Kilimo cha maembe ya kisasa

Kilimo cha maembe ya kisasa

BARA BARA YA 5

JF-Expert Member
Joined
Sep 11, 2009
Posts
1,174
Reaction score
835
Katika hekaheka za kujiandaa kustaafu miaka 7 baadae nimeamua nipande miche kama 500 yaani ekari 10 za maembe kisasa.

Shamba lipo Tabora kwa sasa naendelea kuchimba mashimo. Nitapanda bila mbolea ya samadi ila taweka NPK baada ya miezi 3 ikiwa imeshika.

Mpango wangu miche 450 ipone ili nipate wastani wa embe 500 kila mti mwaka wa 6 na hii itanipa embe 225,000 na kama tauza kwa Tzs 400 nipate 90m.Hapo nitaamua kustaafu kazi nikiwa na miaka 55.
 
Good.
Ila mi nashauri upande na ya kienyeji ila uyapande kisasa. Mfano embe bolibo na embe dodo ni maembe mazuri yanayopendwa Tanzania.
Kitu kingine kwa uzoefu wangu wa kupanda miti ya matunda, ili upate idadi ya miti uliokusudia zidisha miche halafu ikishika ikikua una punguza miti na kubakiza idadi unayotaka.
heka badala ya miche 80 panda 100.
Miti mpaka ije ifungane unakuwa ushavuna mara kadhaa ndio unaipunguza.
 
Ushauri mzuri, kwenye kienyeji ni kweli ila tunataka tuwahi kurejesha capital. Kuhusu kupunguzia nakubaliana na wewe.
 
Miembe ya kisasa inahitaji sana dawa ili update embe nzuri. Nakushauri panda ya kienyeji. Nina miembe ya kienyeji ya Maembe dodo ni matamu na makubwa balaa. Situmii dawa yoyote na ninavuna Maembe kila mwaka pia yana soko kubwa ukienda sokoni
 
Expectation zako mkuu.
Walanguzi wa maembe wakija shambani kwako wanalangua mti mzima na sio embe moja moja eti embe ni shilling mia 4. Mkuu labda uwatafute wanunuzi masokoni na huko madalali sokoni ni shida. Kumbuka kupulizia dawa vibarua wa namna ya kuchuma maembe ili yawe na ubora sokoni ushindane na wengine
 
Good.
Ila mi nashauri upande na ya kienyeji ila uyapande kisasa. Mfano embe bolibo na embe dodo ni maembe mazuri yanayopendwa Tanzania.
Kitu kingine kwa uzoefu wangu wa kupanda miti ya matunda, ili upate idadi ya miti uliokusudia zidisha miche halafu ikishika ikikua una punguza miti na kubakiza idadi unayotaka.
heka badala ya miche 80 panda 100.
Miti mpaka ije ifungane unakuwa ushavuna mara kadhaa ndio unaipunguza.
Hii ya kienyeji inachukua muda gani hadi kuanza kuzaa tofauti na ya kisasa inayozaa baada ya miaka 3
 
Back
Top Bottom