Kilimo cha matikiti maji (watermelon): Ushauri na Masoko

Kilimo cha matikiti maji (watermelon): Ushauri na Masoko

kaka Edmund naomba uni PM tuwasiliane zaidi unipe experience yako nna interest ya kuingia huko kwenye kilimo cha matikiti. Currently nalima vitunguu kidogo kidogo so nahitaji kufahamu kilimo cha matikiti kilivyo and so far una experience ya kutosha

Habari, nilikua naomba tuwasiliane kuhusu hii habari ya vitunguu nahitaji mwanga kidogo jinsi ya kuanza na maeneo yanyofanya hiki kilimo hapa tanzania 0718 684565.
Natanguliza shujrani zangu!
 
Samahani jamani hapa tunaelimishana kuna wengine tunajifunza humu! Sasa mkianza ku PM mtakuwa mnakosea sana kwani lengo si ubinafsi!

Wako sahihi mkuu, vitu vinajadiliwa hapa, lakini inafika muda mtu labda anataka akajifunze kwa mwenzake, huwezi kuomba namba ya simu iwekwe hapa na anwani za mtu anaishi wapi mtaa gani nyumba namba ngapi!!!!!! kama una swali unauliza hapa watu wanarespond tu Mkuu.
 
Kaka tikit inahitaj ardhi yenye kupenyeza maji kwa urahis kwa Maana ardhi ya kichanga .mkuu usijaribu arusha utapoteza
 
Wadau nataka kuanza kilimo kikubwa cha matikiti, ninaanza na eka 100 morogoro,ni kilimo cha umwagiliaji.

Naomba wadau mnipe ushauri juu ya faida, soko na changamoto za kilimo hiki sina uzoefu wa kutosha.na pia ghrama zake za uzalishaji kwa eka.

Na pia nataka kulima heka 200 za sweetsourghum (mtama) amabao unanunuliwa makampuni ya bia kama TBL pia naomba ushauri juu ya hili, has faida na bei kwa kila soko na mavuno kwa kila heka.

Ahsanteni!!

mtama unatengenezea chibuku TBL wnanunua shayiri,ni jamii ya ngano
 
Niko kikazi ushirombo mkoani geita ila ninawazo la kuanza kulima matikiti maji, je kwa wenye kujua hili eneo linafaa kwa hiki kilimo(ni eneo ambalo hulimwa mahindi na mpunga).Je ni maeneo yapi yanafaa kwa kilimo cha matikiti maji?
 
Mimi nalima aina ya Sugar baby inachukua siku 60 tu kuvuna tangu plus siku 3-5 za kukaa ardhini, kwa hiyo kwa mwaka nalima mara 4 tu nina ekari 5 na kila eka napata kuanzia 2M-3M.

Spacing ni 2mx2m na kila shimo naweka mbegu 2 ambazo zinazaa matunda 2-3 kwa maana kila shimo napata matunda 4-6 ( wastani matunda 5).

Hivyo kwa spacing hiyo napata mashimo 1000-1200

Idadi ya matunda: Mashimo x Matunda kwa shimo x ekari [1,000 x 5 x 5 = 25,000]

Mapato: wastani wa shilingi 500 kwa tikiti x idadi ya matikiti kwa eneo la ekari 5 [25,000 x 500 = 12,500,000]

Mapato kwa mwaka: 12,500,000 x 4= 50,000,000

Gharama za uendeshaji wa shamba ni Tsh 25,000,000

Faida Kuu ni Tshs 25,000,000 M.

Tujenge taifa letu kwa kilimo


Edmund post yako ni nzuri, mimi mwaka juzi nilishawishika kufanya hicho kilimo lakini eneo lenyewe halikuwa na mto, nilichimba kisima kirefu (bore hole) nikiamini umeme ungefika mapema lakini hadi leo ni bila bila
 
Edmund post yako ni nzuri, mimi mwaka juzi nilishawishika kufanya hicho kilimo lakini eneo lenyewe halikuwa na mto, nilichimba kisima kirefu (bore hole) nikiamini umeme ungefika mapema lakini hadi leo ni bila bila

Mkuu usiniambie Umeme ndo kikwazo kwani huwezi pata generator la kuendeshea hicho kisima?
 
JF ni kila kitu! Asante sana Wadau' nina eneo langu kubwa hapa Dar, panafaa kwa kilimo hiki' hila tatizo ni maji!
 
JF ni kila kitu! Asante sana Wadau' nina eneo langu kubwa hapa Dar, panafaa kwa kilimo hiki' hila tatizo ni maji!

Tafuta solution mkuu kwa kufikiri nje ya box. Hakuna tatizo lisilokuwa na suluhisho unless uamue kulikumbatia peke yako na kuendelea kufikiria kitatizotatizo badala ya kufikiri kisuluhishosuluhisho. Sorry, huenda ninasound very theoretical kwako lakini huo ndio ukweli mkuu.
 
Mkuu,

Kwanza samahani sana kwa kuchelewa kujibu swali lako. Nimekua mvivu sana wa kuingia JF kutokana na kutingwa kwa shughuli za hapa na pale.

Kwanza kabisa nisingependa kukushauri silime nusu ekari, ni kidogo sana. Kama upo karibu sana na soko, basi haina shida, ila kama unaishi mbali na soko, kulima eneo dogo kunaweza kukufanya upate hasara kutokana na gharama kubwa ya usafiri.

Kadiri unavyokua na mzigo mkubwa, gharama kwa tonne (cost per tonne) ndivyo inavyoshuka na kukuwezesha kupata faida zaidi. Hivyo ukilima eneo dogo, gharama ya kusafiri itakuumiza.

Pili, gharama za kilimo zinategemea sana na aina ya kilimo unachofanya. Maswali ya kujiuliza ni kama ifuatavyo:

1. Je, unatumia kilimo cha kisasa au bora liende?
2. Je, unamtumia bwana shamba?
3. Hapo unapolima, unatumia trekta? Trekta lipo umbali gani toka shambani?
4. Unatumia mbolea ya namna gani? Mbolea inapatikana umbali gani toka shambani?
5. Hapo unapolima kuna vibarua wa kutosha wanaojua kuhudumia matikiti maji?
6. Eneo unapolima, hali ya uchumi ipoje? Hali ya uchumi ikiwa juu, gharama ya vibarua itakua juu pia.
7. Unafanya kilimo cha umwagiliaji au unategemea mvua?
8. Kama unamwagilia, je unatumia mashine ya aina gani? Au unamwagilia kwa mikono?

Na mambo mengineyo mengi.

Kwa ujumla, mambo kama hayo hapo juu hufanya maeneo tofauti kua na gharama tofauti. Hivyo uchaguaji wa eneo ni kitu muhimu sana kabla ya kuanza kulima.

Mimi nilishalima mkuranga mara kadhaa, na za kilimo kwa ekari zilikua around laki saba hadi nane.

Kama wahitaji kujua zaidi, niulize.

I hope that helps.

mi nahitaji kujua zaidi mkuu..nipo kyela..mbegu bora ni ipi kwa hali ya jua kali..
 
Wadau nataka kuanza kilimo kikubwa cha matikiti, ninaanza na eka 100 morogoro,ni kilimo cha umwagiliaji.

Naomba wadau mnipe ushauri juu ya faida, soko na changamoto za kilimo hiki sina uzoefu wa kutosha.na pia ghrama zake za uzalishaji kwa eka.

Na pia nataka kulima heka 200 za sweetsourghum (mtama) amabao unanunuliwa makampuni ya bia kama TBL pia naomba ushauri juu ya hili, has faida na bei kwa kila soko na mavuno kwa kila heka.

Ahsanteni!!

Mkuu Nina kitabu cha Kilimo cha matikiti maji PM me for details
 
Jamani habarini za wkend.., naomba kujua mche wa tikiti maji unaweza kuvunwa mara ngapi matunda yake?

Kwa mfano embe zinavunwa kila mwaka, ndizi unavuna mara moja tu na mche unakwisha kazi yake. Vipi kwa matikiti maji, unavunwa mara ngapi na kwa kipindi/interval gani?

Nataka kulima, yanalipa sana nisaidieni tafadhali.

Mkuu Nina kitabu cha ukulima wa matikiti incase ukiitaji
 
Back
Top Bottom