Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Habari,Mkuu hatua uliyofikia ni kubwa sana huitaji kupunguza uzalishaji kwa kuhofia soko Bakresa anatoa bei nzuri sana kwa matikiti last time ilikuwa 800 TZS per kg ila ananunua minimum 250 tones so kama una eneo kubwa kacheki nao ustrike hiyo dili then uongeze uzalishaji
Ninayo business plan ya kilimo cha water melon!.. Ila iko planed zaidi kwa infrastructure za Dodoma cjui kama itakufaa!..
Naweza kukukodisha eka moja kwa Tsh 60,000/ unanilipa kabla, shamba lipo Pwani ya Mkuranga,maji yapo mengi sana,banda la kuishi kijana lipo. Unaweza pata eka hata 15 zilizo kando ya maji ya kudumu.
Please naomba unitumie contact zako kwenye PM
Zaidi ya 80% ya matajiri duniani ama wametajirika kwa ukulima ama wametajirika kwa mazao ya ukulima.
2kg pack @ Tsh 2,200/=
5kg pack @ Tsh 4,200/=
Popote tu mkuu alimradi usiwe udongo wa mfinyanzi. Huo ukanda wa Pwani tikiti linastawi tu vizuri ila usilime wakati wa mvua, matikiti hayapatani na mvua, inabidi iwe wakati wa kiangazi na iwe Kwa kumwagilia.Mie nataka kulima Mtwara je inawezekana????
Waheshimiwa ina maana hakuna mwenye kujua na kunisaidia katika jambo hili? Msaada wenu tafadhali
Tembelea thread hii hapa inazungumzia kilimo cha tikiti...
https://www.jamiiforums.com/ujasiriamali/125043-kilimo-cha-tikiti-maji.html
Habari zenu wadau.
Wakuu mimi nataka kujaribu kulima tikiti maji kipindi hiki cha masika. Nitafanya kilimo cha kisasa. Mbegu ni Sukari F1 hybrid.
Tatizo nimekuwa nikipata ushauri tofauti kuhusu kipindi hiki ambacho masika inakaribia kuanza (Takribani mwezi mmoja baadaye) Wengine wanasema Matikiti hayapendi mvua nyingi, wengine wanasema kama nitayahudumia kwa madawa hakutakuwa na tatizo.
Wakuu naombeni mawazo yenu, je inawezekana nikafanikiwa kuvuna kipindi hiki cha masika?
Natanguliza Shukrani.
Kilimo kina changamoto nyingi sana, nikuulize swali, wewe unataka kulimia wapi? Je ni huku Pwani au mikoani? Ninachojua, tikiti la masika linasumbua ila likitoka soko lake ni kubwa balaa, kiasi kwamba unaweza dhani ulichelewa wapi, ila ukikosea step kidogo tu,kilio chake hakichukuliki.
Nijibu hayo maswali kwanza.