Mkuu umenena vyema, kununua miche mara nyingi utapata hadi asilimia 30 madume ambayo Kwa hakika ni hasara kwani unatumia muda wa hadi miezi mitatu kubaini kama ni dume ilihali umepoteza raslimali nyingi.
Acha story za kufunga magunzi ya mahindi au kukata eti itabadilika, haina ukweli.
Mkuu,
Miye nimekwisha fanya kosa hili. Nilinunua miche toka kwa wauzaji wa barabarani. Nina miche kama 14 hivi nyumbani na nimeipanda kama 'shamba darasa' kwa ajili ya mradi mkubwa nitakaoufanya baadaye.
Kwa sasa miche inakaribia miezi 2 ila bado sijajua ipi ni jike (itakayoniletea matunda) na ipi ni dume (hasara). Kuna namna rahisi ya kuitambua ikiwa na umri kama huo wa miezi miwili?
Asante.