Swali zuri lenye lengo zuri nitachangia ushauri.Mbegu nzuri kwa uzalishaji fika maduka ya pembejeo kariakoo ulizia mbegu za kampuni ya royal( holand). Sifa kuu ya mbegu hizi ni uzalishaji mkubwa.Kuna mbegu za kampuni nyingine zenye sifa ya kuzaa mapema Zaidi ila uzalishaji ni kidogo kulinganisha na nilizokutajia.
Samadi yafaa Zaidi kuliko mbolea za kisasa kwa ajili ya urutubishaji shamba,kutunza unyevu na wingi wa mazao.
Kupanda kwa vipimo sahihi vitakuongezea tija.Jambo muhimu zingatia muda sahihi wa kupanda kwa kuangalia mahitajio ya soko.Kwa ukanda wa pwani hiki ni kipindi sahihi.Hongera kwa kufikiri cha kufanya kutatua changamoto badala ya kulalamika.Utakapofanikiwa rejesha taarifa ili kuwatia moyo waliokata tamaa na kusubiri miujiza ya mafanikio iwadondokee.
Muhimu watembelee wakulima wabamia
Amina.Barikiwa kwa kubariki wengine.Mkuu Hwasha, nasema ahasante sana ndugu kwa mchango wako mzuri.
Endelea na moyo huo wa kugawa taarifa kwa wenye uhitaji. Ubarikiwe sana mkuu
Hakika nitaleta mrejesho hapa nikiitekeleza hii shughuli
Wakuu ningependa kujuzwa kuhusu kilimo cha bamia
1. utaratibu wake wa kulima.
2. Ni kilimo cha muda gani
3. gharama za hiki kilimo kwa ujumla hasa kwa heka moja.
4. maeneo mazuri ya kulimia.
5. soko lake likoje
6. na mwisho mrejesho wake wa mapato unakuaje
MWENYE UFAHAMU WA HILI SWALI NAOMBA MSAADA.
Asante mkuu
- Unalima kama kawaida kwa tractor, ng'ombe nk
- Ni kilimo cha mwaka mzima hasa kama una maji ya kumwagilia japo linahitaji maji kidogo.
- Wangalau kwa heka moja unaweza kuotesha kilo moja ya bamia, kwa Arusha unaweza kuipata mbegu yake kwa shilingi 20,000 aina ni PUSA SAWAN. Hapo utaweka na bei ya kulima kwa heka kuanzia 20,000-50,000 kutegemeana na mahali ulipo. Dawa nzuri ya kulinda wadudu wa mmea huu ni Multmectin Plus. Mbolea ya kiwandani ama ya samadi ukipenda.
- Maeneo mazuri ya kulima zao hili ni maeneo yenye joto hasa ukanda wa pwani.
- Soko lake ni zuri hasa kwa wakazi wa pwani hiki ni kiungo kizuri cha mboga na wengi wao hafanya kama mboga kabisa. Wangalau ndoo moja ya kilo 20 ni shilingi 12,000-20,000 kutegemeana na msimu na eneo husika.
- Ni zao ambalo haliwezi kukupa hasara hata kama faida yake inaweza kuwa isiwe kubwa.
Ukichukua hatua itakuwa safi sanaAsante mkuu
Soon ntaanza kilimo hiki
love without limits
- Unalima kama kawaida kwa tractor, ng'ombe nk
- Ni kilimo cha mwaka mzima hasa kama una maji ya kumwagilia japo linahitaji maji kidogo.
- Wangalau kwa heka moja unaweza kuotesha kilo moja ya bamia, kwa Arusha unaweza kuipata mbegu yake kwa shilingi 20,000 aina ni PUSA SAWAN. Hapo utaweka na bei ya kulima kwa heka kuanzia 20,000-50,000 kutegemeana na mahali ulipo. Dawa nzuri ya kulinda wadudu wa mmea huu ni Multmectin Plus. Mbolea ya kiwandani ama ya samadi ukipenda.
- Maeneo mazuri ya kulima zao hili ni maeneo yenye joto hasa ukanda wa pwani.
- Soko lake ni zuri hasa kwa wakazi wa pwani hiki ni kiungo kizuri cha mboga na wengi wao hafanya kama mboga kabisa. Wangalau ndoo moja ya kilo 20 ni shilingi 12,000-20,000 kutegemeana na msimu na eneo husika.
- Ni zao ambalo haliwezi kukupa hasara hata kama faida yake inaweza kuwa isiwe kubwa.
Soko lake liko wapi hasa mkuu
Mimi nalima bamia sana horohoro Tanga, huwa napeleka Mombasa na Tanga. Pia masoko madogo madogo wananunua sana kwani bamia ni mboga yao kuu.