lumia21
JF-Expert Member
- Nov 30, 2015
- 273
- 252
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Sorrry mkuu. Naomba unielekeze suala la kilimo cha matuta mkuu.kwenye hivo vijaruba unavyo viaandaa,mbegu za maarage zinapandwa katika mistar? Na kuhusu umwagiliaji upoje hasa eneo ambalo maji yanaweza kutiririka bila pump, je ni lazima nitumie pump? Na kama sitotumia pump, ntamwagilia kwa staili ip kwenye hivo vijaruba?Ingia kazini mkuu, usikatishwe tamaa na watu pengine wanakupa wrong information. Naamini ukilima muda huu utakutana na soko zuri kabla wakulima wa kanda ya ziwa hawajaanza kutoa mzigo na ili u tackle challenges zote ni pale utakapokuwa fully knowledgable na mazingira yako throughout the year.
Kikubwa imarisha huduma na fuata ushauri toka kwa wataalam kadri ipasavyo.
Mkuu ni kama unajichanganya katika uulizaji wa swali lako.Sorrry mkuu.naomba unielekeze suala la kilimo cha matuta mkuu.kwenye hivo vijaruba unavyo viaandaa,mbegu za maarage zinapandwa katika mistar? na kuhusu umwagiliaji upoje hasa eneo ambalo maji yanaweza kutiririka bila pump,je ni lazima nitumie pump? na kama sitotumia pump,ntamwagilia kwa staili ip kwenye hivo vijaruba?
Naomba unielekeze mkuu Kisima
Mkuu ni kama unajichanganya katika uulizaji wa swali lako.
Umesema maji yana uwezo wa kutililika pasipo msaada wa water pump; hapa nafikiri ni wewe kuyaelekeza yapite vipi kwenye majaruba au matuta yako kutegemea na ulivyo andaa shamba lako.
Hapa kinachotakiwa ni kuweka kingo katika kila tuta au majaruba yako uliyo andaa kwa vipimo maalum.
Katika kila kijaruba au matuta yako utapanda punje za maharage kwa uwiano wa vipimo sahihi cm20 umbali wa shimo kwa shimo na cm50 umbali wa mstari moja hadi mwingine kwa kupanda punje mbili kila shimo.
Mkuu hapa tunaongelea kilimo cha umwagiliaji so lazima uwe na enhanced facilities kuruhusu unyweshaji wa maji kwenye mmea.shukrani saana mkuu kwa majibu murua.ila ningependa kujua faida ya kilimo cha vijaruba ukilinganisha na kile kilimo kilicho zoeleka cha ulimaji maharage
Ni kilimo cha umwagiliaji mkuu..maana ni kilimo pekee chenye uhahkika wa mavuno. Nashkuru saaana kwa elimu uliyo nipatiaMkuu hapa tunaongelea kilimo cha umwagiliaji so lazima uwe na enhanced facilities kuruhusu unyweshaji wa maji kwenye mmea.
Huwezi ukalima in a scartered or misallocated way then ukamudu kumwagilia eneo kubwa kwa kiasi kidogo cha maji.
Hivyo basi ili kumudu upotevu wa maji, lazima u draft shamba lako katika namna ambayo litaruhusu mtiririko wa maji through gravitational effect. Hii ni njia ambayo ni common sana inajulikana kama furrow irrigation method.
Unaweza pia uka opt kutumia drip lines ambayo ni ghari sana kufanya complete installation kwa shamba la ekari moja.
Kifupi sijaelewa mkuu unataka kufanya kilimo cha namna gani? kama unategemea mvua, basi unaweza kulima kikawaida kama ilivyo zoeleka pasipo kukiuka vipimo na taratibu zote za matunzo ya zao husika ili upate mavuno bora.
Nakukaribisha!
Ok kila la kheri katika harakati zao mkuu!Ni kilimo cha umwagiliaji mkuu..maana ni kilimo pekee chenye uhahkika wa mavuno.nashkuru saaana kwa elimu uliyo nipatia
Ahsante saana mkuu.Ok kila la kheri katika harakati zao mkuu!
Nimeuza 2000kg bora ningeleta dar kumbe
Dar bei inacheza 1650 -2200 kwa kiloKwa sasa maharage ya njano yana range bei Tshs 1500-1700 kwa kilo , kama huna haraka yakuuza tulia nayo kwasababu kuna kipindi bei itafika hadi Tsh 4000 kwa kilo.
Then it means sokoni ni 2300 - 2600
habari mkuu... I like your plan.Mkuu Kisima habari yako.
Binafsi mwezi uliopita nilijaribu kuanza kulima harage la njano. Nilianza na nusu heka,sasa hivi yashaanza kutoa maua. Nilifikia uamuzi huu baada ya kugundua asilimia kubwa ya wakulima wanalima kienyeji sana hivyo ubora wa maharage unakuwa mdogo.
Huwa nanunua maharage kwakiasi kikubwa toka kwenye soko la mazao na kuyasafirisha Dar. Changamoto kubwa ya biashara hii ni endapo mzigo wako ukipata competition ya ubora na mizigo mingine,hapa itabidi ushushe bei kidogo. Kwa upande wa maharage ya njano,mikoa ya Arusha na Tanga ndio wanaongoza kwa ubora then Lilondo na Madaba (Ruvuma). Harage la njano la Songea mjini nilipolifikisha Dar liliuzwa kwa 1700 per Kg,wakati ya Lilondo ni 2000 per Kg na Arusha na Tanga ni 2200 - 2400 per Kg.
Kinachotofautish bei ni unene na ubora wa harage. Utafiti wangu ndio umenifanya nijaribu kulima mwenyewe (nimeanza na nusu heka) ila hapo baadae nitaingia miguu yote miwili pindi nikikamilisha utafiti. Wakulima wengi wanakwepa gharama za utunzaji na uendeshaji kilimo. Ila kama utapanda na kufata taratibu zote za uwekaji mbolea na upuliziaji dawa,nna uhakika outcomes ni nzuri na zao litakuwa bora (hiki ndio nataka nikifanye) then nisafirishe direct hadi Dar.
Ila kwa upande wangu nataka nifanye kilimo cha umwagiliaji,hapa namaanisha nikivuna kwenye ili jaribio langu mvua ndio zitakuwa zinaanza. Nitatulia kwanza then nisubirie kununua kwa wakulima wengine kama kawaida. Then nitaingia shambani tena mwezi wa 3 mwishoni mvua zikianza kupungua ili niexecute plan yangu.
Nikirudi kwako mkuu@kisima, pamoja na mchanganuo uliotutolea kwa upande wako. Ila itakuwa vizuri ukituonesha na picha walau tuone hayo matuta yanakuwaje,upandaji wa hizo mbegu umekaaje na mfumo mzima wa hizo pump za umwagiliaji upoje ili walau tuwe na clear image vichwani mwetu.
Shukrani.
Sent using Jamii Forums mobile app
Shukrani mkuu. Mdogo mdogo ndio mwendo,ngoja tujikongoje.habari mkuu... I like your plan.
Japo ni muda lakini ninaamini utaiona comment yangu.1) Natumia 6ltr@acre
2) kawaida namwagilia mara 10 mpaka kuvuna maharage kulingana na hali ya hewa.(6ltr*10=2500*6*10=>150,000/-)
3) natumia mbolea ya CAN Kg50@are=>Tsh90000
4)Tsh200,000 kulima na kuchora muelekeo wa utiririkaji wa maji.
5)booster 2ltr@6000=>12,000
6)fungicide=>40,000
7)insecticide=>48,000
8)mbolea supergro tsh 250,000.
9)palizi nafanya mwenyewe
10) navuna na kupokea mkwanja nikiwa shamba. Siku hiyo lazima nichinje jogoo kwajili ya mteja!
Karibuni sana shamba.
Ukiamua kuchagua upande huu utakuwa njia sahihi.
Usimtegemee mwajiri wako maana anakutumia kwa ujira finyu na ukizeeka hatakuhitaji kamwe.
Janjaruka mwanangu usiwe poyoyo!!