Drip irrigation ni somo refu sana, so inabidi nijipange sana ili kuelezea kitu kinachoeleweka. Ila kwa kifupi, kuna mambo machache ya kuzingakita kama ifuatavyo:
1) Umbali kati ya mche na mche (Plant Spacing)
Umbali kati ya mche na mche kwa zao la matikiti maji hutofautiana kutokana na ulimaji. Kuna wengine huacha umbali wa 1.8 - 2.0m kati ya shimo na shimo na kila shimo wanaacha miche mitatu hadi minne. Kuna wengine wanaacha nafasi ya 1.0m na wanaweka miche miwili kila shimo.
Binafsi nilikua nataka kujaribu kuacha nafasi ya 0.5m na kuacha mche mmoja kila shimo, ingawa kuna wengine wanasema unaweza ukaacha umbali wa 0.3 - 0.4m kwa kila mche. Mimi nimeshawahi kuacha nafasi ya 1.5m kati ya shimo na shimo na kila shimo niliacha miche mitatu.
Unapochagua drip tapes (ambayo ni mipira midogo yenye matundu) unatakiwa uzingatie umbali kati ya mmea na mmea kutokana na ulimaji wako. Kuna drip tapes zenye umbali wa 10cm ~ 30cm na kuendelea. Ila ambazo zinapatikana sana ni zile za 20cm and 30cm.
Hivyo, kama unataka uache umbali wa 1.5m kati ya shimo na shimo basi utapata wakati mgumu sana kupata drip tapes zenye umbali huo.
Kama unataka kulima tikiti maji, tafuta drip tapes za 30cm spacing na unaweza ukaruka tundu (dripper) moja kila baada ya mche. Hii itafanya umbali kati ya mche na mche kuwa 60cm.
2) Ukubwa wa mabomba (Main and Sub-main Pipe Sizes)
Kwenye drip irrigation unatakiwa utumie mabomba kuendana na kiasi cha maji kinachohitajika shambani. Kadiri maji yanavyohitajika kwa wingi ndio unavyolazimika kutumia mabomba makubwa. Kwa ekari moja unaweza tumia sub-main yenye ukubwa wa 2" hadi 2.5" kutegemeana ma mwinuko wa shamba.
3) Kiasi cha maji kinachohitajika (Water consumption)
Unalazimia kukokotoa kiasi cha maji kinachohitajika shambani ili uweze kutengeneza ratiba yako ya umwagiliaji. Kwa mfano, kama shamba lako lina miche 4,000 na kila mche mmoja unatakiwa kiasi cha maji cha lita 2 kwa siku, basi shamba lako kwa siku litahitaji lita 8,000. Kama unamwagilia mara mbili, basi asubuhi lita 4,000 na jioni lita 4,000. Hii itakufanya uwe na ratiba mbili kwa siku.
Kama ratiba ya asubuhi hufanyika ndani ya saa moja, basi inabidi uwe na mabomba (main and sub-main) ambayo yanaweza kupitisha lita 4,000 za maji kwa saa. Pia lazima uwe na pump yenye uwezo wa kusukuma kiasi hiki cha maji kwa saa katika presha inayotakiwa. Drip system nyingi hutumia pressure ya 0.7 - 1.0bar. So pump yako lazima iweze kusukuma kiasi cha lita hizo kwa saa kwa msukumo wa 1.0bar.
Pia, drip tapes zako lazima ziwe na matundu yenye flow rate ya 1 litter per house (1lph) at the operating pressure. (could be 0.7 ~ 1.0bar depending on dripper construction)
Kama nilivyokwisha sema, mambo ni mengi kwenye drip irrigation. Ila kwa leo naomba niishie hapa. Kama una swali uliza tuelimishane taratibu.